Sijui kwanini nimeumia hivi

Yaani, Asante mkuu kwa ushauri mzuri🙏
 
Shukuru una watu,yaani shida ya mwezio unamweleza Mamako ana kuhangaikia anatuma pesa.Shukuru sana.Najua unaumia kama mtu ulieachwa na mtu unayempenda au pengine unampenda.basi umeshaijua rangi yake.
Kwakweli nashukuru Mungu kwa hilo, Bora nimeandika hapa maana najua ningemwambia mama angeumia pia na yeye
 
Kwakweli
 
Nimeumia sana mkuu, ameshindwa kunishukuru basi hata angenipigia Simu anijulishe kama wanaendelea vizuri.. Nimeumia haki ya Mungu tena🥺
Ndivyo wanadamu tulivyo. Mie nilialikwa kwenye mahafali ya jamaa yangu mahali, jamaa ambaye nimembeba room kwangu hakunitambulisha wkt wa utambulisho, lakini alitambulisha watu niliokaa nao meza moja na kuwashukuru kumchangia pesa ya mahafali, ingawa nami nilimchangia pakubwa. Imagine maumivu yake, na sherehe ilipoisha tukarudi room kwangu wote. Very painful. Ndio maana waswahili wanasema rafiki yako nae ana rafiki yake!
 
Hapo cha muhimu baki na ubinadamu wako kama ulivyoanza nao kwa kudhamiria kuokoa maisha ya mtoto na hatimaye ukafanikiwa.

Uzuri ulifika hadi Hospital na bill ya vipimo uliiona ukaibeba.

Ebu jaribu kuwa imara na usiitafute shukrani yake.

DUNIA DUARA
 
Asante kwa ushauri mkuu🙏
Pole sana kwa yaliyokukuta....ubinadamu kazi!

Ila kwa jinsi nilivyosoma maelezo yako inaelekea kuna namna umemkwaza wakati unamsaidia(aidha kwa maneno au matendo), jitafakari.

Kwa mazingira ya kawaida hawezi kumshukuru aliyetoa elfu tano akakuacha wewe wa laki tatu.
Angeacha kushukuru wote ingeeleweka kwamba ni mtu asiyekuwa na shukurani.
 
Sawa nitajotahidi kujichunguza mkuu. Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…