Sijui kwanini nimeumia hivi

Sijui kwanini nimeumia hivi

Kuna watu wanakutafuta wakiwa na shida tu,wakisort mess zao hutawaona mpaka watokewe tena na shida.

Rafiki yako anashida ya uaminifu.Alipaswa kupokea simu yako walau kukushukuru na kukupa update.
Kuwa post hao wengine kwa elfu 5 ni kwaida tu kwa watu wasioweza kuficha mambo yao.
Wew ni daraja rafiki wengi wanapita wanakuja kulikumbuka wakati wa kurudi.Hapo mpaka akuhitaji tena Ndio atakutafuta.
Ila nimeumia mkuu.. Hajanipigia hadi saizi bado
 
Wewe nae ukome bhn, haha
Ukishaskia mtu ni Single mother, kaa nae mbali sana. Hao hawanaga akili ndo maana wameachiwa watoto walee wenyewe. Ni wajinga kupita maelezo, unakuta ni Ego zao ndo zilifanya wakatoka kwa wanaume ili wawaonyeshe kama wanaweza kulea mtoto peke yao na kumbe hawawezi. Take your lessons and go
 
Kwanza kabisa nikupongeze kwa kutoa msaada, ni wachache sana wanaojali matatizo ya wengine na kuyabeba kama yalivyo bila kujali yatawagharimu kiasi gani. Nadhani ulifanya hivyo kwa moyo mkunjufu kabisa, na kama ni hivyo usiumie kwa hayo yanayoendelea mshukuru Mungu hata kwa hilo. Ukishasaidia umesaidia hayo mengineyo ni wao. Kuna kipindi nilisaidia baadhi ya watu humu wengine inasemekana ni matapeli ila mimi sijali hilo kwa sababu nilitoa kama msaada na si vinginevyo.

Pili, hii tabia ya kugeuza watoto mitaji na chanzo cha kupatia pesa wanawake wengi wanayo sana, waache hii tabia sio nzuri. Kuna siku nimeshuhudia mmama akinyang'anywa mtoto na mzazi mwenzie baada ya kudanganya kuwa mtoto kazidiwa kalazwa inahitajika hela kumbe ni janja janja tupu, baba mtoto alikuwa mkoani huko akamtuma ndugu yake afuatilie na alibaini kuwa ni uongo.

Tatu hili naomba nibold ili wengi wazingatie, wanawake wengi wana tabia ya kupuuzia mambo hasa wakishasaidika jambo, hii ni tabia ipo sana kwa wanawake, wengi huona umuhimu wa kumjibu mtu pale wakiwa na shida tu vinginevyo wanakaa kimya, ishu hata ya kumjibu mtu kwa ujumbe ambao hauzidi 5 seconds to type inakuwa ngumu. Nadhani wewe umeona ni jinsi gani inaumiza.

Ni watu wenye busara tu huweza kushukuru. Huyo anafanya maigizo ndio maana kapost.
Umeongea ukweli wote mkuu.. Barikiwa sana
 
Kwanza hongera umefanya kitu kizur kwa moyo mzuri sana, hivi ambavyo unaumia kama usingemsaidia na hali ya mtoto ikawa vinginevyo ungejikuta hatian mara nyingi zaid

Watu kama hawa wapo na kama ni hulka sio wa kubadilika kwasabab hamna sehem ya ubongo wao inaonyesha wamekosea.

Wewe sasa badilika mpotezee kabisa, ilimrad mtoto yupo sawa ndo wakat wa kumpotezea sio sim sio salam labda akikuanza lakin usimpe ukarib unaoanza wewe. Sabab moyo wako utakutuma ufanye hichi tena inapotokea kadhia alafu utaumia tena mpaka utabadili personality yako bure. Uzur watu kama hawa wakipotezewa huwa nao wanapotea maana wew ndio umemshikilia.

Umefanya kitu kizuri kumsaidia
Kwakweli
 
Utafall inlove kizembe kwa huyo single mother na ndicho anachotaka kitokee na anaenda kufanikiwa maana anafikiri unamsaidia sababu unamtaka.

