Sijui kwanini nimeumia hivi

Asante mkuu kwa ushauri mzuri 🙏🙏
 
Pole sana aisee.. Walau nimepata ahueni baada ya kuandika hapa maana nilikua naumia tu ndani kwa ndani
Utakuwa sawa ni suala la muda tu, mimi huwa nachekaga tu kama kontawa.

Watu wasichokijua watu wenye mioyo ya kusaidia ni wengi ila wenye uwezo wa kusaidia ni wachache mno na hustahili kuwapoteza hata mmoja labda wapoteze uhai.
 
Ushauri mzuri sana

Unasaidia ulichonacho, unatoa sadaka ulichovuna wewe.

Sio ukope halafu usaidie, au katoe sadaka haiji. Wenye hekima walishasema kopesha kile unachoweza kupoteza. Sasa iweje ukopeshe kile usichoweza hata kuafford!! Why
 
Watu wengi hawana shukrani na ni wanyenyekevu tu wakiwa na shida. Inaumiza mbaya aisee lakini wewe kausha na kuna siku atakuja kwenye 18 zako.
 
Duuh...! Nimeumia pia. Najua situation uliyopitia. Ndivyo MUNGU alivyopanga kwa tukio lako.

Fanya hivi nenda kamjulie khali na mwambie yote. Pia mwambie tu hajakufanyia sawa. Ukitoka hapo moyo wako utaachia. Pia naomba nieleweke maana ya kumwambia ni kuondoa mashtaka yako kwa MUNGU. Ksbb ukikaa kimya ukaendelea kuumia peke yako Kwanza utakuwa unaendelea kujiumiza hata wewe. Pili ukikaa kimya na ukasamehe bila kuongea nae wazi ni shtaka kubwa sana mbele za MUNGU.

Kwa hiyo nikuombe ukaongee nae. Ili pia uutengeneze moyo wako. MUNGU akupe wepesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…