Sijivunii wazazi wangu

Sijivunii wazazi wangu

Najivunia wazazi wangu, namshukuru Mungu kwa kunipa wazazi hao. Kama nilivyo na mapungufu mimi, na wao wana ya kwao, naheshimu maamuzi yao na jitihada zao, na kamwe siwezi kukosoa matakwa yao na mnana yao waliyonilea.

Asante Mungu kwa zawadi ya wazazi. Kwani wapo ambao walizaliwa hawakupata kuwaona wazazi wao kwa sababu moja au nyingine, walitamani ata kuwa na mtu wa kumiita baba au mama na hawakupata. Eeh Mwenye enzi Mungu uwape uzee usio na maradhi, na uwafanyie wepesi katika mwisho waa na mwisho uwape mwisho mwema. Amina.
Sawa, ubarikiwe
 
Kifupi ni kwamba fanya kulingana na moyo wako usiforce ikiwa moyo hautaki..
Pia kama waliishi maisha yao kwa anasa na kutojipanga usikubali kubeba mzigo huo..
Ogopa mtu anajekufanya ujione na hatia kila wakati huo ni ubinafsi..
Usikope hela kusaidia mtu never never
 
thank you for the advice man
 
Hivi ni wote mna wazazi kama wangu?, au mliwahi kuwa na wazazi kama wangu?, Najua ambao hamuelewi nini nazungumzia hapa haiwezi kuwaingia akilini au pia mnaweza kuhisi labda sina akili timamu na wale ambao kwa bahati mbaya mlishapoteza wazazi wenu basi pia hii tungo haitowaingia akilini, ila aina ya maisha ninayoyaishi ndo yanafanya niandike tungo hii ngumu ambayo si rahisi kuisikia kwa watu.

Sorry kwa kusahau kuwasalimu, ila kwa leo nipo na bad mood naji-feel tu kutema hii sumu ili isiniue maana hii kitu inaniuma sana wakuu, Imagine unakuwa na wazazi ambao hawajawahi kukupa direction ya maisha, Connections, Hawajaaliwa kumiliki kiwanja au hata nyumba useme utarithi, Haya basi wangekupambania usome uwatoe kwenye hiyo hali. wapi, Haya basi hata shughuli ya kufanya basi iwe imetokana na connection zao. wapi, Haya basi hata ushauri nini cha kufanya au pita njia hii. wapi, Kiufupi baada ya kumaliza Kidato cha nne nikaja Dar habari ya wao na mimi iliishia palepale.... I'm sure hata matokeo yangu hawayajui, ila wao wanajua mimi nimefeli. Mimi kuamua kuwaacha nisiwasumbue masuala ya kunisomesha kwa kuwa niliona hali ya nyumbani sio basi wao akili zao zimesave kwamba nilifeli ila sivyo. Okay, tuseme ni ukweli nimefeli hebu niambie je, mwanao ikitokea ameshindwa kuendelea na masomo basi unamtelekeza akajuane na maisha yeye mwenyewe?

Dah! Asee inaniuma kinoma ni Dsm mwaka wa nne sasa, Mzee yupo Arusha mama yupo Iringa (Wao waliachana punde tu baada ya mimi kuzaliwa) Mimi ni mtoto wa pekee kwa baba ila mama tayari ana watoto wengine wawili huko alipo.... Simu zao zikiita kwangu basi najua ni vizinga tu, Baba aliwahi kuanzisha mradi wake huko Moshi akanishawishi nimtumie kahela fulani tuwekeze tufanye jambo litatulipa nikafanya ikaja ikalaga kwangu nikasemehe kwa kuwa ni mzazi, Baba yangu anaishi kwa wazazi wake yaani kwa bibi yangu mimi., Mama yangu anaishi Iringa amepangisha na hata baba wa watoto wawili aliokuwa nao pia walishaachana (sahivi ni single mother)

