Jasusi,
Mbona
na wewe unaharibu sasa? Sokoine hakuwahi kujiuzulu kwa sababu yoyote. Alichaguliwa
April 12, 1977 kuwa Prime Minister.
Leo tuko kwenye bunge la 10, hili la Anne Makinda. Hivyo, Sokoine wakati anachaguliwa alikuwa ni mbunge katika bunge la 03 ambalo mwisho wake ulikuwa ni uchaguzi wa mwaka 1980.
Akakaa na post hiyo hadi bunge lilipovunjwa mwaka 1980 na nchi ikaingia kwenye uchaguzi mkuu wa serikali mpya yaani kati ya Nyerere na na mpinzani wake wa siku zote aliyeitwa
kivuli.
Uchaguzi mkuu ukafanyika Jumapili, October 26, 1980, na Nyerere akakishinda kivuli kwa kura nyingi tena zaidi ya 90% ndipo akawa na kazi ya kuunda Baraza jipya la mawaziri kutokana na bunge jipya la 04.
Baada ya Nyerere kuapishwa, kazi ya kwanza ya kuunda cabinet ikawa ni kuteua Prime Minister kama ilivyotakiwa. Hivyo, November 07, 1980, siku 10 baada ya uchaguzi akamteua Cleopa Msuya kuwa Prime Minister.
Hivyo, huwezi kusema kuwa Sokoine alijiuzulu kwa sababu yoyote. Hapana. Muda wa bunge lake la tatu uliisha ikaja zamu ya bunge la nne.
Hata Mkapa angeweza kufanya hivyo yaani kutoendelea na Sumaye ile mwaka 2000, na tusingesema kwamba Sumaye alijiuzulu au kuachishwa. Tungesema kwamba Sumaye bunge lake la saba liliisha (1995-2000) na lilipoingia bunge la nane Mkapa akateua mtanzania mwingine kuwa Prime Minister.
Tuiweke concept hii kwenye usahihi wake kama hivi.
Cc:
Mwanakijiji