Uchaguzi 2020 Sijui Gwajima atatumia Sabuni gani ya 'Kuwatakatisha' Waislamu wa Kawe 'aliowadhihaki' na 'Wakatoliki' waliokwazika naye 'alipomshambulia' Pengo

Uchaguzi 2020 Sijui Gwajima atatumia Sabuni gani ya 'Kuwatakatisha' Waislamu wa Kawe 'aliowadhihaki' na 'Wakatoliki' waliokwazika naye 'alipomshambulia' Pengo

Pamoja na Ulofa wako angalau Leo umenena la maana, Kwa niwajuavyo ndugu zangu wa kikatoliki watakua wanapandishwa katika majukwaa yake ya kampeni ili kumsafisha kwanza baada ya kupewa mlungula.
Wakatoliki hatuko na hiyo tabia.

Mimi ni voter wa Kawe. Nakuambia Gwajima hatapata kura za maana kutoka kwa wakatoliki na Waislamu.

Hapo Magufail kafeli kweli kweli.
 
Hizo kauli zake zilikuwa zimesahaulika naona zimeibuka tena gafla baada ya kushinda ,hii funzo kwamba kuwa makini na unachoongea itafika mda itakuathiri ,sasa hivi hii hoja yake imeibuliwa upya tena kwa ushawishi mkubwa

Nilishtuka na Kushangaa sana baada ya Kuona na Kusikia kuwa CCM 'imempitisha' Gwajima Kugombe Jimbo la Kawe. Mdee akijipanga analishinda.
 
Wameshachelewa na ninachojua tu ni kwamba kama kuna Jimbo ambalo Askari Polisi na FFU wengi watajaa wakati wa Kutajwa Matokeo ni Kawe.
Hilo ni kweli ila hii itachafua taswira halisi ya Tanzania, Dar es salaam na Kawe binafsi natamani uchaguzi uwe huru na haki maana kuna maisha baada ya uchaguzi.

Mungu ibariki Tanzania
 
Mimi si Mkatoliki ila wakatoliki wengi wana misimamo thabiti linapokuja suala la kashfa na dharau kwa viongozi wao

Ukiachia mbali tu la Ukatoliki, ila Mkuu hakuna Jimbo lenye wana CCM 'Wanafiki' kama la Kawe. Gwajima na CCM yake wanaweza wasiamini kabisa.
 
Nawalaumu sana 'Research Team' ya CCM kwa Kushindwa Kwake 'Kumshauri' vyema Mwenyekiti Taifa Rais Magufuli juu ya hili. Ninaogopa mno tu!
Hao ccm huwa wanatumia mabavu sio akili. Ningeshangaa kama wangetumia akili kufikiri.

Sasa huyo Magufuli lini kawahi kushaurika?

Kilichokuwa kinnangaliwa ni msukuma gani anaweza kupiga kelele zaidi ya mwenzake, siyo kupata muwakilishi.

Huyo Gwajima anataka ku prove kwa waumini wake kwamba anaweza kufanya lolote na chochote, akiwadanganta ni nguvu ya Mungu.

Sijui kwanini hawakumtumia kule Lupaso kumfufua aliyefariki, ningewaona wanaakili japo kidogo. Maana anajiitia anaweza kufufua watu, hiyo ingekuwa litmus test kwake.
 
Huenda Pengo na waislamu walishamsamehe Gwajima hivyo hayo yameshapita, sasa tunaganga yajayo.

Kila laheri Askofu Gwajima na wagombea wengine wote.

Nadhani huwajui 'Waislamu' hasa wa Jimbo la Kawe na 'Wakatoliki' Kiujumla walivyo na 'Misimamo' yao na wanavyojua 'Kumchinja' Mtu kwa Kura.
 
Back
Top Bottom