Dah wakuu kuna vitu navificha hapa sitaki visema kutoka kwa huyu baba yangu na mama yangu kuna maneno waliwahi kunitamkia kwa nyakati tofauti tofauti maana nilishajuza kwamba hawaishi pamoja, ila acha niseme tu, kwa sasa wao wanajua mimi napiga harakati zangu za hapa na pale kwahiyo kuna wakati nawakumbuka japo 10k kila mmoja, Sasa ikitokea labda imepita muda mrefu sijafanya hivyo kila mmoja wao huisi kwamba nampendelea mwingine na pengine labda ndo inapelekea nisitume hela kwa muda mrefu. Jambo hili huleta mgogoro wa vinyongo baina yangu mimi na mzazi atakaehisi hivyo, Ni wote tu sometimes ni mama sometimes baba me, hupambana kuwaelewesha kwamba sivyo wanavyofikiriana hadi huchoka.... Kuna siku mzee aligomba hadi akanikatia simu nikakopa 12k nikamtumie eti akapiga simu muda huohuo huku anacheka "Mwanangu wewe ndo umetumia hii asante sana" nikamjibi ndiyo kwa hasira nikamkatia simu.

Wote tunaamini wazazi wetu ndo wanatupenda kwa dhati ila mimi kwangu ni tofauti kwani nilishajithibitishia kabisa kwamba wazazi wangu wapo after money, hata simu zao zikiita muda huu najua tayari hapa napigwa kizinga.

Baba alishawahigi kunitamkia maneno haya "Mimi nahesabu sina mtoto bana, Mtu hata hunisaidii chochote hapo nikikuambia nitumie kalaki kamoja utasema huna, kwenda kule me sio baba yako" hiyo ilikuwa kwenye simu and i was in hard situation for sure imagine pa kulala penyewe palikuwa kwa mshikaji kanisitiri, ila baadae tulikuja tukamalizana mshua kiume tukaendelea kuishi kinafki. Mama nae aliwahi kuniambia maneno haya "Yaani mi nahesabugi nina watoto wawili tu, We mtoto gani unamsahau mama yako kiasi hiki? Yaani hujawahi hata kunitumia zaidi ya 30,000 acha nimuombee huyu mwanangu wa pili ndo naona atakuja kunitoa kwenye umasikini...." Huyu mtoto wa pili sahivi yupo form 5 na anasomeshwa na mashangazi zake wao upande wa ndugu zake wapo vizuri kiuchumi kiasi chake so, mama yupo proud na huyu wa pili.... Me hiyo kitu though inaniuma mimi kama first born ila me humuachia Mungu wangu kwani ndiye alieruhusu niishi haya maisha.

Kiufupi me najionaga kama nina laana hivi, Imagine unazaliwa nje ya ndoa alafu bado wazazi wanaachane tena punde tu after umezaliwa😁😁😁, Acha nicheke tu maana muonekano wangu jamani ndo unafanya nione kabisa kwamba familia yetu ni kama kuna mahali ilichezewa, Me muonekano wangu ni ambao unaonesha kabisa kwamba imetokea bahati mbaya tu me kuzaliwa kwenye aina hii ya familia, Me najipenda sana watu hudhani me ni mtoto wa geti kali, Huishia kuitwa majina kama Bishoo,Sharo, Wa kishua ila me hubaki tu kushangazwa na hayo majina laiti wangejua.

Anyways ambao wangependa kujua naishije hapa Dar ni kwamba naishi ki-mission zaidi, Me ni kijana ambae napenda uhakika sana sinywi pombe,sivuti bangi, sina hobby na ladies, Me ni mtu ambae kiufupi sina mambo mengi, Me ni kijana ambae Mungu angenijaalia wazazi ambao wanaelewa wajibu wao ningekuwa mbali mno, Fikiria nimelelewa na baba pekee... though alikuwa careless ila hadi namaliza 4m4 sijawahi kuingia kwenye mtindo mbovu wa maisha, Me nimekuja Dar mbali na wazazi sina hili wala lile and they didn't even care of me na still nimeweza kujitegemea, Hadi kuna wakati najiuliza usikute hii kitu ndo imefanya wakaona huyu kashajiweza tuachane nae. Maana me nikiwa 17 tuu washaanza kunipiga vizinga na nikaonesha kuvimudu japo kibishi.

