Uchaguzi 2020 Sijui Gwajima atatumia Sabuni gani ya 'Kuwatakatisha' Waislamu wa Kawe 'aliowadhihaki' na 'Wakatoliki' waliokwazika naye 'alipomshambulia' Pengo

Duh...!.
P
 
Nadhani watu wa Kawe watamchagua tu huyo anayetaka kubadilisha nyumba za ibada kuwa Sunday school,ksababu wengi walifurajishwa na suala la kumshambulia Kadinali Gego baada ya kutofautiana na wenzie issue ya mahakama ya kadhi na kuunga mkono iwepo
 
Hizo kauli zake zilikuwa zimesahaulika naona zimeibuka tena gafla baada ya kushinda ,hii funzo kwamba kuwa makini na unachoongea itafika mda itakuathiri ,sasa hivi hii hoja yake imeibuliwa upya tena kwa ushawishi mkubwa
"Zilikuwa zimesahaulika, zimeibuka tena ghafla baada ya kushinda", unasema? Baada ya "kushinda" uchaguzi upi? Huu ubabe wenu na kuwafanya Watanzania wapumbavu, safari hii mtatumia mtutu wa bunduki kumtangaza Gwajima.
 
GENTAMYCINE,

Nguvu ya Gwajima ni tume ya uchaguzi na na polisi. Otherwise Mdee bila hata kampeni anapita.

Ikiwa Mdee atafanya kampeni nguvu kubwa ni kuhimiza ulinzi wa kura.
 
GENTAMYCINE,

Kauli ya Gwajima kuwa atageuza Madrasah KAWE kuwa Sunday Schools sio tu ni kupata Laana ya waislam wa KAWE na kunyimwa kura yeye Kama Gwajima,Bali laana hiyo na kunyimwa kura vitasambaa kama Kansa kwa CCM nzima.

Waislam wanasema hawawezi kumchagua Gwajima kwa hilo na pia hawawezi kukichagua CCM ambacho kinaona watu kama Gwajima aliyewadhihaki kuwa ndio watu wanaofaa kwenye Chama chao.

Hii iko applied kwa Wakatoliki kuanzia KAWE na Nchi nzima

Kwa Kumpitisha Gwajima KAWE, CCM imepata laana wa Waislam na Wakatoliki nchi nzima

Hawa hakuna atakayemchagua Gwajima na CCM kwa Ujumla wake.
 
GENTAMYCINE,

Wagombea wote watatu mwenye nafuhu kidogo ni Gwajima tu wengine saa mbili tu asubuhi Halima angefunga hesabu ila kwa Gwajima halima atafunga hesabu kabla mihogo ya kukaanga na vitumbua havijaisha yaan saa nne mpaka saa tano jimbo linachukuliwa na Mdee.
 
Kauli za Gwajima kuwa akiwa Mbunge atavifanya Vyuo vyote vya Kiislamu Kawe kuwa 'Sunday School' na ile Kauli yake ya 'Kumshambulia' Kadinali Pengo ambayo tunajua ndiyo 'Mzizi' Mkuu wa Wakatoliki nchini Tanzania ( na wa Kawe nao wakiwemo ) zisipofanyiwa Kazi mapema tena kwa Gwajima Mwenyewe Kujirudi, Kuzitengua na Kuomba Radhi ( Msamaha ) zinaweza Kumponza.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kweli we ni pompoma unajitengenezea Maneno alafu unamwekea Gwajima hivi unauhakika hii kauli aliongea?
 
Gwajima ni mropokaji namba moja nchini. Tena huropoka "kanisani"

Hivo ataropoka tu kujifanyia kampeni kanisani kwake.

Hilo ni kosa kisheria na kero kwa wasio fuata dini yake.

Pili waislam hawatampa kura na shura ya maimamu hilo suala tayari lipo katika kampeni dhidi yake.

Wakatoliki hawaminiki viongozi wao ni watu maslahi tu ni kama bakwata Pengo anaweza kutumika kwa kumsamehe.

Ila watu wa kawe wanajua gwajima kawekwa na magufuli kwa sababu za usukuma wake na udini.
Hivo watamkata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Gwajima Ni weak candidate against Mdee kusingekuwa na thread nyingiii za kumchafua, hicho Ni kiashiria kuwa anaogopeka


Ni kweli umenena vyema kabisa!

Wanamuona ni threat kubwa zidi ya upinzani Ndiyo maana wana mgwaya!

Gwajima hazuiliki!
 
Alimshambulia Askofu Pengo kama mtu binafsi, lakini alijidai hatambui mamlaka ya Askofu Pengo kikanisa, na alimtukana, mjinga na mpumbavu.
Video hii itamletea taabu sana,lugha aliyotumia ni kali mno.Bahati mbaya Gwajiboy bungeni huwezi kurap,airtime ya bungeni utapewa 15 minutes only,pia kuna point of information huwezi kubwabwaja maneno bila udhibiti wa Spika. Najiuliza na sipati jibu ya Gwajiboy kusaka ubunge ni faida ya nani?
 
Sioni tatizo kwa Gwajima kugombea Jimbo la Kawe na ukizigangatia anayo haki ya kikatiba, kama issue ni hiyo video clip yake inayozunguka kwenye Mitandao ikihusu ndoto ya misikiti kuwa Sunday school akisimulia waamini wake pia itachekesha ikiwa Halima au Chadema watasimama na agenda mfu hii.

Waislam siyo wote watakaolishwa tango pori mmoja wao ni Mimi na kama ilikuwa na madhara bila shaka hatua za kisheria zingechukuliwa dhidi yake kama ilivyokuwa kwa Askofu Pengo ingawa sikujua kesi ile kama ilimkuta Gwajima na hatia au la!
 
Jana nilikua kawe jamaa wanasema hatuna maneno mengi wamlete huyo askofu wao tapeli kazi ni moja tuu.nikajisemea kimoyomoyo kumtawala msomi ihaitaji akili ya ziada. Bora wangempeleka akagombee mvumi huko dodoma vijijini.
Au Mtera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…