Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe utakuwa pacha wangu manake una roho mbaya kama mimi na akili kama zangu🤣🤣Kuna watu wana roho za tofauti sana na huyo shoga ako ana tabia za kiswahili. Ndio umeumia sana lakini overtime utakua sawa.
Cha kufanya delete namba yake akikutafuta muulize yeye nani. Mpotezee mazima hafai kabisa. Amekuona wewe ndio chuma ulete wake
Shukrani inafaida kubwa sana kwa pande zote mbili ndio maana kwenye dini pia kuna kutoa sadaka.Siku zote ishi kwa kusaidia bila kutegemea malipo yeyote. Iwe ya shukrani ama chochote.
Kwa sababu hata shukrani isingekuongezea chochote.
shida ni kwamba ulikuwa unasaidia mtu ili upate credit/shukran. unaposaidia mtu, saidia kama kwa Mungu, usitegemee shukrani, akikushukuru umeshapata thawabu au kwa lugha nyingine shukran izo ziende kwa Mungu ili Mungu akubariki wewe, ukizipokea wewe basi umekwishapata thwawabu hivyo hutabarikiwa. wewe saidia, nenda zako, kama amekudanganya sawa asipokudanganya sawa, atajuana na Mungu huko huko na ni Mungu ndiye anatoa thawabu sirini.Habari za asubuhi wana JF,
Iko hivi, nina rafiki yangu ana mtoto (naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae O level huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.
Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia.
Nilimkuta yuko good ila mwanaye alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana hela na almost kila aliyempigia simu wamemuahidi tu tangu asubuhi na hakuna aliyemtumia mpaka muda huo sa 1 jioni inaelekea saa 2.
Kiukweli sikua na hela and i was totally broke, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu. Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela, kweli tukamshawishi mzee bila hiyana akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule.
Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine (muda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje.
Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa (Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki 2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha. Kwasababu kazini walikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena.
Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi Peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa. Jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtumia hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini. Screenshot kama kumi na kitu hivi na amewataja na majina kabisa...
Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia siku ileile ambayo aliniambia na mimi niende kwake kumuona( Nilikua nasoma tarehe na muda wa zile transactions ).
Mimi ambaye nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma.
Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee, sijui nifanye nini nikae sawa😥😥
[emoji16]tukiwaambia mtu anayebeba mimba akiwa bado hajaolewa ana kasoro zake muwe mnaelewa, nyie mnawaita single mother
amewafanyia dharau wazazi wake , ndugu zake wa tumbo moja. amekuja amevurugana na aliyemzalisha, wewe ndo atakupa heshima.
Pole sana
Huyu bidada siyo chuma au jiwe ni binadamu lazima atamani na yeye kutambuliwa mchango wake kwa vile msaidiwa kaamua kuwataja wahisani wake naye alipaswa kumtaja.Siku zote ishi kwa kusaidia bila kutegemea malipo yeyote. Iwe ya shukrani ama chochote.
Kwa sababu hata shukrani isingekuongezea chochote.