Simu zao za kinafki husema kwamba "Mwanangu lini uje kunisalimia, miaka mingi hujaonana na na baba/mama yako hivi unajua najisikiaje huku nilipo fanya uje bana" hapo ni baada ya 10k kuingia kwenye cm ya mmoja wapo... Kimoyomoyo mimi hujosemea kwamba "Kama sio ninyi maisha yangu yasingekuwa ya taabu hivi, Acheni niwatumie kidogo changu hiki ili mjihisi nanyi mna mtoto" Ila kiukweli sijivunii wazazi wangu, Sasa jamani hata useme ukasalimie unaenda kulala wapi Baba hana nyumba yupo kwa bibi imagine kweli tuende wote tukarundikane kwa bibi mjukuu na baba yake kweli? au haya kwa mama, Kapanga room mbili mimi na midevu yangu nikaingie nikae kwenye bedroom ya mama sure?

Eeh Mungu wangu nisamehe kama nakosea ila acha niyatoe tu maana sina wa kunisikiliza nitakufa kwa maumivu haya niliyonayo, Sometimes inafikia nakufuru kuona ni bora mtu uwe hauna wazazi kuliko kuwa nao ambao wanachangia kukurudisha nyuma na kukuvunja moyo, Wazazi waliotangulia wenye ramani ila hawakuoneshi njia.

Mtu mnajua mmeshindwa kumhakikishia mwanenu maisha bora haya basi kaonesha anaweza kupambana basi muacheni still bado mnataka kumpa majukumu ya kuwazingatia ninyi sure?
HESHIMU Baba na mama yako (waliokuzaa) upate kuishi miaka mingi na heri duniani! Mapungufu yao hayabadili ukweli kuwa walikuzaa, bila wao kukutana usingetype huu UPUMBAVU hapa!
 
Nikikuta simba anataka kumla baba angu nitamsaidia simba amle Vizuri. Basi tu siwezi kumbadirisha!
people think it's easy mtu kumlaumu mzazi, watu tunawapenda sana wazazi wetu ila wanachotufanyia hadi kuna wakati mtu unafika unawaza au hawa sio wazazi wangu? waliozaliwa wakabahatika kupata wazazi wanaojielewa vizuri hawawezi kuelewa nini nasema.
 
Wazazi wachache sana wanajielewa
Wengi wanazaa tu ili kuonekana wana watoto lakin kuhudumia watoto hakuna wanaacha watoto wajitegemee umri mdogo na Ndio maana watoto wengi wa kike wanadanga sana kwasababu ya umaskin kwao
Ingekuwa wazazi wanazaa kwa mpango na kutunza watoto wao vizuri mabinti wengi wasingehangaika
Kuna wale wazazi wanazaa kila mtoto baba yake familia inakuwa na mgawanyiko mkubwa
 
HESHIMU Baba na mama yako (waliokuzaa) upate kuishi miaka mingi na heri duniani! Mapungufu yao hayabadili ukweli kuwa walikuzaa, bila wao kukutana usingetype huu UPUMBAVU hapa!
Mkuu wapi nimesema siwaheshimu? kutokujivunia na kutokuheshimu ni vitu sawa? Acheni kufikiri watu hawajitambui bhna ndo maana mwanzo nikasema huu uzi ni mgumu maana sio rahisi kukuta mtu akiandika kulaumu wazazi wake maana wengi tunaamini wazazi wetu wana upendo kwetu kuliko kiumbe yeyote
 
Another idiot
Jitafakari mkuu sometimes usipoelewa mambo kiundani unaweza ukawa wewe ndo idiot kabla ya ku-comment mfikirie alieandika ni kitu gani kapitia hadi akaandika, na usingalie wewe unachopitia
 
Wazazi wachache sana wanajielewa
Wengi wanazaa tu ili kuonekana wana watoto lakin kuhudumia watoto hakuna wanaacha watoto wajitegemee umri mdogo na Ndio maana watoto wengi wa kike wanadanga sana kwasababu ya umaskin kwao
Ingekuwa wazazi wanazaa kwa mpango na kutunza watoto wao vizuri mabinti wengi wasingehangaika
Kuna wale wazazi wanazaa kila mtoto baba yake familia inakuwa na mgawanyiko mkubwa
Imagine, Hapa mimi nawawaza future yao kuliko hata future yangu.... wanapoelekea ni uzee then they don't even own a house hata kama ni ya msonge ila ningejua kwamba nitawazingatia kula hadi Mungu abariki kama ningeweza kuwajengea lakini wapi, ni kwamba mimi ndo nakuja kuangukiwa na majukumu yote hayo ...na ukiwatazama hata haya ninayoyawaza hayapo akili mwao
 
Kama ni backgrounds, wapo watoto walio fiwa na wazazi wakingali wadogo.

