Sijui kwanini nimeumia hivi

Sijui kwanini nimeumia hivi

Kuna watu wana roho za tofauti sana na huyo shoga ako ana tabia za kiswahili. Ndio umeumia sana lakini overtime utakua sawa.

Cha kufanya delete namba yake akikutafuta muulize yeye nani. Mpotezee mazima hafai kabisa. Amekuona wewe ndio chuma ulete wake
Yaani, Asante mkuu kwa ushauri mzurišŸ™
 
Shukuru una watu,yaani shida ya mwezio unamweleza Mamako ana kuhangaikia anatuma pesa.Shukuru sana.Najua unaumia kama mtu ulieachwa na mtu unayempenda au pengine unampenda.basi umeshaijua rangi yake.
Kwakweli nashukuru Mungu kwa hilo, Bora nimeandika hapa maana najua ningemwambia mama angeumia pia na yeye
 
Acha kuhangaika na wajinga mkuu, zaidi utajikuta unajikosea na kuumiza moyo wako.
Niwakati sasa wa kukaa kimya na kujitenga na rafiki wa namna hiyo.
Sikuzote hua napenda kuwaambia watu kwamba kutunza urafiki ni gharama, sasa inapo tokea mmoja kati yenu haoni thamani ya mwingine basi mteme.
Kwakweli
 
Nimeumia sana mkuu, ameshindwa kunishukuru basi hata angenipigia Simu anijulishe kama wanaendelea vizuri.. Nimeumia haki ya Mungu tena🄺
Ndivyo wanadamu tulivyo. Mie nilialikwa kwenye mahafali ya jamaa yangu mahali, jamaa ambaye nimembeba room kwangu hakunitambulisha wkt wa utambulisho, lakini alitambulisha watu niliokaa nao meza moja na kuwashukuru kumchangia pesa ya mahafali, ingawa nami nilimchangia pakubwa. Imagine maumivu yake, na sherehe ilipoisha tukarudi room kwangu wote. Very painful. Ndio maana waswahili wanasema rafiki yako nae ana rafiki yake!
 
Habari za asubuhi wanajf

Iko hivi... Nina rafiki yangu ana mtoto( naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae olevel huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.

Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia...
Nilimkuta yuko good ila mwanae alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana ela na almost kila aliyempigia simu wamemuahid tu tangu asubuhi na hakuna aliuemtumia mpaka mda huo sa1 jioni inaelekea saa2..

Kiukweli sikua na hela and i was totally broke,, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu.... Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela.. kweli mzee bila hiyana tukamshawishi akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule...

Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine( mda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba tu ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje....
Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa ( Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha.. Kwasababu kazini nilikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie,, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena..

Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa.... Kuanzia jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtuma hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini.. Screenshot kama kumi hivi na kitu na amewataja na majina kabisa...

Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito.. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia sikuileile ambayo aliniambja na mimi niende kwake kumuona,,.. Mimi ambayo nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma..

Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee[emoji26][emoji26]
Hapo cha muhimu baki na ubinadamu wako kama ulivyoanza nao kwa kudhamiria kuokoa maisha ya mtoto na hatimaye ukafanikiwa.

Uzuri ulifika hadi Hospital na bill ya vipimo uliiona ukaibeba.

Ebu jaribu kuwa imara na usiitafute shukrani yake.

DUNIA DUARA
 
Asante kwa ushauri mkuušŸ™
Pole sana kwa yaliyokukuta....ubinadamu kazi!

Ila kwa jinsi nilivyosoma maelezo yako inaelekea kuna namna umemkwaza wakati unamsaidia(aidha kwa maneno au matendo), jitafakari.

Kwa mazingira ya kawaida hawezi kumshukuru aliyetoa elfu tano akakuacha wewe wa laki tatu.
Angeacha kushukuru wote ingeeleweka kwamba ni mtu asiyekuwa na shukurani.
 
Pole sana kwa yaliyokukuta....ubinadamu kazi!

Ila kwa jinsi nilivyosoma maelezo yako inaelekea kuna namna umemkwaza wakati unamsaidia(aidha kwa maneno au matendo), jitafakari.

Kwa mazingira ya kawaida hawezi kumshukuru aliyetoa elfu tano akakuacha wewe wa laki tatu.
Angeacha kushukuru wote ingeeleweka kwamba ni mtu asiyekuwa na shukurani.
Sawa nitajotahidi kujichunguza mkuu. Asante
 
Back
Top Bottom