Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,298
- 3,059
Sasa kwa miaka katibu thelathini tumefuata sera na ushauri wa IMF na Benki ya Dunia? Tumeridhika?
Mwalimu hakutaka kuendeshwa na Wazungu!
Baada ya kueleza hayo alinyanyuka kwa hasira na kuwaacha wageni wametunduwaa!!! yaani hapo ni kama namuona nyerere live alivyokunja ndita.
Sokoine hakuwahi kujiuzulu kwa sababu ya kutofautiana na Nyerere. Kama kuna mtu aliyekuwa karibu kikazi na Nyerere alikuwa ni Sokoine. Alijiuzulu kwa ajili ya matibabu na pia fursa ya kujiendeleza kielimu. That is a fact. Lete jingine.
Jasusi,
Mbona na wewe unaharibu sasa? Sokoine hakuwahi kujiuzulu kwa sababu yoyote. Alichaguliwa April 12, 1977 kuwa Prime Minister.
Leo tuko kwenye bunge la 10, hili la Anne Makinda. Hivyo, Sokoine wakati anachaguliwa alikuwa ni mbunge katika bunge la 03 ambalo mwisho wake ulikuwa ni uchaguzi wa mwaka 1980.
Akakaa na post hiyo hadi bunge lilipovunjwa mwaka 1980 na nchi ikaingia kwenye uchaguzi mkuu wa serikali mpya yaani kati ya Nyerere na na mpinzani wake wa siku zote aliyeitwa kivuli.
Uchaguzi mkuu ukafanyika Jumapili, October 26, 1980, na Nyerere akakishinda kivuli kwa kura nyingi tena zaidi ya 90% ndipo akawa na kazi ya kuunda Baraza jipya la mawaziri kutokana na bunge jipya la 04.
Baada ya Nyerere kuapishwa, kazi ya kwanza ya kuunda cabinet ikawa ni kuteua Prime Minister kama ilivyotakiwa. Hivyo, November 07, 1980, siku 10 baada ya uchaguzi akamteua Cleopa Msuya kuwa Prime Minister.
Hivyo, huwezi kusema kuwa Sokoine alijiuzulu kwa sababu yoyote. Hapana. Muda wa bunge lake la tatu uliisha ikaja zamu ya bunge la nne.
Hata Mkapa angeweza kufanya hivyo yaani kutoendelea na Sumaye ile mwaka 2000, na tusingesema kwamba Sumaye alijiuzulu au kuachishwa. Tungesema kwamba Sumaye bunge lake la saba liliisha (1995-2000) na lilipoingia bunge la nane Mkapa akateua mtanzania mwingine kuwa Prime Minister.
Tuiweke concept hii kwenye usahihi wake kama hivi.
Cc: Mwanakijiji
Tumekuwa chini ya rwanda kimaendeleo, hata wakorea waliokuwa sawa na sisi sasa wako mbali sana. Kuna viongozi wanafikiri wakichapisha pesa zaidi (print more money to cover deficit) bado wanaweza kudhibiti thamani ya pesa yao, kama Idi Amini. Haiba yao huwa ni hasira wanapoambiwa ukweli na kususia vikao. Mwasho uongozi huwashinda na uchumi kuporomoka vibaya.mtoa mada.....what have we achieved so far after deceiving those IFM ideas in term of our social, economic and political development
Ni kama benki tu, haulazimishwi kukopa, ila ukitaka kukopa lazima ufuate masharti. Tatizo la watu kama nyinyi mnataka kukopa shilingi 20 mlipe shilingi 10 (Dezo). Mkinyimwa mnawaita wenzenu mashetani.I.m.f ni ya shetani na ipo kunufaisha watu wachache wanaomiliki dollar currency na federal bank of u.s.a ndo maana hata rais wa imf wanamchagua wao,,,,
sasa nyie mnaowasapoti mnadhani kuna faida yeyote ka hii miaka yote tuna shida baada ya kufuata wanachosema,,angalia haki ya ugiriki,uspania,ureno i.m.f imewamaliza,,
Ok, huenda kweli Sokoine hakujiuzulu. Jiulize ni kwa nini Mwalimu alimteua Msuya?
.Ni kwa sababu Sokoine alikwenda Ulaya mashariki kwa matibabu na masomo?
Kwa nini Sokoine aliporudi alichaguliwa tena kuwa waziri mkuu mpaka mauti ilipomkuta 1984?
Kwa nini Msuya hakumaliza term yake ambayo ingemalizika 1985?
Mi nadhani Mtei alikosea yeye kwanza ile approach ya kwenda na wageni kwa mwalimu wiki end na hoja yao na ambayo yaelekea mtei aliikubali tayari.Hivyo kwa hali ile alitazamia mwl.akubali haraka mbele ya wageni? Hakufikiri kinyume chake yaweza kuwaje.Kama ilikuwa lazima kwenda kwa mwl. siku ile,nadhani angeacha wageni watoe hoja ile,amshauri mwl.wapewe muda wa kushauriana na kutafakari,nadhani wangeondoka vizuri na hao wageni imf.Hivyo mzee mtei alichemka; hata mi ningeweza kumfukuza uwaziri.
Jasusi,
Sijui kwa nini ujiingize katika shughuli ya kujiuliza kwa nini Nyerere hakumteua Sokoine katika bunge la nne wakati hakuna hata tone ya sheria iliyomlazimisha kuendelea naye zaidi ya porojo za kwenye klabu za pombe.
Vivyo hivyo, siwezikujiuliza kwa nini Mwinyi naye alimuiga Nyerere kwa kumuacha Warioba aliyemaliza naye bunge la tano lakini lilipoanza bunge la sita akamchukua John Malecela.
Nadhani haya yanatosha kukujibu kwa swali la freedom ya uteuzi wa rais.
.
Sasa kama mwenyewe unasema alienda kwa sababu za kimatibabu au masomo, basi kumbe unajua sababu ya yeye kuwa nje ya nchi na hata ukatibu kata asingeuweza. Mbona baadhi yenu humu JF mko nje ya nchi, mnaweza kueleza sababu yenu?
Kwani kubadili waziri mkuu au waziri yoyote wakati hakuna cha kukuzuia ni jambo la kujiuliza au kujipa homework? Ile ni ofisi ya umma unaweza kuwekwa na kuondolewa wakati wowote hata kama hujafanya kosa lolote.
Hakuna kifungu kinachomlazimisha Waziri mkuu amalize term ya miaka mitano kama ambavyo kwenye bunge la tatu Kawawa hakumaliza miaka mitano na akampisha Sokoine.
Cc: Swiper
sio mashetani....wao wamefiriki hivyo kwa maslai yao.....kwa nini na sisi tusifikri what can be done to boost our economyI.m.f ni ya shetani na ipo kunufaisha watu wachache wanaomiliki dollar currency na federal bank of u.s.a ndo maana hata rais wa imf wanamchagua wao,,,,
sasa nyie mnaowasapoti mnadhani kuna faida yeyote ka hii miaka yote tuna shida baada ya kufuata wanachosema,,angalia haki ya ugiriki,uspania,ureno i.m.f imewamaliza,,