Wapo watoto walio zaliwa na kisha wakauzwa utumwani.

Wapo watoto walio zaliwa na kisha wakateswa.

Nakadhalika nakadhalika.... Haya yote unayo yaandika ninahakina ni sababu ya hasira tu kijana.

Mimi nafikiri haya umeyaandika ili upate kuuponya moyo na kupunguza maumivu.
Umeongea point sana hapa maana kuna mtoto wa ndugu yangu alizaliwa alipofikisha miezi mitatu baba yake akafariki kwa malaria hivyo hamjui baba tunamuonesha picha tu na anaishi mpka sasa na yuko form two
 
jitafakari mkuu sometimes usipoelewa mambo kiundani unaweza ukawa wewe ndo idiot kabla ya ku-comment mfikirie alieandika ni kitu gani kapitia hadi akaandika, na usingalie wewe unachopitia
Haijalishi umepitia nini Baba yako alitoa mbegu Mama yako akatoa yai ukazaliwa. Bila wao usingekuwepo unapata wapi nguvu za kusema "nikimkuta simba anamburuza baba nitamsaidia "? Narudia tena kwa kiswahili huu ni UJINGA
 
kuzaliwa unataka wewe mkuu?
 
mkuu wapi nimesema siwaheshimu? kutokujivunia na kutokuheshimu ni vitu sawa? Acheni kufikiri watu hawajitambui bhna ndo maana mwanzo nikasema huu uzi ni mgumu maana sio rahisi kukuta mtu akiandika kulaumu wazazi wake maana wengi tunaamini wazazi wetu wana upendo kwetu kuliko kiumbe yeyote
Kama mama yako hakupendi Nani alikunyonyesha ukiwa mdogo? IDIOT
 
Hivi ni wote mna wazazi kama wangu?, au mliwahi kuwa na wazazi kama wangu?, Najua ambao hamuelewi nini nazungumzia hapa haiwezi kuwaingia akilini au pia mnaweza kuhisi labda sina akili timamu na wale ambao kwa bahati mbaya mlishapoteza wazazi wenu basi pia hii tungo haitowaingia akilini, ila aina ya maisha ninayoyaishi ndo yanafanya niandike tungo hii ngumu ambayo si rahisi kuisikia kwa watu.

Sorry kwa kusahau kuwasalimu, ila kwa leo nipo na bad mood naji-feel tu kutema hii sumu ili isiniue maana hii kitu inaniuma sana wakuu, Imagine unakuwa na wazazi ambao hawajawahi kukupa direction ya maisha, Connections, Hawajaaliwa kumiliki kiwanja au hata nyumba useme utarithi, Haya basi wangekupambania usome uwatoe kwenye hiyo hali. wapi, Haya basi hata shughuli ya kufanya basi iwe imetokana na connection zao. wapi, Haya basi hata ushauri nini cha kufanya au pita njia hii. wapi, Kiufupi baada ya kumaliza Kidato cha nne nikaja Dar habari ya wao na mimi iliishia palepale.... I'm sure hata matokeo yangu hawayajui, ila wao wanajua mimi nimefeli. Mimi kuamua kuwaacha nisiwasumbue masuala ya kunisomesha kwa kuwa niliona hali ya nyumbani sio basi wao akili zao zimesave kwamba nilifeli ila sivyo. Okay, tuseme ni ukweli nimefeli hebu niambie je, mwanao ikitokea ameshindwa kuendelea na masomo basi unamtelekeza akajuane na maisha yeye mwenyewe?

