Mkuu nashindwa nikupe pole au vipi kwamaana tatizo ulilopo limesababishwa na tamaa.Ila pia siwezi kukulaumu saana kwavile hata mimi nilishawahi kuwa katika hali kama hiyo ingawa ushapita muda kidogo.
Wahenga walisema ukiwa na vitu viwili unavyovipenda,ni vizuri ukabaki na chaguo la pili.Walisema hivi wakiwa na maana ya kwamba,kama ungekuwa kweli umelipenda chaguo la kwanza hakika husingehadaika na chaguo la pili (tafsiri yake ni kuwa macho au moyo wako umependezwa sana na chaguo la pili kuliko la kwanza)
But mkuu kwa situation yako ni kwamba umezungumzia "mke".Kama ni kweli unatarajia kuoa mmoja kati ya hao wawili basi ni heri ukachanganua tabia zao na mambo yao kwa ujumla.
Ila kuwa makini na fanya maamuzi haraka,maana MTAKA YOTE KWA PUPA HUKOSA YOTE MKUU.
"Analyse"