Sijawahi kuisahau hii siku

Sijawahi kuisahau hii siku

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Nikiwa primary nlikuwa mtoro saana na mtukutu

Kuna siku nilitoroka shule na "masela" wangu mida ya kama saa5 tukaenda kuiba miwa kwenye shamba la mzee mmoja hivi lipo karibu na shule.

Sasa basi, tukazama shambani tukaingia ndanindani kusaka miwa mikubwa [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Tulikuwa kama wa3 ilikuwa kipindi cha joto so tunavuja jasho hatari.

Kumbe kwenye ile miwa kwa juu kuna UPUPU wa matunda kama maharage[emoji28][emoji28][emoji28]. Hapo hatuna panga so unauvuta muwa hadi ukatike.

Balaa lilianzia hapo ule upupu ukawaga VUMBI lake ukichanganya na jasho sasa [emoji21][emoji21][emoji21] aisee tuliwasha tukaanza kulia kwa sauti na miwa hatujaiacha [emoji28][emoji28][emoji28][emoji38].

Kwenye shamba kulikuwa na mfereji wa maji tukazama kuoga ila wapi ni mwendo wa kuwashwa ike mbaya hadi tukavimba.

Tukasema kuingia porini na miwa yetu tukakaa kivulini, baada ya.muda muwasho ukaisha tulianza kuchekana kwa sauti balaa huku tunakula.miwa yetu ya wizi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Upupu wenyewe unafanana na huu hapa chini.

Una kisa cha kutusimulia?

Tiririka hapa
FB_IMG_1626986780488.jpg
 
Haki tulikua tunang'oa miwa halafu maganda tunatoa na meno hamna kisu wala nini [emoji2][emoji2], hatujahamia kwa vibungo na ndizi pori/furu na mazagazaga ya porini lakini ukitukuta Four point by Sheraton unaweza dhani tumezaliwa Uingereza
 
Weka mbali na watoto.
Kuna ndugu yangu aliniona nina mavuzi akatamani naye ayapate nikamwambia weka upupu yataota muda si mwingi. Akaweka.
Aliteseka sana ila hakulia maana nilimwambia ukilia tu dawa itagoma
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] we jamaa chizi sana
 
Haki tulikua tunang'oa miwa halafu maganda tunatoa na meno hamna kisu wala nini [emoji2][emoji2], hatujahamia kwa vibungo na ndizi pori/furu na mazagazaga ya porini ..
lakini ukitukuta Four point by Sheraton unaweza dhani tumezaliwa Uingereza
Miwa ya karibu na shule ilipata tabu sana.

Kisu kitoke wapi shuleni
 
Back
Top Bottom