Kenya 2022 Sikiliza Busara za Ansbert Ngurumo kutoka juu ya funzo kutoka uchaguzi wa Kenya

Kenya 2022 General Election
Uchambuzi kutoka akili kubwa. Changia hoja na si matusi. Challenge hoja zake, then JF itakuwa na Great Thinkers.

Msikilize

CC Tundu Lisu; Mbowe Freeman, Godbless Lema

Hata mimi naamini ile handshake ilikuwa ni changa la macho kwa Raila !! UHURUTO ilikuwa ipo kazini ! Hapo akili kubwa imetumika !!
 
Hii nadharia inayozungumzwa ya Ruto na Uhuru kutengeneza "uadui" kati yao ili wamzime Raila, binafsi naiona ngumu kutekelezeka japo kweli inawezekana ilitokea.

Nakumbuka kuna wakati Ruto alimuomba samahani Uhuru kwa hicho kinachoitwa ugomvi wao, japo Uhuru alionekana kupuuza hakuwa msikivu sana kwa Ruto wala kumjibu chochote cha maana.

Binafsi nikitaka kuuzungumzia huu uchaguzi wa Kenya, zaidi nitaangalia mambo matatu; Uchaguzi ulivyofanyika, Ushindi wa Ruto, na malalamiko ya Raila.

- Uchaguzi wa Kenya, huu ulionekana kufanyika kwa uhuru na uwazi mpaka kura zilipomaliza kupigwa, hapakuwa na mawakala kusumbuliwa vituoni, karatasi za kupigia kura kuchelewa kufika vituoni, vituo kuchelewa kufunguliwa n.k kama ambavyo tumezoea kwenye chaguzi zetu Tanzania.

Hapo nawapa wakenya na tume yao 95% nikiamini kwamba kama palikuwepo na irregularities, basi zilikuwa kwa kiwango kidogo ambacho hakiwezi kuharibu taswira nzima ya uchaguzi wao mkuu waliofanya.

- Ushindi wa Ruto; binafsi nikiri, mwanzo sikutegemea kabisa kuona Ruto akiibuka na kutoa ushindani mkali kiasi kile, na mwishowe akatangazwa mshindi.

Kilichokuja kunifanya nijue wapi Ruto alipata nguvu zake nikajua ni kwenye kampeni zake, hapa naungana na mwandishi Ngurumo alipozungumzia maeneo kama kuwashawishi na kuaminiwa na vijana hasa kuhusu ukosefu wa ajira, hawa walijitokeza kwa wingi kupiga kura.

Tukaona picha wengine wakiwa na taulo viunoni, wengine miswaki mdomoni kuonesha vile walivyojitoa kumpigia kura waliyemuamini, pia chimbuko la Ruto ametokea tabaka la chini [hustler] ni sababu nyingine ya kuaminiwa na kuchaguliwa kwake, na hicho kinachoitwa ugomvi wake na Uhuru [sijui kama ni wa kweli, au uongo].

Hapo kwa tathmini yangu naamini Ruto ameshinda kihalali, alikuwa na hoja nzito alizofanikiwa kuwashawishi wapiga kura wakamchagua.

- Malalamiko ya Raila, hapa nimekuja kugundua kumbe wale makamishna wanne kati ya saba waliogoma kukubali matokeo ya ushindi wa Ruto waliteuliwa na Uhuru, hivyo kwa akili za kawaida watu wanaona kwamba inawezekana hii ndio sababu yao kumkataa Ruto wakimtaka "mgombea wao" nikimaanisha aliyewekwa na mtu wao ndie ashinde.

Lakini tatizo linakuja kwamba, kama tukienda na mentality hiyo ya kusema hao walioteuliwa na Uhuru walimtaka Raila ashinde, basi nami naweza kusema pia, inawezekana na huyo Chebukati ambaye hakuteuliwa na Uhuru, akawa kipenzi cha Ruto ndio maana akampa ushindi.

Hivyo kama picha itaenda kwa mtindo huo, basi naona madai ya Raila na hao makamishna wanne kuamini kwamba matokeo yaliyotangazwa na IEBC yalikuwa na tatizo, ni VALID, kwasababu inaonekana hiyo tume ilikuwa na pande mbili zenye wagombea wao tofauti, hapa tume kwa mtazamo wangu inapoteza uhalali wake.

Kwa hali hiyo, inavyoonekana kwa nje, hakuna wa kumuamini kati ya Chebukati na makamishna wake watatu wa IEBC, au Makamu wake na makamishna wake wanne, naona tuiachie Supreme Court yao ije kutupa majibu ya mwisho, mpaka hapa Urais wa Ruto ni 50% anything can happen mahakamani.
 
Kuhusu vijana kutakamanadiliko, hata hapa Tanzania wako wengi ninavyoona, shida ni pale hasa wale wa vyioni kikoansiliaha sehemu waliopo lakini ikibakia muda wawili moja kabla ya kupiga kura, Serikali ambayo inaongozwa na mgombea, inavifunga vyuo vyote, na kuwataka Wana vyuo kuondoka Mara moja. Hii inawafanya kukosa sifa ya kupiga kura kwa sababu wanakoenda huko hawakujiandikisha. Nafikiri hili nalo ni tatizo la kuangaliwa kwa mapana zaidi kwa chaguzi zijazo.
 
