Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi nimekuelewa Sana mleta madaYaani nashindwa kueleza ninavyojiskia,, sihitaji anilipe chochote wala chochote ila tu nimeumia ndomana najishangaa kwanini inakua hivi hadi nashindwa kujizuia.. Hata sielewi naumia nini yani
Pole ndo ukubwa huo mi siku hizi nimekuwa na roho mbaya baada ya kupigwa vitu vizito huko nyuma yani shida za mtu wa karibu sijui ndg au nani nani hazinigusi kabisaaa ndo ije kuwa classmate,
Tuishi humoSiku zote ishi kwa kusaidia bila kutegemea malipo yeyote. Iwe ya shukrani ama chochote.
Kwa sababu hata shukrani isingekuongezea chochote.
Achana nae mbwa huyo....afu hatoboi....yaan hatoboi😖Habari za asubuhi wanajf
Iko hivi... Nina rafiki yangu ana mtoto( naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae olevel huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.
Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia...
Nilimkuta yuko good ila mwanae alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana ela na almost kila aliyempigia simu wamemuahid tu tangu asubuhi na hakuna aliuemtumia mpaka mda huo sa1 jioni inaelekea saa2..
Kiukweli sikua na hela and i was totally broke,, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu.... Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela.. kweli mzee bila hiyana tukamshawishi akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule...
Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine( mda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba tu ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje....
Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa ( Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha.. Kwasababu kazini nilikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie,, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena..
Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa.... Kuanzia jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtuma hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini.. Screenshot kama kumi hivi na kitu na amewataja na majina kabisa...
Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito.. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia sikuileile ambayo aliniambja na mimi niende kwake kumuona,,.. Mimi ambayo nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma..
Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee😥😥
Hukutambulishwa ukaumia [emoji23]...hukulipizia kwenye vinywaji na misosi?Ndivyo wanadamu tulivyo. Mie nilialikwa kwenye mahafali ya jamaa yangu mahali, jamaa ambaye nimembeba room kwangu hakunitambulisha wkt wa utambulisho, lakini alitambulisha watu niliokaa nao meza moja na kuwashukuru kumchangia pesa ya mahafali, ingawa nami nilimchangia pakubwa. Imagine maumivu yake, na sherehe ilipoisha tukarudi room kwangu wote. Very painful. Ndio maana waswahili wanasema rafiki yako nae ana rafiki yake!
Asante mkuu 🙏🙏Hapo cha muhimu baki na ubinadamu wako kama ulivyoanza nao kwa kudhamiria kuokoa maisha ya mtoto na hatimaye ukafanikiwa.
Uzuri ulifika hadi Hospital na bill ya vipimo uliiona ukaibeba.
Ebu jaribu kuwa imara na usiitafute shukrani yake.
DUNIA DUARA
Duh, huyo alizidi sasa khaa😃😃Mimi nimekuelewa Sana mleta mada
Kuna binadamu ukisaidiwa hata kidogo hutoa shukrani hata ya mdomo just neno "asante" inafariji na inakupa moyo kwamba ametambua msaada wako Ila kwa hiki kizazi hasa hawa viumbe wa kike hawana huo moyo!
Kuna dada mmoja nlimkuta njiani mvua kubwa inanyesha nikasimamisha kigari changu(kama cha Mr Bean) nikampa lift japo alikuwa keshaanza kuloa na mvua nikamchukua mpaka mtaa anaokwenda nikamshusha lakini cha ajabu hata neno asante hakuna yaani anashuka anashika simu yake na kumpigia mtu kwamba ndo anashuka kwenye "bajaji"😀
Kisha akatokomea uchochoroni akiendelea kuongea na simu hata hakuniaga yaani nilijiskia vibaya Sana nikajilaumu kumpa lift na kuacha njia yangu kumpitisha huku anakoelekea
Mie nadhani malezi ya siku hizi ndo chanzo mtoto tangu akiwa mdogo hajafundishwa kusema samahani anapokosea na hajui kusema Asante anapopewa kitu
Inaumiza sana, sema tu ndo hivyo hatuna namnaNdivyo wanadamu tulivyo. Mie nilialikwa kwenye mahafali ya jamaa yangu mahali, jamaa ambaye nimembeba room kwangu hakunitambulisha wkt wa utambulisho, lakini alitambulisha watu niliokaa nao meza moja na kuwashukuru kumchangia pesa ya mahafali, ingawa nami nilimchangia pakubwa. Imagine maumivu yake, na sherehe ilipoisha tukarudi room kwangu wote. Very painful. Ndio maana waswahili wanasema rafiki yako nae ana rafiki yake!
Kigari kama cha Mr Ben kikawa BAJAJI.Mimi nimekuelewa Sana mleta mada
Kuna binadamu ukisaidiwa hata kidogo hutoa shukrani hata ya mdomo just neno "asante" inafariji na inakupa moyo kwamba ametambua msaada wako Ila kwa hiki kizazi hasa hawa viumbe wa kike hawana huo moyo!
Kuna dada mmoja nlimkuta njiani mvua kubwa inanyesha nikasimamisha kigari changu(kama cha Mr Bean) nikampa lift japo alikuwa keshaanza kuloa na mvua nikamchukua mpaka mtaa anaokwenda nikamshusha lakini cha ajabu hata neno asante hakuna yaani anashuka anashika simu yake na kumpigia mtu kwamba ndo anashuka kwenye "bajaji"[emoji3]
Kisha akatokomea uchochoroni akiendelea kuongea na simu hata hakuniaga yaani nilijiskia vibaya Sana nikajilaumu kumpa lift na kuacha njia yangu kumpitisha huku anakoelekea
Mie nadhani malezi ya siku hizi ndo chanzo mtoto tangu akiwa mdogo hajafundishwa kusema samahani anapokosea na hajui kusema Asante anapopewa kitu
Utafall inlove kizembe kwa huyo single mother na ndicho anachotaka kitokee na anaenda kufanikiwa maana anafikiri unamsaidia sababu unamtaka.Mkuu kwa jinsi alivyo atarudi tu,, maana hij ni mara ya pili namsaidia halafu inatokea vilevile.. Sijui hata natakiwa kufanya nini, ila ngoja nimpigie kwanza simu nitarudi