Dah! Asee inaniuma kinoma ni Dsm mwaka wa nne sasa, Mzee yupo Arusha mama yupo Iringa (Wao waliachana punde tu baada ya mimi kuzaliwa) Mimi ni mtoto wa pekee kwa baba ila mama tayari ana watoto wengine wawili huko alipo.... Simu zao zikiita kwangu basi najua ni vizinga tu, Baba aliwahi kuanzisha mradi wake huko Moshi akanishawishi nimtumie kahela fulani tuwekeze tufanye jambo litatulipa nikafanya ikaja ikalaga kwangu nikasemehe kwa kuwa ni mzazi, Baba yangu anaishi kwa wazazi wake yaani kwa bibi yangu mimi., Mama yangu anaishi Iringa amepangisha na hata baba wa watoto wawili aliokuwa nao pia walishaachana (sahivi ni single mother)

Dah wakuu kuna vitu navificha hapa sitaki visema kutoka kwa huyu baba yangu na mama yangu kuna maneno waliwahi kunitamkia kwa nyakati tofauti tofauti maana nilishajuza kwamba hawaishi pamoja, ila acha niseme tu, kwa sasa wao wanajua mimi napiga harakati zangu za hapa na pale kwahiyo kuna wakati nawakumbuka japo 10k kila mmoja, Sasa ikitokea labda imepita muda mrefu sijafanya hivyo kila mmoja wao huisi kwamba nampendelea mwingine na pengine labda ndo inapelekea nisitume hela kwa muda mrefu. Jambo hili huleta mgogoro wa vinyongo baina yangu mimi na mzazi atakaehisi hivyo, Ni wote tu sometimes ni mama sometimes baba me, hupambana kuwaelewesha kwamba sivyo wanavyofikiriana hadi huchoka.... Kuna siku mzee aligomba hadi akanikatia simu nikakopa 12k nikamtumie eti akapiga simu muda huohuo huku anacheka "Mwanangu wewe ndo umetumia hii asante sana" nikamjibi ndiyo kwa hasira nikamkatia simu.

Wote tunaamini wazazi wetu ndo wanatupenda kwa dhati ila mimi kwangu ni tofauti kwani nilishajithibitishia kabisa kwamba wazazi wangu wapo after money, hata simu zao zikiita muda huu najua tayari hapa napigwa kizinga.

Baba alishawahigi kunitamkia maneno haya "Mimi nahesabu sina mtoto bana, Mtu hata hunisaidii chochote hapo nikikuambia nitumie kalaki kamoja utasema huna, kwenda kule me sio baba yako" hiyo ilikuwa kwenye simu and i was in hard situation for sure imagine pa kulala penyewe palikuwa kwa mshikaji kanisitiri, ila baadae tulikuja tukamalizana mshua kiume tukaendelea kuishi kinafki. Mama nae aliwahi kuniambia maneno haya "Yaani mi nahesabugi nina watoto wawili tu, We mtoto gani unamsahau mama yako kiasi hiki? Yaani hujawahi hata kunitumia zaidi ya 30,000 acha nimuombee huyu mwanangu wa pili ndo naona atakuja kunitoa kwenye umasikini...." Huyu mtoto wa pili sahivi yupo form 5 na anasomeshwa na mashangazi zake wao upande wa ndugu zake wapo vizuri kiuchumi kiasi chake so, mama yupo proud na huyu wa pili.... Me hiyo kitu though inaniuma mimi kama first born ila me humuachia Mungu wangu kwani ndiye alieruhusu niishi haya maisha.

Kiufupi me najionaga kama nina laana hivi, Imagine unazaliwa nje ya ndoa alafu bado wazazi wanaachane tena punde tu after umezaliwa😁😁😁, Acha nicheke tu maana muonekano wangu jamani ndo unafanya nione kabisa kwamba familia yetu ni kama kuna mahali ilichezewa, Me muonekano wangu ni ambao unaonesha kabisa kwamba imetokea bahati mbaya tu me kuzaliwa kwenye aina hii ya familia, Me najipenda sana watu hudhani me ni mtoto wa geti kali, Huishia kuitwa majina kama Bishoo,Sharo, Wa kishua ila me hubaki tu kushangazwa na hayo majina laiti wangejua.

