Uchaguzi 2020 Sijui Gwajima atatumia Sabuni gani ya 'Kuwatakatisha' Waislamu wa Kawe 'aliowadhihaki' na 'Wakatoliki' waliokwazika naye 'alipomshambulia' Pengo

Kiongozi yupi wa dini kiislamu aliemuita mkristo kafil Kisha akataka madaraka yakisiasa wakristo wakampigia Kura? .
 
Kuikashifu dini yetu kwako linaweza kuwa jambo dogo, lakini kwa muislam hakuna cheny thaman zaidi ya dini yake.
 
Ukiwa ccm unaongea tu mwanzo mwisho, na ukikatishwa hata Segundo, wanakufidia 15 zingine.
 
Kuikashifu dini yetu kwako linaweza kuwa jambo dogo, lakini kwa muislam hakuna cheny thaman zaidi ya dini yake.


Tupendane sisi wote ni waTz tunajenga nyumba moja ya Taifa Tanzania!

Familia zenyewe tumeingiliana wa dini zote na wasio na dini!

Dini zenyewe zimefanya kuletwa na Melikebu toka mbali!

Tuache kuhusudu vijimaneno vitokanavyo na mihemko ya wahubiri au watoa mawaidha!
 
Kiongozi yupi wa dini kiislamu aliemuita mkristo kafil Kisha akataka madaraka yakisiasa wakristo wakampigia Kura? .


Hata ikitokea nakwambia wakristo siyo watu wakujali mambo madogo hivyo!

Wakristo si watu wa visasi maana maandiko yameainisha wazi marufuku kulipiza visasi la sivyo mabaya hayataisha kukupata!

Wakristo wanaamini MwenyeEnzi Mungu ndiye Hakimu wa haki wa kujua kumlipa mtu aliyekosea!

Wakristo wanaamini ktk kupigwa shavu moja na kugeuza lingine lipigwe!

Hata hivyo mimi mpaka sasa sijaamua niwe wa dini gani maana baba yangu mzazi ni Muislam na mama ni mkristo.

Sasa bado naangalia badae nichague dini moja kati ya hizo mbili , bado najifunza mambo yao!
 
Viongozi wadini wabaki katika dini zao viongozi wakisiasa watumikie siasa zao. Narudia kukueleza hakuna muislam anaweza mchagua Gwajima, Halima pia nimkristo lakini waislam wako tayari kumchagua Halima maana hakuna mahala popote alipoikashifu dini yamtu mwingine. Au Mkristo yeyote atachaguliwa na waislam lakini sio yule anaesimama hadharani kutukashifu, mtu anaekashifu kabla hajapata madaraka,akipata itakuwaje?

Kama mngehitaji hata hili lisizungumzwe basi mgeleta mgombea ambae hatoneshi nafsi zetu katka dini zetu. Mimi nimuislam na ntashawishi waislam wenzangu wakawe tumsichague Gwajima kwa sababu Gwajima nimdini na ameonesha chuki zake juu yetu waislam.
 
Pamoja na Ulofa wako angalau Leo umenena la maana, Kwa niwajuavyo ndugu zangu wa kikatoliki watakua wanapandishwa katika majukwaa yake ya kampeni ili kumsafisha kwanza baada ya kupewa mlungula
Njaa mbaya sana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Usitupangie kawe sisi ni Halima mdee.maaskofu wahuni huni hawana nafasi.
 
Hili jimbi limepata laana, mmoja ni shetani na mwingine ni msagaji. Iko kazi kwa wana kawe.
 


Halahala usijedakwa wakati wa kuwashawishi ukaonekana unaleta uchochezi ukatiwa nguvuni!

Yani tunaweza kujadili yote hapa tukamaliza lakini ukweli ni kwamba jamaa hazuiliki!

Halafu tusijidanganye na mambo ya humu kwenye mitandao!

Wapiga kura wapo mtaani ambao wenyewe wanachotaka ni mtu wa kushirikiana na serikali kuleta maendeleo na siyo mihemko ya udini.

Ni wazi kuwa kuna kundi la watu waovu, Matapeli, wavamizi wa ardhi na maeneo ya watu tangu wasikie jina la Gwajima hawalali sababu wanajua mambo yao ya uovu yanakwenda kukoma .

Ndiyo maana wanakesha mitandaoni kwa kutafuta vijisababu visivyo na maana ili mradi wanazani itasaidia kumkomoa Gwajima lakini Gwajima hazuiliki!

Kwa hatua ilipofika jamaa hazuiliki!

Bora kuanza kumpenda na kushirikiana naye ili kuyajenga pamoja kama ambavyo tunapaswa kumpenda Magufuli na kumuunga mkono sababu naye hazuiliki!
 
Usitupangie kawe sisi ni Halima mdee.maaskofu wahuni huni hawana nafasi.


Wananchi hawapo after mtu fulani wao wapo after mtu atakaeshirikiana vizuri na serikali kuleta maendeleo!

Itakuwa ajabu sana kama siyo ujinga kwamba eti Mtu uache kuchagua mtu atakaeshirikiana serikali kuleta maendeleo jimboni badala yake ukachague mtu ambaye atakuwa anaendesha kesi zidi ya serikali na kupoteza muda kwa miaka 5 ili hali maendeleo yanasuasua!

