Sijui kwanini nimeumia hivi

Iliwahi kunitokea nashukuru nilisahau hata alivonitafuta miezi saba badae sikuwa na kinyongo naye


NB single mom hawasaidiwagi
 
Nahic hata hakukutaja kwenye screenshot hiyo ya miamala mwambie ahsante kama mtoto amepona tu bc sio rfk huyo endelea na yako
 
Pole sans mkuu, lakini jifunze siku nyingine mwanamke aliezaliswha na mtu usihangaike nae utapotea. Shukuru kaposti miamala, je angepost kaenda kwa jamaa na alisema hapokei simu kumpa hela ya matibabu ya mtoto ungejisikiaje japo sio mpenzi wako. Anyway huend anataka kuja kukupa SPECIAL THANKS kuwa mvumilivu ule tunda.
 
Wewe utakuwa pacha wangu manake una roho mbaya kama mimi na akili kama zangu🤣🤣
 
Ubinadamu kazi my dear

And it's okay moyo kukuuma

Lakini usiruhusu kuumia sana

Take it easy, umefanya kwa nafasi yako kadri ulivoweza

Mengine mwachie yeye na Mungu wake watajuana wenyewe
 
Mpigie simu toa dukuduku lako au mtumie sms then kata mawasiliano nae, watu ni washenzi saana
 
Huyo atakuja tena mwenyewe shida haziishi na sikuzote jua mkataa pema pabaya panamwita huyo akirudi na shida usimuonee tena huruma mwache afe na matatizo yake kuna watu hawastahili huruma ni vile tu tunajipendekezaga
 
Siku zote ishi kwa kusaidia bila kutegemea malipo yeyote. Iwe ya shukrani ama chochote.

Kwa sababu hata shukrani isingekuongezea chochote.
Shukrani inafaida kubwa sana kwa pande zote mbili ndio maana kwenye dini pia kuna kutoa sadaka.

Kutokutoa shukrani kunaweza mfanya mtu asisaidie tena mtu yoyote kwa kujitoa kiasi hicho, shukrani ni lazima na muhimu sana.

Hizi stori za sijui tenda wema nenda zako ni kama zimepitwa na wakati, sahivi tenda wema alafu kaa angalia huo wema umeleta faida gani au umetapeliwa na wahuni. Muhimu kujua na kujifunza pia.
 
shida ni kwamba ulikuwa unasaidia mtu ili upate credit/shukran. unaposaidia mtu, saidia kama kwa Mungu, usitegemee shukrani, akikushukuru umeshapata thawabu au kwa lugha nyingine shukran izo ziende kwa Mungu ili Mungu akubariki wewe, ukizipokea wewe basi umekwishapata thwawabu hivyo hutabarikiwa. wewe saidia, nenda zako, kama amekudanganya sawa asipokudanganya sawa, atajuana na Mungu huko huko na ni Mungu ndiye anatoa thawabu sirini.
 
tukiwaambia mtu anayebeba mimba akiwa bado hajaolewa ana kasoro zake muwe mnaelewa, nyie mnawaita single mother
amewafanyia dharau wazazi wake , ndugu zake wa tumbo moja. amekuja amevurugana na aliyemzalisha, wewe ndo atakupa heshima.
Pole sana
[emoji16]
 
Siku zote ishi kwa kusaidia bila kutegemea malipo yeyote. Iwe ya shukrani ama chochote.

Kwa sababu hata shukrani isingekuongezea chochote.
Huyu bidada siyo chuma au jiwe ni binadamu lazima atamani na yeye kutambuliwa mchango wake kwa vile msaidiwa kaamua kuwataja wahisani wake naye alipaswa kumtaja.
Tusiweke unafiki hata wewe na sisi tungeumia.
Huoni mfano mabango ya KWA HISANI YA WALIPA KODI WA MAREKANI au JAPAN?
 
Huyo mdada ulimsaidia hela ambayo ingetosha matibabu yote kwa hiyo kukuandika hapo status ingezua taharuki kwa wale wengine waliochanga pesa ndogo ndogo .HAPO HAJAKUWEKA WW ILI KUJILINDA YEYE SIO KWAMBA AMEKUDHARAU .ILA AMESHINDWA KUKUPA TAARIFA NA PIA HANA AKILI NZURI MANA ANGEWEZA HATA KUKUWEKA STATUS UONE PEKE YAKO MUAMALA ULIO MTUMIA.
 
Dada Leejay49 nimeyavaa maumivu yako yamenishinda na mimi nimejikuta naumia kama vile yamwnikuta mimi .
Watu wema ila watu wabaya , njia nzuri jitahidi kusahau hayo , futq namba ya huyo mchawi , anza maisha mapya bila kukumbuka uliwahi kujuana na Shetani wa aina hiyo
Usimpe tena hata chance ya kupiga story na wewe mfute maishani mwako huyo sio rafiki , sio ndugu , sio mtu mwema hata kidogo .
Wahenga walisema tenda mema nenda zako ila haikuwa utende wema uende kama hivi ulivyoondoshwa dada Leejay49 samehe ila usimsahau .
Pole sana , nasikitika na wewe na pia naumia na wewe , karibu Chabruma tupige story
 
Tenda wema uende zako na pia shida zina tabia ya kuwarudisha watu kwa watu waliowakosea. Aombe sana huyo dada asipate shida itakayohitaji msaada wako maana atashindwa kukurudia kwa kuona aibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…