Kwa kweli sikutegemea chama Kili kingeweza kufanya makosa haya ya kumchagua mtu kama Gwajima! Kigeugeu! Mwenye cotroversies nyingi mno pamoja na matendo na lugha za kiajabu mno!
Kama dira ya ccm ya watu bora ni mfano huu basi inatia shaka ccm wana nia gani na nchi hii!
Haishangazi sana kwangu mimi. Hii ni matokeo ya ccm ya sasa. CCM sasa siyo taasisi tena, bali ni mali binafsi ya mtu binafsi anayeitwa John Joseph Pombe Magufuli. CCM ya Nyerere, japo alikuwa na influence kubwa sana, ilibaki kuwa Taasisi kamili, na hivyo iliwahi kufanya maamuzi ambayo Nyerere hakuyapenda lakini aliyapokea kwa kuwa yalikuwa maamuzi halali ya kikao.
Siwezi kujenga picha kikao kikubwa cha CCM chini ya uenyekiti wa Magufuli , kiamue tofauti na mtizamo binafsi wa Magufuli.
Ushahidi angalia suala la waraka wa Kinana na Makamba lilivyoshughulikiwa. Majungu ya Musiba wala hayakuguswa, mpishi wa majungu wala hakuguswa, ila walalamikaji ndio wakashughulikiwa, tena kwa kuvunja sheria za nchi.
Njia pekee iliyokuja "kuwaokoa" wala haikuwa vikao vya CCM, bali kumwomba radhi Magufuli binafsi.
Pamoja na Bashiru Ali, Katibu Mkuu, kufafanua kwamba pamoja na kuomba radhi, bado "watuhumiwa" watawajibika mbele ya chama, hiyo wala haikuwa ishu. Sasa inadhihirika kwamba Makamu Mkiti, Katibu Mkuu, naibu katibu mkuu bara na visiwani, vyeo vyote hivyo vimekusanywa na mtu mmoja tu: JPM. Yeye ndio CCM, na CCM ndio yeye. Na ndio maana hata akipigiwa kura hupata 100%. Msimamizi gani wa kura ya kumthibitisha Magu, atatangaza ushindi wa chini ya Asilimia 100?