Sijui kwanini nimeumia hivi

Sijui kwanini nimeumia hivi

Yaani nashindwa kueleza ninavyojiskia,, sihitaji anilipe chochote wala chochote ila tu nimeumia ndomana najishangaa kwanini inakua hivi hadi nashindwa kujizuia.. Hata sielewi naumia nini yani
Mimi nimekuelewa Sana mleta mada
Kuna binadamu ukisaidiwa hata kidogo hutoa shukrani hata ya mdomo just neno "asante" inafariji na inakupa moyo kwamba ametambua msaada wako Ila kwa hiki kizazi hasa hawa viumbe wa kike hawana huo moyo!
Kuna dada mmoja nlimkuta njiani mvua kubwa inanyesha nikasimamisha kigari changu(kama cha Mr Bean) nikampa lift japo alikuwa keshaanza kuloa na mvua nikamchukua mpaka mtaa anaokwenda nikamshusha lakini cha ajabu hata neno asante hakuna yaani anashuka anashika simu yake na kumpigia mtu kwamba ndo anashuka kwenye "bajaji"😀
Kisha akatokomea uchochoroni akiendelea kuongea na simu hata hakuniaga yaani nilijiskia vibaya Sana nikajilaumu kumpa lift na kuacha njia yangu kumpitisha huku anakoelekea
Mie nadhani malezi ya siku hizi ndo chanzo mtoto tangu akiwa mdogo hajafundishwa kusema samahani anapokosea na hajui kusema Asante anapopewa kitu
Pole ndo ukubwa huo mi siku hizi nimekuwa na roho mbaya baada ya kupigwa vitu vizito huko nyuma yani shida za mtu wa karibu sijui ndg au nani nani hazinigusi kabisaaa ndo ije kuwa classmate,
 
Habari za asubuhi wanajf

Iko hivi... Nina rafiki yangu ana mtoto( naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae olevel huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.

Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia...
Nilimkuta yuko good ila mwanae alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana ela na almost kila aliyempigia simu wamemuahid tu tangu asubuhi na hakuna aliuemtumia mpaka mda huo sa1 jioni inaelekea saa2..

Kiukweli sikua na hela and i was totally broke,, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu.... Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela.. kweli mzee bila hiyana tukamshawishi akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule...

Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine( mda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba tu ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje....
Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa ( Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha.. Kwasababu kazini nilikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie,, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena..

Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa.... Kuanzia jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtuma hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini.. Screenshot kama kumi hivi na kitu na amewataja na majina kabisa...

Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito.. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia sikuileile ambayo aliniambja na mimi niende kwake kumuona,,.. Mimi ambayo nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma..

Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee😥😥
Achana nae mbwa huyo....afu hatoboi....yaan hatoboi😖
 
Ndivyo wanadamu tulivyo. Mie nilialikwa kwenye mahafali ya jamaa yangu mahali, jamaa ambaye nimembeba room kwangu hakunitambulisha wkt wa utambulisho, lakini alitambulisha watu niliokaa nao meza moja na kuwashukuru kumchangia pesa ya mahafali, ingawa nami nilimchangia pakubwa. Imagine maumivu yake, na sherehe ilipoisha tukarudi room kwangu wote. Very painful. Ndio maana waswahili wanasema rafiki yako nae ana rafiki yake!
Hukutambulishwa ukaumia [emoji23]...hukulipizia kwenye vinywaji na misosi?

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu wanakutafuta wakiwa na shida tu,wakisort mess zao hutawaona mpaka watokewe tena na shida.

Rafiki yako anashida ya uaminifu.Alipaswa kupokea simu yako walau kukushukuru na kukupa update.
Kuwa post hao wengine kwa elfu 5 ni kwaida tu kwa watu wasioweza kuficha mambo yao.
Wew ni daraja rafiki wengi wanapita wanakuja kulikumbuka wakati wa kurudi.Hapo mpaka akuhitaji tena Ndio atakutafuta.
 
Hapo cha muhimu baki na ubinadamu wako kama ulivyoanza nao kwa kudhamiria kuokoa maisha ya mtoto na hatimaye ukafanikiwa.

Uzuri ulifika hadi Hospital na bill ya vipimo uliiona ukaibeba.

Ebu jaribu kuwa imara na usiitafute shukrani yake.

DUNIA DUARA
Asante mkuu 🙏🙏
 
Mimi nimekuelewa Sana mleta mada
Kuna binadamu ukisaidiwa hata kidogo hutoa shukrani hata ya mdomo just neno "asante" inafariji na inakupa moyo kwamba ametambua msaada wako Ila kwa hiki kizazi hasa hawa viumbe wa kike hawana huo moyo!
Kuna dada mmoja nlimkuta njiani mvua kubwa inanyesha nikasimamisha kigari changu(kama cha Mr Bean) nikampa lift japo alikuwa keshaanza kuloa na mvua nikamchukua mpaka mtaa anaokwenda nikamshusha lakini cha ajabu hata neno asante hakuna yaani anashuka anashika simu yake na kumpigia mtu kwamba ndo anashuka kwenye "bajaji"😀
Kisha akatokomea uchochoroni akiendelea kuongea na simu hata hakuniaga yaani nilijiskia vibaya Sana nikajilaumu kumpa lift na kuacha njia yangu kumpitisha huku anakoelekea
Mie nadhani malezi ya siku hizi ndo chanzo mtoto tangu akiwa mdogo hajafundishwa kusema samahani anapokosea na hajui kusema Asante anapopewa kitu
Duh, huyo alizidi sasa khaa😃😃
 