Haipaswi kuchagua kwa kumkomoa mtu fulani siyo Busara maana mwisho wa siku wananchi wanataka maendeleo na siyo mtu tu!
 
Kuikashifu dini yetu kwako linaweza kuwa jambo dogo, lakini kwa muislam hakuna cheny thaman zaidi ya dini yake.


Labda wa siku hizi sababu kwa kuzisoma hadithi za Mtume M. S. W. Yeye alijaa subira!

Kwa kuwa bado najifunza Habari zake kwa haraka haraka sizani kama alikuwa mtu wa visasi!

Maana kuna wakati mtu alienda kujisaidia msikitini wafuasi wake walipotaka kumdhuru aliwakataza kabisa badala yake akawaambia wasafishe wapige deki na kumuacha!

Mwishoni yule mtu alirudi kuomba msamaha na akataka atiwe maji awe Muislam sababu wakati ule ilionekana kuwa na amani!

Sasa Kwani siku hizi mmekuwa wa tofauti?

Mtu kama mzee mwinyi ni miongoni mwa wanaoutangaza uislam vizuri sana na Ndiyo maana Mungu anamuweka !

Na atazidi kumuweka InshaAllah maana hanaga ubaya wala nongwa !

Tuepuke kuhusudu vijimambo vidogo vidogo!

Mimi nakwambia yanayosemwa na watoa mawaidha wa dini ya kiislam kwa miaka mingi sana kama wakristo wangekuwa watu wakuyahusudu hayo wanayosemwa nazani amani kwenye jamii ingekuwa mashakani siku nyingi!
 
Haishangazi sana kwangu mimi. Hii ni matokeo ya ccm ya sasa. CCM sasa siyo taasisi tena, bali ni mali binafsi ya mtu binafsi anayeitwa John Joseph Pombe Magufuli. CCM ya Nyerere, japo alikuwa na influence kubwa sana, ilibaki kuwa Taasisi kamili, na hivyo iliwahi kufanya maamuzi ambayo Nyerere hakuyapenda lakini aliyapokea kwa kuwa yalikuwa maamuzi halali ya kikao.

Siwezi kujenga picha kikao kikubwa cha CCM chini ya uenyekiti wa Magufuli , kiamue tofauti na mtizamo binafsi wa Magufuli.
Ushahidi angalia suala la waraka wa Kinana na Makamba lilivyoshughulikiwa. Majungu ya Musiba wala hayakuguswa, mpishi wa majungu wala hakuguswa, ila walalamikaji ndio wakashughulikiwa, tena kwa kuvunja sheria za nchi.

Njia pekee iliyokuja "kuwaokoa" wala haikuwa vikao vya CCM, bali kumwomba radhi Magufuli binafsi.

Pamoja na Bashiru Ali, Katibu Mkuu, kufafanua kwamba pamoja na kuomba radhi, bado "watuhumiwa" watawajibika mbele ya chama, hiyo wala haikuwa ishu. Sasa inadhihirika kwamba Makamu Mkiti, Katibu Mkuu, naibu katibu mkuu bara na visiwani, vyeo vyote hivyo vimekusanywa na mtu mmoja tu: JPM. Yeye ndio CCM, na CCM ndio yeye. Na ndio maana hata akipigiwa kura hupata 100%. Msimamizi gani wa kura ya kumthibitisha Magu, atatangaza ushindi wa chini ya Asilimia 100?
 
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema, amemsamehe Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima alimtolea maneno makali kutokana na kutofautiana naye juu ya msimamo wa viongozi wa Kikristo kuhusu Katiba Inayopendekezwa
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Angekuwa Sheikh angetukanwa matusi yote.
 
Kwako mkuu kuikashifu dini yetu waislam linaweza lisiwe Jambo la maana lakini sio kwetu sisi waislam, dini yetu kwanza Mambo mengine baadae. Kama huamini nayokueleza kuhusu Gwajima naomba tusubiri baada ya octoba 28 tutarud hapa, kama Jimbo lakawe atalichukua huyo muhuni anaechafua dini zawatu.

Kama vyombo vya dola vilishindwa kumtia nguvuni Gwajima ambae alikuwa anatangazia watu wafungua Whatsapp group za kisukuma ili waweke mikakati msukuma mwenzao ashinde, wanashindwa mkamata Gwajima anaejirekodi huku akifanya zinaa kinyume kabisa na maadili na utamaduni wa mtanzania basi hawana uwezo wakukikamata Mimi.
 
Hakika mkuu Ritz
 
Sasa sisi ndio wananchi hatupangiwii. Kama mnampenda sana huyo gwajima kanyweni nae chai chamwino
 
Ktk kupambana kutafuta ugali mambo mengi sana hujitokeza njiani, kuna kujikwaa, kuanguka, n.k.tuvumiliane na kusameheana sana watanzania hasa vijana, kama gwajima hana sifa za uongozi basi tusimchague kwa sbb hiyo ila kamwe tusimhukumu kwa mapito yake aliyopitia ambapo hata sisi pia tunayo ya kwetu, Ni Mungu tu ametusitiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…