Siku 40 bila mwamba: Ulituheshimisha sisi wanyonge na masikini, pumzika kwa amani Hayati Dkt. Magufuli

Siku 40 bila mwamba: Ulituheshimisha sisi wanyonge na masikini, pumzika kwa amani Hayati Dkt. Magufuli

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
207
Reaction score
677
SIKU 40 BILA MWAMBA: ULITUHESHIMISHA SISI WANYONGE NA MASIKINI,PUMZIKA KWA AMANI JPM.

Katika awamu ya nne ya Rais Mstaafu Kikwete kurudi nyuma hadi Azimio la Zanzibar, Matajiri na Wafanyabiashara walikuwa na Jeuri za kila aina,kwa maana walianza kufanikiwa kuifanya CCM kuwa ya Wafanyabiashara, Wakulima na Wafanyakazi kitu ambacho kilikiuka miiko ya CCM iliyokuwa ya Chama Cha Wakulima na Wafanyakazi,na CCM ambayo inaongozwa na itikadi ya Kijamaa,sio ya Kibepari.

Dhana ya Wafanyabiashara kuhodhi mali za CCM na kuitawala CCM iliwapa jeuri Matajiri ambao wengi wao ni Wafanyabiashara waliokuwa wafadhiri lakini pia Mafisadi,jeuri ya Matajiri ilikuwa kubwa hasa awamu ya nne,matajiri walifikia mpaka kuamua uhai wa watu masikini waishi vipi wakae wapi wale nini kwa maana gap la tajiri na masikini lilikuwa kubwa na baadhi ya matajiri walikuwa na utajiri kiasi cha kuweza kuikopesha Serikali.

Alipoingia Hayati Rais Daktari John Pombe Magufuli alituheshimisha wanyonge ambao tulikuwa tukionewa na matajiri hata sauti zetu zisisikike popote, Wanyonge ambao hatukuwa na mtu wa kutupa kimemo ili twende kwa Mkurugenzi fulani atuajiri,Rais wa Awamu ya tano, Daktari John Pombe Magufuli alituheshimisha sisi Masikini (Mimi nikiwemo) kuwa hata sisi pia ndani ya hii Ardhi ya Mama Tanzania tuna thamani yetu,tuliokuwa matombo Morogoro tuliweza kupata ajira tukiwa kijijini matombo na wasiopata walikuwa na matumaini ya kupata, Hayati Rais Magufuli alitupa ujasiri (akatujaza) jeuri sisi masikini mpaka Matajiri nao wakaanza kutunyari (kutuogopa) Wanyonge na masikini nasi tukaanza kuona kuwa Tanzania ni nyumbani kwetu sio nyumbani kwa matajiri peke yao.

Watu wanauliza mnyonge ni nani? wengine wakianzisha kampeni wasiitwe wanyonge,lakini niwaambie mnyonge ni mtu yule anaepata mlo mmoja au miwili kwa siku, akipata milo mitatu kwa shida,inabidi achakarike na asisumbuliwe, mfano Mmachinga anafukuzwa na askari sehemu yake anayofanya biashara. JPM aliwapa kibali cha unafuu, wataacha kumpenda?kwa mnyonge, akipata kile anachotafuta bila kusumbuliwa, ni Raha yake na anamuamini aliyemuwezesha,Hayati Rais John Pombe Magufuli aliweza hilo.

#Ahsante Rais Magufuli
#Pumzika kwa Amani Mwamba.
 
Uliona wapi mnyonge na masikini akaheshimiwa? 'Haipogo' hivyo duniani. Na isitoshe kwanini usiombee mtu akutoe kwenye unyonge na umasikini badala yake unashukuru kakufanya sasa unatambulika rasmi kuwa u mnyonge na masikini?

Ingekuwa amewasaidia mliokuwa wanyonge na sasa si masikini tena hapo ingekuwa afadhali sana. Sasa mnashukuru kisa amewafanya mmekuwa proud na unyonge na umasikini wenu na matokeo yake mnachukia matajiri bila kujali wameupataje utajiri wao.

Shida sana.

We dogo sikia, tangu kuumbwa kwa dunia hii hakuna mnyonge na masikini aliyeheshimiwa. Amka tafuta kazi chakarika tafuta hela acha kujisifia unyonge na umasikini.
 
Daah katika tawala zote zilizopita hakuna watu walioishi kama mashetani kama katika utawala wa awamu ya 5 si kwa matajiri si kwa masikini,ukija kwa wale aliowaita yeye ni mtawala wa wanyonge ndo walikatwa shingo kabisaa badala ya kunyongwa, kila kona yalikuwa ni Mayowe matupu kama nchi iko kwenye moto wa jehanamu aliyoandaliwa shetani na malaika wake.
 
Aisee kama ni hivi basi wanyonge ni wajinga sana.
Wajane watajiliza humu mpaka kamasi ziishe na kukauka sio leo 😂😂😂 walie tu
SAMIA huyoooo.. maisha yanaendelea.
Sisi kwetu raha tu...tushafukia kwisha kabisa...🙅🏽🙅🏽🙅🏽 Chaliii!! na gundi tumeziba domo chafu hatutaki kusikia matusi yake..💃🏾🕺🏽💃🏾🕺🏽💃🏾🕺🏽
 
Back
Top Bottom