Ndivyo wanadamu tulivyo. Mie nilialikwa kwenye mahafali ya jamaa yangu mahali, jamaa ambaye nimembeba room kwangu hakunitambulisha wkt wa utambulisho, lakini alitambulisha watu niliokaa nao meza moja na kuwashukuru kumchangia pesa ya mahafali, ingawa nami nilimchangia pakubwa. Imagine maumivu yake, na sherehe ilipoisha tukarudi room kwangu wote. Very painful. Ndio maana waswahili wanasema rafiki yako nae ana rafiki yake!
Inaumiza sana, sema tu ndo hivyo hatuna namna
 
Kwanza kabisa nikupongeze kwa kutoa msaada, ni wachache sana wanaojali matatizo ya wengine na kuyabeba kama yalivyo bila kujali yatawagharimu kiasi gani. Nadhani ulifanya hivyo kwa moyo mkunjufu kabisa, na kama ni hivyo usiumie kwa hayo yanayoendelea mshukuru Mungu hata kwa hilo. Ukishasaidia umesaidia hayo mengineyo ni wao. Kuna kipindi nilisaidia baadhi ya watu humu wengine inasemekana ni matapeli ila mimi sijali hilo kwa sababu nilitoa kama msaada na si vinginevyo.

Pili, hii tabia ya kugeuza watoto mitaji na chanzo cha kupatia pesa wanawake wengi wanayo sana, waache hii tabia sio nzuri. Kuna siku nimeshuhudia mmama akinyang'anywa mtoto na mzazi mwenzie baada ya kudanganya kuwa mtoto kazidiwa kalazwa inahitajika hela kumbe ni janja janja tupu, baba mtoto alikuwa mkoani huko akamtuma ndugu yake afuatilie na alibaini kuwa ni uongo.

Tatu hili naomba nibold ili wengi wazingatie, wanawake wengi wana tabia ya kupuuzia mambo hasa wakishasaidika jambo, hii ni tabia ipo sana kwa wanawake, wengi huona umuhimu wa kumjibu mtu pale wakiwa na shida tu vinginevyo wanakaa kimya, ishu hata ya kumjibu mtu kwa ujumbe ambao hauzidi 5 seconds to type inakuwa ngumu. Nadhani wewe umeona ni jinsi gani inaumiza.

Ni watu wenye busara tu huweza kushukuru. Huyo anafanya maigizo ndio maana kapost.
 
Mimi nimekuelewa Sana mleta mada
Kuna binadamu ukisaidiwa hata kidogo hutoa shukrani hata ya mdomo just neno "asante" inafariji na inakupa moyo kwamba ametambua msaada wako Ila kwa hiki kizazi hasa hawa viumbe wa kike hawana huo moyo!
Kuna dada mmoja nlimkuta njiani mvua kubwa inanyesha nikasimamisha kigari changu(kama cha Mr Bean) nikampa lift japo alikuwa keshaanza kuloa na mvua nikamchukua mpaka mtaa anaokwenda nikamshusha lakini cha ajabu hata neno asante hakuna yaani anashuka anashika simu yake na kumpigia mtu kwamba ndo anashuka kwenye "bajaji"[emoji3]
Kisha akatokomea uchochoroni akiendelea kuongea na simu hata hakuniaga yaani nilijiskia vibaya Sana nikajilaumu kumpa lift na kuacha njia yangu kumpitisha huku anakoelekea
Mie nadhani malezi ya siku hizi ndo chanzo mtoto tangu akiwa mdogo hajafundishwa kusema samahani anapokosea na hajui kusema Asante anapopewa kitu
Kigari kama cha Mr Ben kikawa BAJAJI.

Noma sana hii Mwaisaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwanza hongera umefanya kitu kizur kwa moyo mzuri sana, hivi ambavyo unaumia kama usingemsaidia na hali ya mtoto ikawa vinginevyo ungejikuta hatian mara nyingi zaid

Watu kama hawa wapo na kama ni hulka sio wa kubadilika kwasabab hamna sehem ya ubongo wao inaonyesha wamekosea.

Wewe sasa badilika mpotezee kabisa, ilimrad mtoto yupo sawa ndo wakat wa kumpotezea sio sim sio salam labda akikuanza lakin usimpe ukarib unaoanza wewe. Sabab moyo wako utakutuma ufanye hichi tena inapotokea kadhia alafu utaumia tena mpaka utabadili personality yako bure. Uzur watu kama hawa wakipotezewa huwa nao wanapotea maana wew ndio umemshikilia.

Umefanya kitu kizuri kumsaidia
 
Mkuu kwa jinsi alivyo atarudi tu,, maana hij ni mara ya pili namsaidia halafu inatokea vilevile.. Sijui hata natakiwa kufanya nini, ila ngoja nimpigie kwanza simu nitarudi
Utafall inlove kizembe kwa huyo single mother na ndicho anachotaka kitokee na anaenda kufanikiwa maana anafikiri unamsaidia sababu unamtaka.

Ushamsaidia unampigia wa nini? Vumilia hayo maumivu yataisha in time. Subiri yeye apige kukushukuru, unadhani hajui kuwa upo na unajiuliza kwanini hapigi? Anajua sana ila ana objective zake, Atakuvuruga huyo hutaamini. chukulia umemsaidia mtoto, achana na huyo mama yake.

Akija next time kuomba msaada mwambie bila kupepesa macho kuwa wewe huna shukrani upo kama mnyama wa mwituni ni vile mtoto hana kosa ndo maana huwa najitoa otherwise nisingekusikiliza.

NB: Pesa huna, unapoteza pesa za wazazi wako kijinga jinga,
 
Back
Top Bottom