Sijui kwanini nimeumia hivi

Sijui kwanini nimeumia hivi

Mkuu kwa jinsi alivyo atarudi tu,, maana hij ni mara ya pili namsaidia halafu inatokea vilevile.. Sijui hata natakiwa kufanya nini, ila ngoja nimpigie kwanza simu nitarudi
kaa mbali nae... anakutumia kama daraja... au tuseme toilet paper 😭😭😭 shida ikiisha haoni thamani yako... mtu kama huyo hupaswi kabisa kumkaribisha nyumbani kwako.

hao ni aina ya watu ambao wakikuona na kitu kipya wana kuuliza umekinunua bei gani.... 🤣🤣🤣

watu kama hao hawana msaada na wewe siku ukikwama.....! na akifanikiwa yeye lazima afanye jambo ili ujue kuwa nae amejipata... na mara nyingi huwa wanafanya mambo ya kijinga ili uumie utambue kuwa na yeye ana kipato kukuzidi😭😭😭😭​
 
Futa mawasiliano pambana na maisha yako; hiyo hela uliyoitoa chukulia kama ni ada uliyolipia ili kujua tabia halisi za binadamu baada ya kufanikiwa.
 
Hapana, bora ukaushe tuu. Kama hakuona umuhimu wa kukushukuru bc hakuna umuhimu wa ww kumpigia simu ili ety moyo wako utapata ahueni.

Hili chukulia kama funzo tuu, na kuumia ndio funzo lenyewe mana usipoumia hapo bado hujajifunza.
Asante umenielewesha vizuri
 
Kiubinadamu inaumiza ila kuna uzi upo humu unahusu watu wema kwa nini Mungu huwachukua mapema kuliko hata muda ambao jamii/familia inavyowahitaji. Fact ambayo imeungwa mkono na wengi ni kwamba sifa, utukufu na shukrani wanazopata kutokana na huo wema unabeba sifa na utukufu wa Mungu. Hivyo Mungu anabeba hicho kiumbe chenu mnachokipa utukufu kuliko yeye ili awaonyeshe kuwa YEYE ni MKUU kuliko huyo.
Unapaswa ushukuru kwa alichokifanya ili wewe ubaki salama mikononi MWAKE.
Amen, somo zuri sana hili
 
Pole sana sister ndo binadamu tulivyo ila mwenzio anachukulia ni kawaida tu...

Fanya kama umetoa sadaka kwa watu wasiojiweza ila siku c nyingi rafiki yako atakuja kukushukuru na atafika mpaka kwa mama. labda anaandaa siku maalumu kwa ajiri ya hilo.
 
rafiki yangu usiumie hapo huja msaidia huyo rafiki yako... aliekuwa na shida ni huyo malaika...! ambae kupitia wewe amepata kupona...!

ambae nina amini ipo siku isiyo na jina atakuja kukushukuru... iwe kwa kutamka au kwa vitendo ila shukrani ya kumsaidia huyo mtoto utaipata.

na inawezekana muda sio mrefu ukapanda cheo au ukapata ajira nzuri zaidi ya hiyo unayo fanya lolote jema kubwa litakalo kutokea ujue ni sauti ya yule mtoto ulieokoa maisha yake.

wala usinung'unike... mtu akikufanya mjinga wewe mpuuzie...!​
Na ikawe hivyo Amen 🤲🤲🙏
 
Yeah ni kweli, but sometimes kushukuru kunamfanya aliyekusaidia ajiskie vizuri
Sure.. Pia nimewaza kuwa au pengine ulikuwa na mahusiano naye ya kimapenzi hujataka kueleza hapa, na hiyo imepelekea kutokukushuru na kuona kama hata ulichofanya bado hakikufikia wajibu wako kama mpenzi wake. Yaani kwa maana nyingine akaona kuwa bado hujawajibika, na hivyo ulivyokuwa bize siku nzima akaona kama ndo umewatelekeza.
Wanawake sometimes wana akili za kijinga sana mkishachanganya na masuala ya kimahusiano hapo kati.
 
kaa mbali nae... anakutumia kama daraja... au tuseme toilet paper 😭😭😭 shida ikiisha haoni thamani yako... mtu kama huyo hupaswi kabisa kumkaribisha nyumbani kwako.

hao ni aina ya watu ambao wakikuona na kitu kipya wana kuuliza umekinunua bei gani.... 🤣🤣🤣

watu kama hao hawana msaada na wewe siku ukikwama.....! na akifanikiwa yeye lazima afanye jambo ili ujue kuwa nae amejipata... na mara nyingi huwa wanafanya mambo ya kijinga ili uumie utambue kuwa na yeye ana kipato kukuzidi😭😭😭😭​
Duuh 🤔🤔.. wacha nitulie tu basi
 
Sure.. Pia nimewaza kuwa au pengine ulikuwa na mahusiano naye ya kimapenzi hujataka kueleza hapa, na hiyo imepelekea kutokukushuru na kuona kama hata ulichofanya bado hakikufikia wajibu wako kama mpenzi wake. Yaani kwa maana nyingine akaona kuwa bado hujawajibika, na hivyo ulivyokuwa bize siku nzima akaona kama ndo umewatelekeza.
Wanawake sometimes wana akili za kijinga sana mkishachanganya na masuala ya kimahusiano hapo kati.
Me ni mwanamke pia mkuu,
 
Habari za asubuhi wana JF,

Iko hivi, nina rafiki yangu ana mtoto (naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae O level huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.

Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia.

Nilimkuta yuko good ila mwanaye alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana hela na almost kila aliyempigia simu wamemuahidi tu tangu asubuhi na hakuna aliyemtumia mpaka muda huo sa 1 jioni inaelekea saa 2.

Kiukweli sikua na hela and i was totally broke, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu. Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela, kweli tukamshawishi mzee bila hiyana akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule.

Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine (muda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje.

Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa (Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki 2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha. Kwasababu kazini walikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena.

Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi Peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa. Jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtumia hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini. Screenshot kama kumi hivi na kitu na amewataja na majina kabisa...

Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia siku ileile ambayo aliniambja na mimi niende kwake kumuona.

Mimi ambaye nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma.

Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee😥😥
Daah mpaka na Mimi nimeumia aisee.
 
Ni mngoni, mmatengo, myao maana najua hawezi kuwa mnyasa wanyasa tumenyooka sana
 
Back
Top Bottom