LGE2024 Sijapenda Approach ya Lema kule Arusha

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Lema alidai CHADEMA watashiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa na kuahidi kupambana. Pamoja na sisi wanachama kudai ya kwamba CHADEMA isishiriki huo uchaguzi lakini bado Viongozi hao akiwemo Lema walikazana CHADEMA ishiriki pamoja na rafu zote zile.

Cha kushangaza Jana tarehe 27 Novemba siku ya kupiga kura, Lema anatangaza rasmi kwamba yeye Kama kiongozi amejiondoa kwenye huu uchaguzi na kwamba hatashughulika na lolote. Na sababu za kijiondoa ni kwamba rafu ni nyingi Sana mkoani Arusha. Hivi Lema alitegemea Nini kutoka kwa CCM ? Amesahau 2020 kilichofanyika?. Kwa kweli CHADEMA tunahitaji Viongozi wenye kauli moja na sio Leo unasema hivi na kesho unabadilika na kusema kingine.

Kama mnashiriki uchaguzi mshiriki mpaka mwisho na sio kujitoa dakika za mwisho au Kama hamshiriki msishiriki kabisa. Kushiriki uchaguzi Chini ya serikali dhalimu ya CCM ni kukubali rafu zote na wizi wote wa kura.

Soma pia: Arusha: Godbless Lema ameamua kususia na kujitenga kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa
 
Sometimes CHADEMA nawao hawana msimamo, wana ndimi nyingi sana kila kiongozi wao anaongea analojisikia tu.........Chama hakina command of chain
 
Kila siku nasisitiza humu kuwa Tanzania hakuna uchaguzi bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Ni matumizi mabaya ya raslimali fedha na muda kwenye upuuzi huu uitwao uchaguzi.
 
Fahamu malengo ya kiongozi kabla ya kuwa mfuasi wake. Usifuate anachosema, fuatilia anachotenda, nyendo zake. Siasa ni maslahi.
 
Huu uchaguzi ulikuwa siyo wa kushiriki kabisa

Ova
 
Kama unamuamini Lema basi una safari ndefu sana.Juzi alifika kwenye Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Arusha na kuhamasisha watu kwamba wakae mpaka kieleweke.Madai ya figisu kumbe ni kosa la Mwenyekiti na Katibu wa Wilaya wa Chadema kutoelewa kanuni.Lema alipoingia ndani na kupata maelezo ya nini cha kufanya akawaambia makamanda watawanyike wameshapata maelezo ya nini cha kufanya na ameridhika.
Ili asipoteze hadhi yake alichosema mwanzo akaongeza utoto wa kususia huku Mwenyekiti wake Freeman Mbowe akipiga kura bila bugudha.
 
Lema alidai CHADEMA watashiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa na kuahidi kupambana. Pamoja na sisi wanachama kudai ya kwamba CHADEMA isishiriki huo uchaguzi lakini bado Viongozi hao akiwemo Lema walikazana CHADEMA ishiriki pamoja na rafu zote zile.

Cha kushangaza Jana tarehe 27 Novemba siku ya kupiga kura, Lema anatangaza rasmi kwamba yeye Kama kiongozi amejiondoa kwenye huu uchaguzi na kwamba hatashughulika na lolote. Na sababu za kijiondoa ni kwamba rafu ni nyingi Sana mkoani Arusha. Hivi Lema alitegemea Nini kutoka kwa CCM ? Amesahau 2020 kilichofanyika?. Kwa kweli CHADEMA tunahitaji Viongozi wenye kauli moja na sio Leo unasema hivi na kesho unabadilika na kusema kingine.

Kama mnashiriki uchaguzi mshiriki mpaka mwisho na sio kujitoa dakika za mwisho au Kama hamshiriki msishiriki kabisa. Kushiriki uchaguzi Chini ya serikali dhalimu ya CCM ni kukubali rafu zote na wizi wote wa kura.

Soma pia: Arusha: Godbless Lema ameamua kususia na kujitenga kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa
Kiongozi haitakiwi kuzira kudai haki.
 
Back
Top Bottom