Sijawahi kuona brick-and-mortar store yoyote hapa Dar, lakini watu wana Gucci

Sijawahi kuona brick-and-mortar store yoyote hapa Dar, lakini watu wana Gucci

Nimeona michango mingi ikisema GSM mall ndo mahala sahihi,ambapo mtu anaeza pata original luxury brand clothes..Naomba mwenye clarification kama ni kweli?
 
Mkuu Nyani Ngabu maisha ya nchi zetu hizi ni tofauti sana na ya kule duniani! Kwetu huku kuna tabaka la watu wachache sana (wenzetu walioenda shule, wale wasanii na wanaoigiza wasanii) wenye kuvaa wakijua hizo brand za mavazi. Sisi wengine hatujui hizo brand, ndiyo maana hata wauzaji unakuta wamechanganya na kuzimwaga chini hizo brand na nguo 'zisizo na brand'. Unaokota kulingana na rangi ilivyokuvutia na vile inavyokaa mwilini. Hata muuzaji hakwambii "ukiokota GUCCI ni bei ya juu"! Haya ndiyo maisha ya sisi unaotusema tunakaa hata njia hakuna. Ni vendors wachache sana wanaojipigia hela kwa kutumia hizi brand (wanajipigia kwa ninyi mnaojua na kuzifuata). Kwetu sisi (ambao ndiyo waTZ wengi) wala hatujui na hatuvai kwa brand.
Vitu vinavyoonekana vidogo hivi ndivyo ambavyo serikali makini huvitumia katika kufanya "market intervention". Government intervention kwenye hili itaishia kupunguza tu "supply" na waathirika wakubwa tutakuwa wengi wetu sisi tunaojikuta tumevaa GUCCI by default (kwa kuwa tuliokota chini nguo yenye rangi inayovutia ama iliyokaa vizuri mwilini tulipoijaribu).
 
😀😀😀😀😀

Halafu wengine wala hata hawajui kuwa ni feki!

Ni bora hata ukiwa unajua kuwa ni feki na unaamua tu kununua na kuvaa huku ukijua ni feki.

Wale wanaonunua na kuvaa huku hawajui kuwa ni feki [wakidhani kuwa ni genuine] ndo wanatia huruma maana ni wajinga halafu hata hawajui kuwa ni wajinga!
Ukishaenda kariakoo manake unaenda kununua kitu ya mchina.ukitaka ufurahi iweke kwa maji ufue,anika ikikauka utapata kitu nyingine kabisa.mchina si mtu mzuri.
 
Back
Top Bottom