Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 20,694
- 32,527
Habari wanajf, moja kwa moja niende kwenye mada husika.
Juzi wengi tulimsikia mgombea wetu akiweka msimamo mara mbilimbili kuhusu kuendelea na kampeni siku ya leo na kwa muktadha huo alikuwa anamaanisha na ndio maana akafanya press siku hiyo.
Na kwa uhakika makamanda tulikuwa tumejiandaa kwa lolote, ikumbukwe tulishasema SASA BASI.
Mgombea wetu alieleza wazi kuwa hajapokea barua yoyote na hajasikilizwa hivyo uamuzi huo wa tume ni batili kwa kuwa barua haijamfikia kabisa.
Kitendo cha kamati kuu iliyoongozwa na mwenyekiti wetu kuja na maamuzi tofauti na aliyosema mgombea wetu ni tatizo kubwa sana.
Kwanza ni kama mmekiri kupokea barua ambayo kimsingi alivyoeleza mgombea ni kuwa haijapokelewa.
Pili, ni kama mmemuweka mgombea wetu kwenye mtego kwa kuonekana alikurupuka siku ya juzi kutoa maamuzi kabla ya kamati kuu kukaa.
Tujirekebishe au la sivyo basi mgombea wetu aambiwe asitoe msimamo kabla ya kamati kuu kuamua.
Mwenyekiti amekiri kuwa wagombea ubunge 36 wameenguliwa na wagombea udiwani 500+ wameenguliwa , ila cha kushangaza hadi leo hii chama hakijui wafanye nini ili hawa warudishwe na ni kama ndio imeshatoka hiyo