Sijaona uwezo mkubwa wa Jude Bellingham, hiyo Ballon d’or ni bora apewe Vini Jr

Sijaona uwezo mkubwa wa Jude Bellingham, hiyo Ballon d’or ni bora apewe Vini Jr

Upande wa La liga Jude amechangia pakubwa ubingwa wa Real Madrid I think mashindano ya Euro na Copa America yata amua nani mshindi kati ya Mbappe, Vinni na Jude
Mimi sio mpenzi wa haya matunzo binafsi sababu mpira ni team kubwa sana wanachangia mafanikio lakini, sababu hizi ndio tamaduni zimekuwa ngoja nitoe maoni yangu. Kuna wale wachezaji michango yao ni mikubwa sana ni kama wakati ule Messi yuko top siku akiumwa basi Barca wanapoteza ule ukali unaona pengo, Kina Ronaldo, Iniesta na wengine huko nyuma real stars. Kwa hawa waliopo wachezaji wazuri lakini bado mmoja atokeze anyoshe kidole juu ajitofautishe na wenzake nadhani bado.

Vini mechezaji mzuri sana lakini wakati yuko nje ya uwanja team ilifanya vizuri tu bila yeye. Bellingham mzuri lakini PR wa UK zinamuongezea thamani kuliko uhalisia. Mbape hakuna ubishi mzuri sana tu lakini mwaka wa saba hakuweza kuisaidia PSG ndoto yao ya CL. Mchezaji bora anatakiwa awe na uwezo wa kuibeba team kuifikisha kwenye malengo. Labda huko Euro ataamua lakini kama Euro ndio uamuzi basi sio haki maana kuna wachezaji wengi kama Vini hawako Euro. Hitimisho hakuna anastahili zawadi hii waache jimbo wazi.
 
Uwepo wa Mess na Ronaldo uliwanyima tuzo wachezaji wengi sana wa zuri mfano Zlatani ila sasa tuzo itatolewa tu sababu ni desturi ila ushindan haupo wa kutosha kwa sababu wachezaji wengi hawatofautiani san uwezo' tofauti ya Mess na Ronaldo wao walikuwa wana vitu unique. Sasa hivi tumebaki na wafungaji na wakimbiaji kusnzia Haland, Vin, Mbabe angalau Jude ana skills kidogo.
 
Kumekuwa na kelele mitandaoni kuwa Jude Bellingham anastahili kutwaa tuzo ya Ballo d’or

Msimu huu kwenye Uefa kuanzia hatua ya mtoano mpaka Madrid wanabeba taji sijaona mchango wake walau hata kuamua mechi.

Vini Jr ameshafanya hivyo mara nyingi lakini sifa zote anamwagiwa Jude.

Jude ana kipi haswa cha maana?
Euro 2014 keshokutwa tuu ...tusubiri tuone Bellingham ataifanyia nini national team...
 
Jamaa ana PR matata sana, Na nguvu ya media ya Kiengereza vikiungana tunakoma sana. Ila kiuhalisia Jamaa ni kimeo kabisa
 
Back
Top Bottom