Sijutii kuifahamu JamiiForums hasa Love Connect

Sijutii kuifahamu JamiiForums hasa Love Connect

Heloo

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
4,391
Reaction score
3,404
Kwa heshima ya kipekee na ndani ya moyo wangu,

Kwa mara nyingine Leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa waanzilishi wa JF. Kwangu mimi imenitendea mambo mengi kupitia watu wake.

Mbali na kufahamiana na watu wengi ambao tumejenga undugu na ujamaa wa kufa na kupona.

Pia JF imeniwezesha kukutana na my Soul mate.

Haikuwa kazi rahisi but nitakuwa mchoyo wa fadhila nisiposhukuru wote waliopata wazo la kuanzisha Love Connect.( Mkombozi wa mioyo iliyovunjika)

Kwani kupitia JF imenifanya kurudisha furaha yangu iliyopotea.

Mimi nilikuwa mmoja wa watu niliokuwa siamini watu kujenga uhusiano na ukadumu kwa njia ya mitandao.Lakini mimi nashuhudia kwamba inawezekana na tena mkaishi vizuri.

Nilichojifunza ni uvumilivu na kuwa na moyo wa subira, majaribu yapo lakini ukiamini na kumuomba Mungu hata humu inawezekana ( I have met my eclipse of my heart)

Niliwai kuwa na mchumba wa kukutana uraiani alinitenda mabaya sana pamoja na kumvumilia mengi.

Zikiwa zimebaki siku chache aje kutoa posa kwetu, bila kujua nini hufanya, niliamua kumsuprise badala ya kumsuprise, surprise ilinikuta mimi baada ya kumkuta amelala kitandani na mwanamke kwenye shuka nililofua mimi Jana yake na wakala chakula nilichopika na baada ya kuchunguza haikuwa Mara 1.
Ilinivunja moyo na kunikatisha tamaa sana.( Wadada huwa tunaumia sana hasa muda unaopotea)

Sasa JF kukutanishwa na MTU huyu ambaye amenisahaulisha machungu mengi mengi.Nina kila sababu ya kushukuru kwani na Mimi nimejiona wa Thamani.

Ewe mdada au mama uliyeumizwa usikate tamaa.Popote waweza pata mwenza na kufungua ukurasa mpya.Hakuna aliyezaliwa asononeke.

Fight, search, simamia unaloliamini mtu asikukatishe tamaa better late than never.
 
Hongera
Ungetutajia mwenza wako

Ingependeza zaidi..
Haaa haaa
Anajulikana mbona
Wewe tu unashindwa kuconnect ..
Mpaka jina lingine anaitwa kama langu .Kaongeza tu.Mr.
Si unajuaaa
But kumtaja moja kwa moja hapana
Najua madhara yake
 
Back
Top Bottom