Ushamsaidia unampigia wa nini? Vumilia hayo maumivu yataisha in time. Subiri yeye apige kukushukuru, unadhani hajui kuwa upo na unajiuliza kwanini hapigi? Anajua sana ila ana objective zake, Atakuvuruga huyo hutaamini. chukulia umemsaidia mtoto, achana na huyo mama yake.

Akija next time kuomba msaada mwambie bila kupepesa macho kuwa wewe huna shukrani upo kama mnyama wa mwituni ni vile mtoto hana kosa ndo maana huwa najitoa otherwise nisingekusikiliza.

NB: Pesa huna, unapoteza pesa za wazazi wako kijinga jinga,
Me ni mwanamke mkuu.. Ila umenifunza kitu, Asante kwa ushauri 🙏🙏
 
Wewe nae ukome bhn, haha
Ukishaskia mtu ni Single mother, kaa nae mbali sana. Hao hawanaga akili ndo maana wameachiwa watoto walee wenyewe. Ni wajinga kupita maelezo, unakuta ni Ego zao ndo zilifanya wakatoka kwa wanaume ili wawaonyeshe kama wanaweza kulea mtoto peke yao na kumbe hawawezi. Take your lessons and go
Asante kwa ushauri mzuri mkuu🙏
 
Ww ndo hujaelewa.

Kaombwa msaada na hakua na uwezo wa kutoa.

Kakomaa kujiombeleza na yeye kwa niaba ya rafiki yake.

Anyway huwezi elewa hata nikirudia.

Ila epuka kujifanya mungu mtu usaidie kila anaekuomba, utafirisika, utapata heartbreaks zisizo na ulazima
Mimi nakuelewa, ila Shida inakuja kwa kuwa msaada ulikuwa ni kwa mgonjwa na yeye alimuona mgonjwa huyo hivyo ikapelekea moyo kumsukuma kuomba hela kwa wazazi ( watu wake wa ndani) ili asaidie eneo lile, Ukileta Neno Mungu mtu kwenye incident kama hii inakuwa hai work out.
 
Habari za asubuhi wana JF,

Iko hivi, nina rafiki yangu ana mtoto (naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae O level huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.

Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia.

Nilimkuta yuko good ila mwanaye alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana hela na almost kila aliyempigia simu wamemuahidi tu tangu asubuhi na hakuna aliyemtumia mpaka muda huo sa 1 jioni inaelekea saa 2.

Kiukweli sikua na hela and i was totally broke, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu. Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela, kweli mzee bila hiyana tukamshawishi akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule.

Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine (muda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba tu ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje.

Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa (Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki 2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha. Kwasababu kazini nilikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena.

Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi Peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa. Kuanzia jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtuma hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini. Screenshot kama kumi hivi na kitu na amewataja na majina kabisa...

Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia siku ileile ambayo aliniambja na mimi niende kwake kumuona.

Mimi ambayo nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma.

Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee😥😥
tukiwaambia mtu anayebeba mimba akiwa bado hajaolewa ana kasoro zake muwe mnaelewa, nyie mnawaita single mother
amewafanyia dharau wazazi wake , ndugu zake wa tumbo moja. amekuja amevurugana na aliyemzalisha, wewe ndo atakupa heshima.
Pole sana
 
Acha kuumia hivyo Asante yako inakuja.

Lakini nimeumia Sana kuona unaumia kidoti wangu.
 
Mimi nakuelewa, ila Shida inakuja kwa kuwa msaada ulikuwa ni kwa mgonjwa na yeye alimuona mgonjwa huyo hivyo ikapelekea moyo kumsukuma kuomba hela kwa wazazi ( watu wake wa ndani) ili asaidie eneo lile, Ukileta Neno Mungu mtu kwenye incident kama hii inakuwa hai work out.
Asante mkuu, umenielewa sana.. kwa hali aliyokua nayo haikua rahisi kusema tu sina ukizingatia unao watu walau wanaweza kukuunga mkono kwenye kutoa msaada.. Angekua ameniambia kwa simu kwa jinsi hali yangu ilivyokua ningemwambia sina
 
Back
Top Bottom