Sijui kwanini nimeumia hivi

Mbona mimi ni wa kike mkuu😃😃
 
Na usikute hata hizo kilo kilo za vipimo anaweza kuwa alipiga michongo na daktari wakupune wewe "chuma ulete" wao
Hapana mkuu, siwezi tu kuanika tatizo ila mtoto alikua anaumwa very serious
 
Duuh, sawa.. Ila nadhani ungesoma kwanza kwa utulivu na kunielewa, ni sahihi kwake hata hajanipa taarifa kama wameruhusiwa na wanaendelea vizuri hadi narudi tena hospitali hawapo??? Seriously??
 
Hello Ms Leejay49 , Pole sana kwa hili lilikutokea na ndivyo ilivyo watu wenye moyo wa huruma kama wewe ni wepesi sana wa kuumizwa. Ninachokushauri jitahidi sana kufanya mambo kwa kiasi na ukifanya jambo fanya pasipo kutegemea kupewa feedback au shukrani yoyote. Najua sana umbali wa kutoka Songea mjini mpaka Peramiho ni 25KM. Huyo Shoga yako hana shukrani ishi nae kwa akili na usijitoe sana kwake na hata kama unamsaidia msaidie nusu nusu sio full msaada, kwa mfano akitaka 10,000 mpe 7000 au 5000 tu na usitegemee shukrani
 
Jifunze


Jifunze haya mambo

Source
Giver
Taker

Ukielewa haya mambo you will be disappointed .

Shukrani kubwa ambayo unabidi kuipata ni kuhakikisha umegusa maisha ya MTU in positive way .

ntarudi Ahsante.
Sawa
 
Asante mkuu, inabidi nianze kujifunza roho mbaya
 
Watu tumetoka kwenye kaubavu kenu halafu mnataka tufanane. Huwez pingana na nature, mwanaume ni mwanaume tu.
 
Nakushauri,usiumia sana, umetumiza wajibu wako,endelea na maisha. It happened to me miaka kadhaa iliyopita,nilimpigania sana mtu kupata kazi sehemu, alipoandaa keki ya kushukuru, hakunialika kabisa
 
Kuna watu wanafanya wengine washindwe kusaidiwa sababu ya tabia zao..!!

Tenda wema nenda zako! Shida haina siku moja. Atarudisha mironjo yake siku nyingine watu wa aina km hiyo huwa hawana aibu kuomba tena msaada..!!

Nikwambie kitu wala usihuzunike na kuvunjika moyo. Kwanza hapo umeokoa maisha ya mtoto ambaye hajui chochote kuhusu dunia hii. Baraka zako zipo kwa huyo mtoto na sio mama yake, Mungu atakubariki zaidi ulipotoa na usife moyo siku nyingine kusaidia wengine..!!
 
Hongera kwa kutenda wema and the good thing umemtendea mtoto (aliyeugua) hesabu hiyo kuwa ni sadaka. Ni vyema sasa umefahamu ya kwamba unaedhani ni rafiki yako ni TAPELI so utakuwa makini naye
Be blessed kwa msaada uliotoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole mkuu. Hata Mimi nimehisi kama Mimi ndiye niliyefanyiwa. Cha msingi elewa kuwa urafiki wa huyo upo kimaslahi zaidi
 
Huna haja ya kusubiri hiyo taarifa wala asante yake. Ukifanya jambo amua unalifanya kwa ajili ya wewe na sio kwa ajili ya mtu mwingine. Kwa hiyo ukifanya unakuwa umetimiza nia yako na kama mazingira hayakupi favour kuendelea na hilo, unaishia hapo kama ilivyotokea kwako.
 
Pole sana
Kwani ulimsaidia Ili akulipe wema?au atoe shukrani?
Wema wako Mungu ndo anajua na atakulipa kupitia Kwa wengine ila binadamu Huwa hatuna shukrani Wala hatulipi jema Kwa jema
 
Ndio maana mimi sipendagi ujinga, acha wakuone na roho mbaya tu, unaweza kujitoa kumsaidia mtu na kumsomesha lakini na bado asione thamani yako ni kawaida tu, wewe ili moyo wako uwe na amani mchana aisee, mwambie ukweli kabisa ili uwe huru.
Pole Sana,Katika nafsi yako Na Moyo Wako Mkaribishe Mungu,Hesabu umetoa sadaka,peleka Maombi yako Kwa Mungu atakuondolea Maumivu Na utaendelea kusikia furaha
 
Y
I hope hamna common friends maana kituo kinachofata ni "yule mnavoona ana kazi kumbe poyoyo, hela anaomba kwa wazazi wake...hana lolote...."
Yaani😃😃😃, Mbona nitafedheheka😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…