Sijasafiri Nje ya Nchi kwa muda sasa, naombeni Utaratibu wa kupata Pasi Mpya ya Kielektroniki Nisafiri

Sijasafiri Nje ya Nchi kwa muda sasa, naombeni Utaratibu wa kupata Pasi Mpya ya Kielektroniki Nisafiri

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Na je, ukiwa bado unayo ile Pasi ya zamani ukienda kuhitaji hii mpya ya Kielektroniki mchakato ni mkubwa au details zilizoko katika Pasi ya zamani ndiyo hizo hizo zitatumika kwa hii ya Kielektroniki na kuipata Kiuharaka?

Na je, muda wa kupata Pasi Mpya ya Kielektroniki ni upi? Je, huko kwa Wahusika hakuna Utoaji wa lazima wa Asante ya Kiulaghai / Rushwa?
 
Si useme tu hujawahi kuvuka boda!
Unazunguuukaaa!!!!
Niko serious acha Utani basi sijasafiri nje ya Tanzania tokea November 2001 ila nina Pasi ile ya zamani bado sijaibadilisha Ili niipate hii mpya ya Kielektroniki na ndiyo maana nawaombeni Muongozo kwani nahisi kuna Safari inakuja mwishoni mwa mwaka huu wa 2022 au mapema mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2023.
 
Unapply kupitia website kama mpya kwenye sababu za uhitaji utaandika unahitaji passport za kielectroniki kisha lipia kwa control no fee ya awali, utadownload, print na kucertify - kuna eneo la mwanasheria kucertify.

Kisha nenda ofisi za Immigration na certified copy na original documents zote usisahau vyeti vya shule au kazi na supporting documents nyenginezo.

Utahojiwa na ukipita watatoa control no. Utalipa final amount iliobaki pale pale na kupigwa picha.

Passport ya zamani utaipeleka wataitoboa toboa code zake ili isisomeke na kukurudishia.

Baada ya wiki moja passport itakuwa tayari. HAKUNA HAJA YA RUSHWA YEYOTE

Gharama zote kwa ujumla ukiondoa mwanasheria ni 150,000/= Hakuna longo longo zozote
 
Unapply kupitia website kama mpya kwenye sababu za uhitaji utaandika unahitaji passport za kielectroniki kisha lipia kwa control no fee ya awali, utadownload, print na kucertify - kuna eneo la mwanasheria kucertify.

Kisha nenda ofisi za Immigration

Upload document zote na nenda na certified copy
Asante sana Mkuu kwa Muongozo huu.
 
Swali liloulizwa ni kwamba kwanini ,ukiwa na pasi ya zamani isiwe ni rahisi kupata mpya ikiwa vielelezo ni vilevila tu na hii inatoa mwanya wa rushwa? Sio kwamba GENTAMYCIME swali lake ni hilo alilouliza ila anataka kujua akili zenu zikoje
Siitwi huyo Tapeli na aliyeiiga ID yangu Ili asafirie nyota yangu Kali yenye Mvuto wa Kipekee aitwae GENTAMYCIME bali Mimi naitwa GENTAMYCINE sawa?

Nipo hapa JamiiForums tokea mwaka 2013 na huyu ( huyo ) Pimbi Kaibuka Juzi tu hapa na mwaka huu 2022.
 
Ngoja nikujibu swali lako, ni kwamba hii yote inatokana na uongozi mzima toka ngazi ya juu hadi uhamiaji wenyewe kila mmoja yupo hapo kwa tumbo lake ila sio kwa ajili ya taifa hili na watu wake, leo hii ukiwa na shida ya pasi mpya na hata kama baadhi ya document huna bado utaipata pasi hiyo ukiwa na hela.

Niliwahi kujipendekeza mahali nilipoona kuna hali sio njema kwenye mipaka ya nchi yetu ikiwa watu unawajua kabisaa hawa sio watz na bado walipata nida na wengi wao wana pasi, siku hiyo ndio nilijua kuwa Tanzania hii uzalendo kafanyie kwenu ila sio katika kulifia taifa letu
 
Siitwi huyo Tapeli na aliyeiiga ID yangu Ili asafirie nyota yangu Kali yenye Mvuto wa Kipekee aitwae GENTAMYCIME bali Mimi naitwa GENTAMYCINE sawa?

Nipo hapa JamiiForums tokea mwaka 2013 na huyu ( huyo ) Pimbi Kaibuka Juzi tu hapa na mwaka huu 2022.
Nisamehe mkuu sikuangalia vizuri kumbe huyu anatumia jina la kufanana na mtu mwenye akili zake timamu
 
Unapply kupitia website kama mpya kwenye sababu za uhitaji utaandika unahitaji passport za kielectroniki kisha lipia kwa control no fee ya awali, utadownload, print na kucertify - kuna eneo la mwanasheria kucertify...
Mkuu umeitendea haki ID yako, Big up.
 
Unapply kupitia website kama mpya kwenye sababu za uhitaji utaandika unahitaji passport za kielectroniki kisha lipia kwa control no fee ya awali, utadownload, print na kucertify - kuna eneo la mwanasheria kucertify...
Kuna mtu alipitia hatua zote hapa na bado mpaka leo ni kisanga, mpaka nilipomtafuta mwenye kibubu chetu ndio ikawa afadhali
 
Swali liloulizwa ni kwamba kwanini ,ukiwa na pasi ya zamani isiwe ni rahisi kupata mpya ikiwa vielelezo ni vilevile tu na hii inatoa mwanya wa rushwa? Sio kwamba GENTAMYCIME swali lake ni hilo alilouliza ila anataka kujua akili zenu zikoje
Hata Mimi kutokana na kujua kuwa GENTAMYCINE ni mtu "well informed" sikutarajia aulize hili swali. Nikadhani Moja Kwa Moja ni GENTAMYCIME ndo anauliza.

Back
Top Bottom