#COVID19 Siku 60 zijazo Tanzania inaweza kuwa zaidi ya India kwenye suala la COVID-19

aisee haya maneno tulishaambiwa sana mkuu, toka mda tu.. kabla hata ya india kabla hata ya uganda... lakini bado tuko tu, na wala hatuendi mahali,

NA HAKUNA KITU MNAWEZA KUTUFANYA
Sya bana tupo
 
Kosa langu ni nini kwenye huu uzi? Ni kutoa angalizo au ni kusema kuna uzembe katika kupambana na huyu mdudu?
Kwanini unafikiri hadi sasa hatujafikia India hasa ukizingatia tumeacha kuchukua tahadhari toka mwaka jana? kinachokufanya uone hatujafikia India ni kipi?
 
Kwanini unafikiri hadi sasa hatujafikia India hasa ukizingatia tumeacha kuchukua tahadhari toka mwaka jana? kinachokufanya uone hatujafikia India ni kipi?
Mwanzo kila mtu alipambana kivyake,kuvaa barakoa,kupiga nyungu, kujihadhari pia. Tofauti ya Tanzania na India sisi hatukuwa na kirusi kipya sasa kimeingia na watu wamekipuuza
 
Mwanzo kila mtu alipambana kivyake,kuvaa barakoa,kupiga nyungu, kujihadhari pia. Tofauti ya Tanzania na India sisi hatukuwa na kirusi kipya sasa kimeingia na watu wamekipuuza
Hiyo mwanzo unayoizungumzia wewe kulikuwa na tahadhari kwa kiasi gani hadi uweze kufikiri kwamba ilisaidia? kwa sababu muda wote serikali ilikuwa inalalamikiwa haichukui tahadhari kwa kiwango kinachotakiwa, humu Jf tu watu walikuwa wanasema hatuwezi kuindoa corona kwa kunawa mikono tu kumaanisha hatukuwa tukichukua hatua za kupambana na corona kwa kiwango kinachostahili. Sasa leo mtu akiniambia kwamba tulichukua tahadhari inanishangaza sana.

Yamepita mawimbi mangapi na ukizingatia hatukuwa tukichukua tahadhari muda wote huo?
 
we jamaa acha kusikiliza wanasiasa imagine kipindi kile bila magufuli si tungekwisha kwa hofu kila mtu alikua ana speculate lake au nasema uongo ndugu zanguuuu
 
Kama sijakosea India hawakupuuzia walichukua hatua kedekede.

Sasa we unataka tuchukue hatua gani akati hatua walizochukua india na wakafa ndo izoizo tutachukua na sisi?
 
Tutoletee mashudu yako hapa.
Unataka tukae lock down ndugu zako huko namtumbo watakula nini?
Hamjaanza kusema haya leo
 
Wazuie vyote vyote ila si nyumba za Ibada kwa sisi waumini. Maaana sisi kuishi kwetu ni Kristo na kufa Kwetu ni Ibada pia.

Afu sijui watu kwa nini wanaogopa hivyo kufa . Kufa ni kawaida tu bana ukishazaliwa wewe ishi kwa Imani yako Mda ukifika basi.
 
Kama sijakosea India hawakupuuzia walichukua hatua kedekede.

Sasa we unataka tuchukue hatua gani akati hatua walizochukua india na wakafa ndo izoizo tutachukua na sisi?
Wanasema India kuna muda watu walilegeza kuchukua hatua kwamba kulikuwa na mikusanyiko na ndio iliyowaletea hayo madhara.
 
Unataka tufungiwe?
 
Sisi tupo kwenye mbio za mwenge kusambaza vizuri [emoji23]
 
Aisee watabiri mmekuwa wengi hadi mnakera.
 
Kosa langu ni nini kwenye huu uzi? Ni kutoa angalizo au ni kusema kuna uzembe katika kupambana na huyu mdudu?
Kosa lako ni kurudi rudia ishu ambayo tunaijua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…