Uchaguzi 2020 Sijui Gwajima atatumia Sabuni gani ya 'Kuwatakatisha' Waislamu wa Kawe 'aliowadhihaki' na 'Wakatoliki' waliokwazika naye 'alipomshambulia' Pengo

Mwenye ile clip ya Halima akimtishia mgombea urais 2015 kuwa "akipiga push up tena watamuitia Juma Nyoso" aiweke hapa. CCM wameleta jeshi la mtu mmoja bingwa wa kurusha maneno ili waone kama Halima atapita kwa "mitusi" yake! Naona wana kawe ni wapenzi wa MIPASHO hahahah!
 
Mbona Gwajima anashinda mapema tu pale kawe.

Halima ajiandae kupisha Jimbo,

Kumi yake inamtosha.
 
Nawalaumu sana 'Research Team' ya CCM kwa Kushindwa Kwake 'Kumshauri' vyema Mwenyekiti Taifa Rais Magufuli juu ya hili. Ninaogopa mno tu!
Research imefanywa na Eagle house, na Mzee hapinduwi kwa wale jamaa, wamemsaidia sana na anawaamini sana.

Watanzania wamekosewa sana na ccm kuliko huyo Gwajima na bado wanaipigia kura ccm
 

Namba mbili hajawahi kututukana wakatoliki hata siku moja usimlishe maneno, na kama unao ushahidi wa kututukana wakatoliki uweke hapa.

Namba tano hayo makanisa ya kilokole ni Saccos za watu, huwezi kumshitaki au kumtuhumu Maxence Melo eti ni mbadhirifu wa pesa za JF, huo utakuwa ni utahaira, mtu huwezi kumuita mbadhirifu kwenye mali zake, kasome katiba za makanisa yao utaelewa.
 
Pamoja na Ulofa wako angalau Leo umenena la maana, Kwa niwajuavyo ndugu zangu wa kikatoliki watakua wanapandishwa katika majukwaa yake ya kampeni ili kumsafisha kwanza baada ya kupewa mlungula
Labda wale wakatoliki hoho wachumia matumbo, wale wenyewe huwa wana misimamo yao inayojulikana
 
Binafsi nahisi labda baada ya kuonekana nepotism kwa mpwa, nafikiri CCM jimbo la Kawe, wameamua kuliachia upinzani!

Gwajima siyo sabuni tu, anahitaji jiki na brashi ya chuma, sijui muda ni mwalimu.

Everyday is Saturday.......................... 😎
 
Kwahiyo Gwajima kamfuta bashite kaingia yeye au bashite atapangiwa kazi nyingine? Naskia anaenda kuwa balozi nchi flani ya ughaibuni!!
 
CCM yangu wameniudhi Sana kutuletea Gwajima Kawe.Watia Nia ya ubunge CCM Kawe walikuwa 170.yaani katika wote hao wakaona Gwajima ndo anafaa ! Walikuwepo Akina mtoto wa Samwel Sita,Akina Francis Nanai,nk mkawaacha.Aisee hii imekula kwetu CCM.Miye Kura yangu ya u-rais Nampa Magufuli ubunge sitampa Gwajima.Sitaki kuwa mnafiki.
 
Gwjm Mzee wa pangaboi bin miuno isiyo mfupa amekalia kuti kavu kwenye mnazi ambalo 2020 hii litaanguka pasipo shaka kwa zambi za kungonoka, kutukana dini za watu na hata viongozi wa dini. Mimi MKAMA NDUME can't cast vote for him yy aendelee na miuno yke ya Zipompa pompa makalio meusi kama blk kiwi.
 
Yaani hapo mkuu mimi ndiyo nimekua serious kwa viwango cha Pi echi dii😁😁.
Halafu huwa sikwaziki na majibu yako, huwa nacheka tu.

Kingine huyo Gwajima mwenyewe uliyemfungulia uzi is just a joke, sasa naanzaje kuwa serious!
Ahahahh,eti Gwajima is a joke
 
Huyu mzee angeielewa tu ramani ya Kawe mapemaaaa, wala asingejisumbua. Alikuja Kippi kabla ya kuteuliwa ingawa na yeye ni mtoto wa huku, kilichomkuta anakijua. Sasa huyu wa Kolomije na kutukana watu juu, hajistukii tu!?

Alijiona yupo crrdible kutukana na kudhalilisha watu kipindi Packers inatema, leo hii anataka apatumie pale pale kuombea kura. Hivi unathubutu vipi kumtukana mtu anayeweza kukuzaa tena mbele ya halaiki na bado ukajinasibu kuwa wewe ni mtumish wa Mungu!?
 
Kwa jinsi kashfa za utapeli, uongo, mambo mbali mbali zinazo ibuliwa kwa mgombea wao hata kabla ya kampeni kuanza wamesha ona walifanya papara kumpitisha Gwajima.

Sasa hivi yale mambo ya kufufua watu, kumtukana Askofu Pengo, picha za ngono na kubadili madrasa za kiislamu kuwa Sunday schools ndio yanaibuliwa kwa nguvu sana hakuna mfano na muda wa kumsafisha hakuna.

Ni bora hata wangempitisha mwenzetu Pascal Mayalla asiye na kashfa
 
Ukiachia mbali tu la Ukatoliki, ila Mkuu hakuna Jimbo lenye wana CCM 'Wanafiki' kama la Kawe. Gwajima na CCM yake wanaweza wasiamini kabisa.
Sisadiki sana usemayo ndugu, ila nataka nikukumbushe tu jambo moja. Jimbo la Kawe naweza kusema ndilo jimbo ambalo linakaliwa na Vibopa wa Biashara Kubwa kwa Tanzania, hivyo ili wafanye biashara zao vizuri wanaona ni bora wajivike viremba vya usisiem bila kupenda ili mambo yao yasonge. Isingekuwa hivyo, ungeshangaa mwenyewe kila kukicha CCM wanavyochakazwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…