Sijui kwanini nimeumia hivi

Siku zote mtu "masikini" usimsaidie masikini, acha masikin asaidiwe na tajiri...

Huku mtaani wanakwambia, gari bovu haliwezi kulivuta gari jingine bovu...

Hili ndilo la kujifunza.

NB: Usiielewe vibaya hiyo masikini niliyoiwekea " "...
😋😋😋. Dahh kuna la kujifunza hapa 🤝🤝. Ingawa moyo unabeba mambo mengi.. Hili nalo niandiko kubwa.
 
Wala kisikuumize Leejay49
Hesabu ni sadaka yako kwa Bwana umetoa...

Kuna watu tunawatendea wema haturudishiwi wema kutoka kwao..Tunalipwa na watu wengine kabisa..Ambao hatujawafanyia chochote...

Wewe kunguta Mavumbi miguuni songa..Utalipwa mbele ya Safari..Kama si wewe Watoto wako watakuja kuishi kwenye huo WEMA....
 
Punguzeni kujifanya miungu watu.
Ww umeombwa hela huna unaanza kuomba na ww.

Ww sio Mungu, kama umeshindwa kumsaidia Mungu wake atamsaidia kupitia wengine, ww sema sina endelea na maisha yako.

Siwezi kukulaumu sana kwa sababu ww ni mwanamke, labda uliingiwa na roho ya huruma,. Ila ndo upate taste ya sisi tunavyojisikua tukihudumia na tunda likamegwa na mwingine, ww hapo umenyimwa credits tu umeumia hvo, hahahahaaa

Anyway pole. Jifunze kutokujiona mungu mtu, saidia unapoweza na kwa uwezo wako, ukiona unaingia hadi kukopa kisa kusaidia mtu basi fikiri mara 10 sabab inawezekana ukawa unafanya mistake kubwa sana
 
Kuna watu wana roho za tofauti sana na huyo shoga ako ana tabia za kiswahili. Ndio umeumia sana lakini overtime utakua sawa.

Cha kufanya delete namba yake akikutafuta muulize yeye nani. Mpotezee mazima hafai kabisa. Amekuona wewe ndio chuma ulete wake
 
Pole sana sana ndio maisha punguza huruma kwa watu ambao hauko karibu nao kwa kiasi cha kujimaliza
 
Shukuru una watu,yaani shida ya mwezio unamweleza Mamako ana kuhangaikia anatuma pesa.Shukuru sana.Najua unaumia kama mtu ulieachwa na mtu unayempenda au pengine unampenda.basi umeshaijua rangi yake.
 
Mbona umeenda op
 
Siku zote mtu "masikini" usimsaidie masikini, acha masikini asaidiwe na tajiri...

Huku mtaani wanakwambia, gari bovu haliwezi kulivuta gari jingine bovu...

Hili ndilo la kujifunza.

NB: Usiielewe vibaya hiyo masikini niliyoiwekea " "...
Kwakweli nimekuelewa mkuu
 
Asante kwa ushauri mkuu🙏
 
Asante mkuu, nitajirekebisha
 
Siwezi kukulaumu sana kwa sababu ww ni mwanamke, labda uliingiwa na roho ya huruma,. Ila ndo upate taste ya sisi tunavyojisikua tukihudumia na tunda likamegwa na mwingine, ww hapo umenyimwa credits tu umeumia hvo, hahahahaaa

Hahah mambo ya "cha mgema huliwa na mlevi na wakati huo huo cha mlevi huliwa na mgema"
 
Asante, walau nimeanza kujiskia vizuri nilivyoandika hapa
 
Hapatikani kawaida, ila WhatsApp yuko online naogopa kumtext
Acha kuhangaika na wajinga mkuu, zaidi utajikuta unajikosea na kuumiza moyo wako.
Niwakati sasa wa kukaa kimya na kujitenga na rafiki wa namna hiyo.
Sikuzote hua napenda kuwaambia watu kwamba kutunza urafiki ni gharama, sasa inapo tokea mmoja kati yenu haoni thamani ya mwingine basi mteme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…