Habari zenu MMU?
Natumaini mko poa kabisa na afya njema. Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Mimi ni kijana wa kitazania ambae nina umri wa miaka 24. Yaani toka nizaliwe sijawahi kufanya mapenzi na mwanamke yoyote hapa duniani, mimi nimwanaume niliekamilika kwa 99%.
Mashine yangu ipo imara sana ila nimekuwa mpweke sana hususani kwenye mambo ya mapenzi, kusema ukweli mapenzi niliyaweka pembeni nikaconcentrate kwenye masomo na mazoezi zaidi, sikuweza kuwatongoza kabisa wanawake japokuwa nilikuwa na hisia kama mwanaume.
Nilijipangia kuwa nitafanya mapenzi nikiwa kwenye ndoa hapo ndio nitasema nimeushinda mtihan, jaman kukaa bila kufanya mapenzi ni mtihan mgumu sana unaelekea kunishida, tangu nije Dar nimetokea kuwa na urafiki wa karibu sana na msichana wa chuo, huyu msichana nimetokea kumpenda sana, tatizo ananichukulia kama rafiki akija dukani napagawa yaani jinsi alivyoumbika mithili ya malaika, kumwambia naweza tatizo nahofia kukataliwa then iwe aibu akija dukani.
Naomba mawazo yenu ya hekima.