Uchaguzi 2020 Sijapenda, CHADEMA rekebisheni haraka haya makosa

Mbowe kaja na maamuzi ya hovyo sana, kwa hapa alipoifikisha chadema tunamshukuru sana ila kwa maamuzi ya hovyo km haya tutamuomba atuachie chama chetu Kwa sasa tunaitaji siasa za kihanarakati na sio siasa za kubembelezana anazoziendekeza yeye
Hizi siasa za kiharakati ndio zinawafelisha

Sio zama za harakati hizi
 
Hujui kitu kuhusu siasa wewe.
Kukusaidia tu ,Siasa ni sayansi na watu wakula kitabu kuisomea
 
Mbowe anafahamu mgombea wake ni mropokaji

Anakiri hilo
 
So lissu alivyosema hakupokea barua alikuwa hajui anachosema, kwa kuwa kamati baada ya kudigest wakakubaliana na wanayosema NEC
 
Hizi siasa za kiharakati ndio zinawafelisha

Sio zama za harakati hizi
Africa bila siasa za kiharakati huwezi kuking'oa chama tawala madarakani. Never ever
 
Juzi Lissu kasema hajapokea barua na ataendelea na kampeni leo, wengi tukafurahi na kusema mwaka huu bampa to bampa. Sasa hapa kosa langu nini?
Wewe jadili yule aliyeomba kusuguliwa achana kabisa na chama chetu.
 
So lissu alivyosema hakupokea barua alikuwa hajui anachosema, kwa kuwa kamati baada ya kudigest wakakubaliana na wanayosema NEC
Ndugu yangu kila kitu kina utaratibu. NEC ikitaka kumfikia mgombea yeyote kuna channel ya mawasiliano, lazima ipitie kwenye chama kilichomdhaminimgombea husika! Hapa nchini hakuna mgombea binafsi, kila mmoja lazima awe mwanachama wa chama cha kisiasa na adhaminiwe na chama hicho.
Lissu anaposema hajapata barua yeye in person kama mgombea Ni kweli pia. Hadanganyi. Lakini Tume inagoma, inasema huo siyo utaratibu. Tume inadai enyewe haina anwani binafsi ya Lissu ila ina anwani ya Taasisi iliyomdhamini Lissu kama mgombea wake. Ndivyo ilivyo hata kwa vyama vingine.
Kamati Kuu ya CDM haina sabahu yoyote ya ku-compromise kampeni ya Lissu Ila inaangalia mambo ktk dimensions kadhaa. Kumbuka Lissu naye ni mjumbe wa Kamati hiyo, kama sehemu ya Kamati naye karidhia. Shida iko wapi hapo?
 
Juzi Lissu kasema hajapokea barua na ataendelea na kampeni leo, wengi tukafurahi na kusema mwaka huu bampa to bampa. Sasa hapa kosa langu nini?
Unajua kusoma?
Basi soma #2 na #3; kama bado huelewi ina maana hujui kusoma na kuelewa kilichoandikwa.
 
mjomba kuwaelewesha sisi ufipa ni kazi ngumu.kwa maana ile tu sisi kujiita wanaharakat ndio bas bah shida kuanzia hapo.sisi wengine hatuelew hata tunataka nini
 
Juzi Lissu kasema hajapokea barua na ataendelea na kampeni leo, wengi tukafurahi na kusema mwaka huu bampa to bampa. Sasa hapa kosa langu nini?
Alikuwa na msimamo binafsi lkn akasema atasubiri maamuzi ya kamati kuu.Na kama ni kumwelewa ni kwamba yeye hayuko juu ya chama na pili pia kamati kuu ingeweza kukazia maamuzi ya mgombea kuwa aendelee na kampeni na hivyo kupingana na maamuzi ya NEC.Kwa muktadha huo MH.Lissu imemlazimu kuyaheshimu maamuzi ya chama.
Ndivyo ilivyo.
 
Juzi Lissu kasema hajapokea barua na ataendelea na kampeni leo, wengi tukafurahi na kusema mwaka huu bampa to bampa. Sasa hapa kosa langu nini?
Kosa lako ni kuwa unajijua ni mwezi mchanga lakini hutaki kukubaliana na hali yako. Idara ya kusikia haiko vizuri, muone daktari haraka.
 
Ulimuelewa Mbowe kweli wewe?
 
Tulia mtoa hoja, CDM inakwenda kisayansi zaidi..... !! ala kumbe na wewe ngoma ya TL ulishaaza kuikatikia mauno eee - pole..

Kwa sasa mgombea kashapangiwa majukumu mengine - stay tuned for more updates.
 
Pili, ni kama mmemuweka mgombea wetu kwenye mtego kwa kuonekana alikurupuka siku ya juzi kutoa maamuzi kabla ya kamati kuu kukaa.

Katika maelezo yake moja ya sentesi alizosema ni kwamba "...vilevile itategemea maamuzi ya cahama"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…