Sijui wale watoto walioungana watakufa pamoja?

Mfano wale wa Iringa kuna vitu wana share na mara nyingi mmoja akiugua na mwingine pia hivyo ikitokea mmoja kafa maanake wote watakufa......ni hayo tu mkuu
 
Mungu ana maksudi yake anajua kwa nini amefanya hivyo
 
Mfano wale wa Iringa kuna vitu wana share na mara nyingi mmoja akiugua na mwingine pia hivyo ikitokea mmoja kafa maanake wote watakufa......ni hayo tu mkuu
Ndo hao nawaongelea
 
Bora kujiwazia kuliko kuwawazia wengine
Kwani kufa dada yangu ni jambo baya......au usipoliwaza haliwezi kutokea? We hujawahi kuwaza hata siku moja kuwa utakufa??
 
Kila jambo amelifanya kwa makadirio yake, Mungu ni mjuvi wa yote
 
Kama wasemavyo wengi kuwa muumba ndiyo anajua maisha ya hawa Viumbe vyake,
Lakini c vibaya kujiuliza na wala c dhambi kujua kwa vile kila kiumbe kitaonja Mauti
Kwa akili yangu ndogo naona kuwa wale pale asilimia kubwa wanna mwili mmoja
Nina maana viungo vingi vya ndani ya mwili ni vimoja,
Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kuwa infection yeyote ikawaathiri kwa pamoja.
Kwa mfano uko uwezekano wa kuwa mfumo wa damu ni mmoja au ni unaotegemeana,
Kwahiyo ni rahisi ugonjwa kutoka step moja na kushambulia upande mungine.
Kwakweli ni vitu vigumu Sana kufikirika Nadhani ata exparts
Wanaumiza vichwa lakini
all in all God knows what will happen.
Nawaombea maisha marefu
Watoto Hawa walioungana
 
Ndo hao nawaongelea
Kama unawaongelea hao vitu vingi sana vya ndani ya mwili wana share........jarib kuwatazama kwe tv siku moja utawaona mmoja akiwa anaongelea kitu fulani na mwingine unamuona anaongea kwa mfumo ule ule......hao wataenda siku moja mkuu
 
Niliwahi kuwaza sana kimoyo moyo hiki kitu.
 
Kila mmoja ana roho yake moyo wake wanashea kifua akifa mmoja madaktari watawatenginisha na huyu aliyebaki ataishi ingawa ni ngumu kufikiria hiyo ni mipango ya mungu yeye anajua kitakacho kuwapo
 
Watoto walioungana kwa kawaida wote huwa wanazaliwa ni wa jinsi moja. Mmoja akifariki moyo wake husimama kupiga na mishipa yake ya damu inapanuka na kama muunganisho unahusisha mishipa mikubwa ya damu, basi damu ya yule aliye hai itaaingia kwa marehemu na hatimaye yule sliye hai naye atakufa kwa kupoteza damu (bleeding into a dead body). Kama muunganiko wao wa mishipa ya damu siyo mikubwa basi huyu mzima hatakufa kwa kupoteza damu bali marehemu ataanza kuoza na kumwabukiza uozo huyo mwingine na kumuua. Kwa kifupi pacha moja akifa na yule aliyebaki ni lazima afe ndani ya muda mfupi tu au baada ya siku chache tu. Nawasilisha.
 
Kama unawaongelea hao vitu vingi sana vya ndani ya mwili wana share........jarib kuwatazama kwe tv siku moja utawaona mmoja akiwa anaongelea kitu fulani na mwingine unamuona anaongea kwa mfumo ule ule......hao wataenda siku moja mkuu
Aise mungu mkubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…