Sijui kama waheshimiwa wetu wanapitia hii changamoto

Sijui kama waheshimiwa wetu wanapitia hii changamoto

Librarian 105

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
261
Reaction score
356
images(3).jpeg

Kumekucha tena wanajukwaa la JF,

Msakatoke mwenzenu nimejaliwa siku mpya tena pamoja na familia yangu. Ntakua mchoyo wa shukrani bila kusema: Asante Muumba kwa siha njema na faragha. Amma baadu, bada ya utangulizi na shukrani.

Siku ni mpya. Nmeamka na maumivu ya deni la mangi shop. Watoto wanadai kitafunwa na chai, mamie wana anataka kodi ya meza, nauli za shule na hela ya mkakati, nikichek bajeti mfukoni ni nusu kanzu, naacha familia kwa saundi za mke ajiongeze mi' ntamcheki kwa simu.

images(4).jpeg

Natoka nje, hamadi! Father house anaswaki uani, nampa salamu lkn anajibu kwa kupunga mkono hali amenipa mgongo. Nawaza dharau gani hii. Ila nikiwaza kodi yake nimechelewesha, nachanganya hatua na kupita vichochoroni mana nina RB kwa mama wa vitumbua na mangi shop.

Siku inaanza kwa stress za maisha yaani. Ghafla nawaza naanzaje kuimba kiitikio cha wimbo "Tanzania kisiwa cha amani" ila uzalendo kwa nchi yangu naimba na kunema huku na kule kwa raha na karaha. Nikiamini ukombozi upo njiani wa njia ya amani na utulivu kwa kushirikiana na makamanda wangu wa mapambano ya kalamu.

Naazimia kuufuta ujinga wa familia yangu kwanza, mzuka umepanda hadi kazini, masela wasua wanauliza vipi?! Nawatoa tongotongo za uoni hafifu na ugando wa mitazamo. Tuchape kazi, tuchape kazi, tuchape kazi, tunaimba na kupokezana verse ya "mabadiliko yanaanza na mimi". Songi halina jina kwani nawaza: hivi muheshimiwa nae anamaliza siku na kuianza siku nyingine kama mimi?!

Ipo siku tutafahamiana.
 
Back
Top Bottom