Sijui laki moja yangu imeenda wapi?

Sijui laki moja yangu imeenda wapi?

Tumia miezi 2 au 3 kuweka stock ya miezi 6/mwaka
Lipa kodi miezi 6/mwaka
Baada ya kufanya hayo yote; pesa yoyote inayokuja peleka kwenye mambo ya msingi
 
Mkuu kasome kitabu kinaitwa THE RICHEST MAN IN BABYLON kuna mtu alikipost kule jf store kwenye mada inayoitwa vitabu viliwahi kubadili maisha yangu itakusaidia saaaaana!
 
Pole sana mimi hiyo hali huwa inanitokea maranyingitu. Laki 5 unajenga vizuri sana ni hela nyingi sana hiyo. Mimi nimejenga nyumba yangu nikiwa na tak home ya laki7 nyumba ina gharama ya 4p mil.nimeijenga kwa 5 yrs. Nlikopa 9mil nikajenga boma likaisha nikawa nimebakiwa na 2.5mil hivi. Nikapata tena 2.5mil zingine kwa ajili ya likizo yangu nikaziunganisha nikatumia kupaulia nikawa nimamaliza nyumba sasa wife akaanza kusumbua hataki kukaa ya kupanga tena naye ni mtumishi nikamwambia kavute 3mil kwa ajili ya madirisha na milango. Dakika 0 tukawa tumemaliza nikaweka na jamvi tukahamia bila lipu maisha yakaendelea. Nlijenga ndani ya miezi 6 ndo ikafika hivo. Nimekuwa nafanya finishing mdogomdogo mpaka sasa nimebakiza kuweka alminium tu
 
Ndo wenye msemo huo..[emoji28][emoji28] nimetaja hii mikoa nimekumbuka nyanyantole [emoji28][emoji28]jamani haya majina haya[emoji28][emoji28]
Kila kanda kuna baadhi ya code zinakua unique kwa eneo husika, kwa kanda yetu huku utakutana na:-
Jojo-buble gum/big G
Ishii-tunavyoshangaa
Kuniga-kabari/roba
Nswalu-mboga
Nsansa-mboga
Nzengo-umoja flani hv n.k.
 
Hivi watu wanaotumia neno "kuhemea".....

wakimaanisha kununua matumizi yao....

huwa n watu wa kabila gani? hawa wahemeaji...
Mkuu hawa ni watu wa mikoa ya Rukwa, Katavi, Kigoma, mikoa ya Lake zone na Kilimanjaro kidogo
 
Zingatia usemi ya mali bila daftari...ukiandika unachotumia wala hili neno 'unashangaa' halitakuwepo
Andika budget ya mwezi mzima,toa kiasi cha hayo matumizi....pesa iliyobaki iache huko bank

Majibu yote ya mishangao yako yatakuwepo katika maandishi
flulanga hakikisha unafata ushauri huu. Hakuna mwizi wala mchawi kwenye pesa zako bali ni kukosa rekodi ya matumizi. Ukifata hivi utasave kiasi cha kumsaidia wife kuanza mradi wa kuleta chochote ndani.
Nimependa ulivo real na nimeguswa na tatizo lako. I bet mkeo ni faraja kwako, Mungu awazidishie.
 
Amina mkuuuu ubarikiwe sana
 
Pole sana mimi hiyo hali huwa inanitokea maranyingitu. Laki 5 unajenga vizuri sana ni hela nyingi sana hiyo. Mimi nimejenga nyumba yangu nikiwa na tak home ya laki7 nyumba ina gharama ya 4p mil.nimeijenga kwa 5 yrs. Nlikopa 9mil nikajenga boma likaisha nikawa nimebakiwa na 2.5mil hivi. Nikapata tena 2.5mil zingine kwa ajili ya likizo yangu nikaziunganisha nikatumia kupaulia nikawa nimamaliza nyumba sasa wife akaanza kusumbua hataki kukaa ya kupanga tena naye ni mtumishi nikamwambia kavute 3mil kwa ajili ya madirisha na milango. Dakika 0 tukawa tumemaliza nikaweka na jamvi tukahamia bila lipu maisha yakaendelea. Nlijenga ndani ya miezi 6 ndo ikafika hivo. Nimekuwa nafanya finishing mdogomdogo mpaka sasa nimebakiza kuweka alminium tu
Duh mkuu hongera sana, hata mimi pia najipa moyo naweza kujenga kwamshahara huu huu
 
Miaka yetu tulikuwa hatuombi ushauri mambo ya kijinga namna hii. Hili ni suala la hovyo kutaka wanaume tujadili. Mkajadiliane wenyewe wanafunzi wa certificate.
Ulitaka nije niombe ushauri waaje?
 
Ikiwa unatebea na fedha hizo zote ambazo ulidhani ni akiba ya koni dhahiri haukuwa serious na unachokifanya.
Ulipaswa kutenga pesa za matumizi pembembeni then hiyo akiba yako ikawekwa kwenye sehemu salama au kwenye account maalum kwa muda utakaojipangia .
 
Walioweka ule usemi wa mali bila daftari huisha bila habari walikuwa wanamaanisha situations kama hizi

Hiyo laki ni wewe umeitumia,hukumbuki tu

Kwanini unawithdraw pesa yote?

Kimsingi ili kujua kila cent imetumikaje ni vizuri ukawa unatumia kwa kuandika ama nzuri zaidi ni kupanga budget ambayo itaonesha zile expenditures(muhimu) zinazotarajiwa kutokea ndani ya mwezi mzima
Hii itakusaidia kuweka records na kuwa na plan nzuri

Theoritically,una take home ya 540,000/=
Sijui bei ya vyakula lakini naassume michele 20 kilos labda ni 50,000+unga 10 kilos 20,000 ambavyo nafikiri hamuwezi kumaliza hivi vyote ndani ya mwezi
Bill ya maji mwezi 20,000
Umeme 50,000
Usafiri na other expenses(emergencies) tenga 150K

Hapo utabakiwa na 250,000
We Ni mwasibu!!!mkuu nimependa umefikirisha....Ila nikuongezee Kama unafamilia kata bima ya mtoto na mama ake.
 
We Ni mwasibu!!!mkuu nimependa umefikirisha....Ila nikuongezee Kama unafamilia kata bima ya mtoto na mama ake.

Wala sio mhasibu,nilichoandika yoyote anaweza kuandika....kipo wazi
 
Back
Top Bottom