Hii nadharia inayozungumzwa ya Ruto na Uhuru kutengeneza "uadui" kati yao ili wamzime Raila, binafsi naiona ngumu kutekelezeka japo kweli inawezekana ilitokea.

Nakumbuka kuna wakati Ruto alimuomba samahani Uhuru kwa hicho kinachoitwa ugomvi wao, japo Uhuru alionekana kupuuza hakuwa msikivu sana kwa Ruto wala kumjibu chochote cha maana.

Binafsi nikitaka kuuzungumzia huu uchaguzi wa Kenya, zaidi nitaangalia mambo matatu; Uchaguzi ulivyofanyika, Ushindi wa Ruto, na malalamiko ya Raila.

- Uchaguzi wa Kenya, huu ulionekana kufanyika kwa uhuru na uwazi mpaka kura zilipomaliza kupigwa, hapakuwa na mawakala kusumbuliwa vituoni, karatasi za kupigia kura kuchelewa kufika vituoni, vituo kuchelewa kufunguliwa n.k kama ambavyo tumezoea kwenye chaguzi zetu Tanzania.

Hapo nawapa wakenya na tume yao 95% nikiamini kwamba kama palikuwepo na irregularities, basi zilikuwa kwa kiwango kidogo ambacho hakiwezi kuharibu taswira nzima ya uchaguzi wao mkuu waliofanya.

- Ushindi wa Ruto; binafsi nikiri, mwanzo sikutegemea kabisa kuona Ruto akiibuka na kutoa ushindani mkali kiasi kile, na mwishowe akatangazwa mshindi.

Kilichokuja kunifanya nijue wapi Ruto alipata nguvu zake nikajua ni kwenye kampeni zake, hapa naungana na mwandishi Ngurumo alipozungumzia maeneo kama kuwashawishi na kuaminiwa na vijana hasa kuhusu ukosefu wa ajira, hawa walijitokeza kwa wingi kupiga kura.

Tukaona picha wengine wakiwa na taulo viunoni, wengine miswaki mdomoni kuonesha vile walivyojitoa kumpigia kura waliyemuamini, pia chimbuko la Ruto ametokea tabaka la chini [hustler] ni sababu nyingine ya kuaminiwa na kuchaguliwa kwake, na hicho kinachoitwa ugomvi wake na Uhuru [sijui kama ni wa kweli, au uongo].

Hapo kwa tathmini yangu naamini Ruto ameshinda kihalali, alikuwa na hoja nzito alizofanikiwa kuwashawishi wapiga kura wakamchagua.

- Malalamiko ya Raila, hapa nimekuja kugundua kumbe wale makamishna wanne kati ya saba waliogoma kukubali matokeo ya ushindi wa Ruto waliteuliwa na Uhuru, hivyo kwa akili za kawaida watu wanaona kwamba inawezekana hii ndio sababu yao kumkataa Ruto wakimtaka "mgombea wao" nikimaanisha aliyewekwa na mtu wao ndie ashinde.

Lakini tatizo linakuja kwamba, kama tukienda na mentality hiyo ya kusema hao walioteuliwa na Uhuru walimtaka Raila ashinde, basi nami naweza kusema pia, inawezekana na huyo Chebukati ambaye hakuteuliwa na Uhuru, akawa kipenzi cha Ruto ndio maana akampa ushindi.

Hivyo kama picha itaenda kwa mtindo huo, basi naona madai ya Raila na hao makamishna wanne kuamini kwamba matokeo yaliyotangazwa na IEBC yalikuwa na tatizo, ni VALID, kwasababu inaonekana hiyo tume ilikuwa na pande mbili zenye wagombea wao tofauti, hapa tume kwa mtazamo wangu inapoteza uhalali wake.

Kwa hali hiyo, inavyoonekana kwa nje, hakuna wa kumuamini kati ya Chebukati na makamishna wake watatu wa IEBC, au Makamu wake na makamishna wake wanne, naona tuiachie Supreme Court yao ije kutupa majibu ya mwisho, mpaka hapa Urais wa Ruto ni 50% anything can happen mahakamani.
Apa naona akili za kipinzani au upinzani wa levo za juu za kimataifaa zaidi..huu ndo uchanganufu wa kimikakati ya upinzani,na hili kama chadema mkiwa na akili kama izi mtakua na maana halisi ya upinzani ...upinzani sio kuropoka tuu ovyoo, upinzani ni kuegemea haki na kua muazi .....hongera kutoka uku ugahaibuni
 
Mkuu mrangi , asante kuni tag
P
Pascal angali analysis ya mwenzako, mwandishi wa habari kama wewe! Una uwezo kama huo? At one time everybody admired you kwa swali ulilomuuliza Magufuli, The shetani by the way, from that time you vanished into thin air due to kutafuta cheo! Leo unahangaika na ubunge wa EALA........ you can make ends meet through high level thinking journalism!
 
Kwahiyo kupigana muda mrefu ndo kuna kupa uhalali wa kupata unachokipignia!?

Yani kwa vile Mbowe kataabika sana basi anastahili kuwa Rais!? Hujui siasa za TZ ni biashara!? Ni kama kuwa na ki mgahawa tu ,unapambana kisife. Eti Mbowe awe Rais!! Acha ujinga.
 
Back
Top Bottom