Sijui nini kimetokea sasa hivi wasanii wamekazana kuimba kuhusu ngono

Ndo tunarudi uko uko hiyo ni demand ya mashabiki.
 
Hazipewi nafasi kwasababu sio demand ya mashabiki.
 
Mkuu kcamp ni kweli soko la muziki linategemea concept ya demand and supply, lkn kiuhalisia demand ambayo ndiyo hadhira inategemea sana suppliers ambao ndiyo wasanii hapa namaanisha huwezi ku demand kitu ambacho hakipo sokoni, so wasanii wana uwezo mkubwa wa kubadilisha akili ya hadhira hasa wasanii wakubwa mana hawa wadogo wanaangalia nn wakubwa wanafanya, kwa mfano kuna mziki umeibuka kwa ss mziki wa singeli japo ulikuwepo kwa mda kdg lkn ulikuwa unaonekana km mziki wa kihuni usio na maadili na ni wa uswahilini, lkn ghafla umeanza kupewa credibility baada ya wasanii wakubwa kuanza kuuimba, hii inaonesha nguvu ya ushawishi waliyonayo wasanii wakubwa na pengine niseme kitu kimoja, ni kwamba huu mziki wa matusi ya wazi wazi muasisi ni Diamond pamoja na kundi lake la WCB japo ni kweli matusi yalikuwepo huko nyuma lakini c kwa kiwango cha ss, huko nyuma ilikuwa nyimbo ikiwa na tusi hata kwny redio stesheni ulikuwa unafinywa kimtindo lkn kwa ss imeshaonekana ni kitu cha kawaida maana utafinya nyimbo ngp ilihali asilimia kubwa ya nyimbo za ss zinafanana, mm mwenyewe ni mpnz wa nyimbo za Mondi na kundi zima la WCB na huu ndio ukweli wenyewe kwmb kupitia wao wasanii wengine wakaona hii ndio direction na mpk ss tunapoelekea ni kubaya zaidi km hii perception ya wasanii wanaimba kulingana na uhitaji itaendelea kugonga ktk vichwa vya wasanii.

Recommendation

Wasanii wakubwa wanapaswa kujuwa wajibu wao kwmb mbali na kuburudisha pia waangalie namna ya kutoharibu maadili yaliyopo katika jamii kwn wao wanaweza kuamua ni mziki gn wa kuimba na hadhira itasikiliza na kupenda itake isitake
 
Nyimbo za matusi zimeanza kuimba kitambo Sana dully Sykes aliimba wimbo unaitwa utamu ndani ya ule una matusi Sana sio kweli mwanzilishi ni diamond
 
Nyimbo za matusi zimeanza kuimba kitambo Sana dully Sykes aliimba wimbo unaitwa utamu ndani ya ule una matusi Sana sio kweli mwanzilishi ni diamond
[emoji116][emoji116] huko kote nimegusa mzee icho kipengele nilisahau kuweka nimeshakiweka so rejea tena utanielewa mkuu
 

Mkuu kwa taarifa yako kama hujui ni kwamba shetani yuko kazini kuvuna wafuasi, mkakati uliopo ni kukifanya hiki kizazi kiwaze masuala ya mapenzi na ngono mda wote Ndio maana hata watunzi wa nyimbo wamejikita sana kwenye nyimbo za mapenzi na kuhamasisha ngono pasipo wao kujijua..ushahidi wa kwamba ibilisi yuko kazini na ameamua kunadili fikra za vijana kabisa basi itokee msanii katoa nyimbo ya kuhamasisha watu kufanya kazi na kuepukana na anasa..hiyo nyimbo haitauza na haitapata ushabiki lakini akiachia ngoma watu wanacheza uchi na kuimba ngono ngono tu watu wote watasifia na atapata viewers mamilioni kwa wiki moja tu. Huo ni mkakatati wa shetani katika ulimwengu wa roho ili kuwaharibu vijana wasiwe hata na future ya maisha yao na nchi yao bali wawe wanawaza tu mapenzi na sio maendeleo. Mifano ipo mingi sna kwa haya tunayo yaona katika kizazi chetu kwa sasa. Angalia hata news nyingi humu JF ni kuhusu mapenzi tu na mambo ya kingono ngono tu.
 
Kiranga amejibu vyema, wanacheza na mahitaji yetu.
Akili za kiafrika zimejaa ngono 90%
JK alisema bungeni...ukitaka kula liwa kidogo.
Unajua kwanini wabunge wote walicheka?
Sababu walitafsiri KINGONONGONO
Raia ndiyo wana-shape aina ya mziki wanaouhitaji au wanamuziki ndiyo wana-shape raia wapende aina gani ya mziki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio nyimbo tu hata Jf ya zamani sio sawa na ya sikuhizi ngono inazungumzwa hadharani
 
Yes mahitaji ya dunia na wakati
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soko la nyimbo za ngono linalipa zaidi bongo ,wabongo wengi wanazipenda hizo nyimbo kuliko nyingine na kwa sababu wasanii wako kibiashara inabidi watoe nyimbo za ngono kwa wingi zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kwel wao ndio masupliers mkuu,lakin ukiona mzabuni hadi anabadlisha msosi ujue kashaona anarud sana na chakula nyumban

Kizaz cha sasa mkuu kimeshapinda mda tu... ukizingatia utandawazi unavyokua kwa kasi..yani hata usipoimba mitaro sijui,bado wakipita upande wa pili wataikuta na wataifukua.

Kwaiyo kitachotokea ni nn incase wasanii wataondoa matus,sio kwamba kizaz kitakua salama,Wala kitakua kimepinda vizur tu..sema sisi tutajisifu wasanii wana adabu sana lakin ukwel mtaani utakua tofaut... hivyo tutakua tunajidanganya wenyewe

Ni kama saizi tunaambiwa uchumi unakua na kiwango cha umaskin kimepungua which is not real.

Mytake..acha tu twende na haya mabadiliko ,itafka mda demand itachange na wao watakuja na kitu kipya japo dunia inapoenda hali ndio itazid kua mbaya..

Wazo lako zuri mkuu lakin biashara inakataa sasa [emoji2] ,tutafika tu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Mimi sijui kwa nini hali kama hii tumeiruhusu yaani ni upumbavu juu ya upumbavu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Artists waimbe wanachotaka fine, kinachotakiwa mamlaka husika waweke mfumo wa kugrade nyimbo zenye matusi (explicit content/parental advisory) na za kawaida za radio. Artists waruhusiwe kutoa version mbili za ngoma moja (ya matusi na ya kawaida).

Za matusi zipigwe club cause watoto na wazee hawaendi kule za kawaida zipigwe kwenye redio. Shida mamlaka husika wanachojua ni kufungia tu.

Mfano ile "Nyegezi" badala ya kufungiwa, wangeruhusiwa kutoa radio version, wanaondoa tu neno "Nyegezi" wanaweka lingine tayari maisha yanaendelea!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…