Anyways ambao wangependa kujua naishije hapa Dar ni kwamba naishi ki-mission zaidi, Me ni kijana ambae napenda uhakika sana sinywi pombe,sivuti bangi, sina hobby na ladies, Me ni mtu ambae kiufupi sina mambo mengi, Me ni kijana ambae Mungu angenijaalia wazazi ambao wanaelewa wajibu wao ningekuwa mbali mno, Fikiria nimelelewa na baba pekee... though alikuwa careless ila hadi namaliza 4m4 sijawahi kuingia kwenye mtindo mbovu wa maisha, Me nimekuja Dar mbali na wazazi sina hili wala lile and they didn't even care of me na still nimeweza kujitegemea, Hadi kuna wakati najiuliza usikute hii kitu ndo imefanya wakaona huyu kashajiweza tuachane nae. Maana me nikiwa 17 tuu washaanza kunipiga vizinga na nikaonesha kuvimudu japo kibishi.

Simu zao za kinafki husema kwamba "Mwanangu lini uje kunisalimia, miaka mingi hujaonana na na baba/mama yako hivi unajua najisikiaje huku nilipo fanya uje bana" hapo ni baada ya 10k kuingia kwenye cm ya mmoja wapo... Kimoyomoyo mimi hujosemea kwamba "Kama sio ninyi maisha yangu yasingekuwa ya taabu hivi, Acheni niwatumie kidogo changu hiki ili mjihisi nanyi mna mtoto" Ila kiukweli sijivunii wazazi wangu, Sasa jamani hata useme ukasalimie unaenda kulala wapi Baba hana nyumba yupo kwa bibi imagine kweli tuende wote tukarundikane kwa bibi mjukuu na baba yake kweli? au haya kwa mama, Kapanga room mbili mimi na midevu yangu nikaingie nikae kwenye bedroom ya mama sure?

Eeh Mungu wangu nisamehe kama nakosea ila acha niyatoe tu maana sina wa kunisikiliza nitakufa kwa maumivu haya niliyonayo, Sometimes inafikia nakufuru kuona ni bora mtu uwe hauna wazazi kuliko kuwa nao ambao wanachangia kukurudisha nyuma na kukuvunja moyo, Wazazi waliotangulia wenye ramani ila hawakuoneshi njia.

Mtu mnajua mmeshindwa kumhakikishia mwanenu maisha bora haya basi kaonesha anaweza kupambana basi muacheni still bado mnataka kumpa majukumu ya kuwazingatia ninyi sure?
Pole kaka na muungwana hubeba mapungufu ya wengine na wazazi ni wazazi hakuna fotokopi!!!!Wapende tu na ujivunie
 
Naam kuna wakati wazazi wanazingua sana, ila hupaswi kuwa na kinyongo kwa mzazi wako kamwe. We samehe kisha sahau kama kuna jambo limetokea, tumia akili kuepuka matatizo yanayo kukabili, kamwe usitumie mihemko.

Epuka kuingilia ugomvi wa wazazi wako, wazazi ni wakuwapenda sana ata kama hawaja tenda wema kwako. Wapende, waheshimu na wajali wazazi wako kadri uwezavyo.
 
Kuna unafiki wa watu wengi hapa Afrika kujifanya wana busara sana za kusema mzazi hakosei. Hakuna mtu alitumiwa barua na mtoto wake ili amzae. Unapompata mtoto ni wajibu wako kumlea hadi atakapojitegemea. Sasa kumleta kiumbe duniani na kumwacha ateseke si ni ushenzi uliopitiliza? Wengi wetu ni tumeamua tu kupotezea ila wazazi wengi hawataki kujua kijana anaishije baada ya kuondoka nyumbani wao ni mizinga ya kila mara. Halafu kitu kidogo tu hukimbilia kulaani mtoto. Watu tunawapenda wazazi ila wazazi nao wanatumia madaraka yao vibaya. Yaani kuna saa hadi unaogopa kupiga simu ya kusalimia kwa kuogopa kizinga. Nashauri wazazi vijana na wanaotarajia kuwa wazazi tupambane sana dhidi ya umaskini na tubebe majukumu yote hadi mtoto atakapoweza kujietegemea. Usimzae mtoto ukitegemea atakuja kuwa kitegauchumi chako.
 
Back
Top Bottom