Simba ya sasa ni Bora, na tuseme kuwa Yanga ikajipange.
magoli kama yale ni kweli Manula anaugonjwa nayo , hata Morrison alimfunga sana Manula kwa staili ile , lakini haindoi uhalisia kuwa bado ni golikipa bora.
Mgunda amefanya a major reform ya Klabu yetu pendwa na kurudisha tumaini ambalo liliondolewa na makocha wakigeni wasioelewa Chemistry ya soka letu.
Chance ya Juma kushinda hii game ilikuwa ni zaidi ya 60%, changamoto ya Dabi inaenda na presha hivyo utulivu unakuwa hafifu, Hongereni simba kwa soka bora , sio lazima kila mechi ushinde, kupiga kandanda ya kujiamini inatia moyo.
Ninaamini Mgunda anacheza NUSU FAINALI , CAF ,Mark my words .
Katika kufanya MOTISHA ya makocha wa kizawa,SSC waache MBAMBAMBAMBA na wamtangaze Juma kama Head Coach haraka sana.
Mshahara wa Head Coach SSC si chini ya Mil 25 pamoja na benefits zote as Head Coach ikiwa ni pamoja na kumpatia makazi tena MASAKI au Osterbay na usafiri binafsi kama jinsi ambavyo makocha wa kigeni hupewa hizo care.
Hii pia itatengeneza career path nzuri na motisha kwa makocha wengine wa ndani.
SSC na Yanga, kabla hamjaanza kuhangaika na makocha wa nje angalieni kwanza ndani , achaneni na mambo ya uzoefu, toeni uzoefu kwa kuwajenga makocha wa ndani ambao kwa asilimia kubwa watakuwa na uelewa mkubwa wa soka la Africa Na kujua hitaji la mashabiki.
Yanga hii game ilikuwa tuwapige nyingi , ni presha tu ya Dabi, but hii game leo ilikuwa tuwapige hata tatu.
Mjipime upya, maana kunauwezekano mkubwa hata makundi ya shirikisho msicheze, siamini na sitokuja kuamini kama mtaweza kuwatoa Africa Club. Maana ile timu inapambana na timu kama Widady na Raja.
Huyu Nabi sasa anaenda kuwa tested kwa mara ya pili, na safari yake ya makundi itaishia tunisia, ndio mtajua kuwa kumbe shirikisho sio ya maloser, na kuna haja ya kupromote talents za ndani.
Na nyie makocha wa ndani anzeni kujiamini na kujiongeza kielimu.