Katika muhula wa Biden na Harris, wahamiaji haramu zaidi ya milioni 20 wameingia Marekani, wengi wakitumia mpaka wa Mexico na baadhi Canada, wahamiaji haramu wengi hasa wa wanaoingia kwa mpaka wa Mexico wakiwa ni wahalifu waliokimbia nchi zao ama wahanga wa kutumikishwa kihalifu kuanzia wauaji, wabakaji, punda wa kubeba madawa, watoto wanaovushwa kutumikishwa kingono (sex traffiking), n.k.
Rais wa Mexico na waziri mkuu wa Canada hawakufanya jitihada, waliichukulia poa sana serikali ya Biden / Harris
Ni jambo lililowakera sana Wamarekani na kupelekea wengi kumpigia kura Trump mwenye historia ya mafanikio makubwa ya kudhibiti wahamiaji haramu katika muhula wake wa 2016 - 2020.
Trump kachimba mkwara wa kuchapa ushuru wa 25%, matokeo yameonekana ndani ya siku chache sana
Tamko la Trump 25 - Novemba - 2024
Kama kila mtu anavyofahamu, wahamiaji haramu wengi wanamiminika kupitia Mexico na Canada, wakileta uhalifu na dawa za kulevya kwa viwango ambavyo havijawahi kuonekana hapo awali. Hivi sasa, msafara mkubwa kutoka Mexico, wenye maelfu ya watu, unaonekana kutoshikika katika jaribio lake la kuvuka mpaka wetu ulio wazi kwa sasa.
Kuanzia Januari 20, kama mojawapo ya Amri Zangu za Kwanza za Utendaji, nitasaini hati zote zinazohitajika kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa BIDHAA ZOTE zinazoingia Marekani kutoka Mexico na Canada, pamoja na mipaka yao isiyo na udhibiti.
Ushuru huu utaendelea hadi pale Dawa za Kulevya, hususan Fentanyl, na Wahamiaji Haramu wote watakapoacha uvamizi huu wa Nchi Yetu! Mexico na Canada wanayo haki na uwezo kamili wa kutatua tatizo hili ambalo limechukua muda mrefu.
Tunadai rasmi kwamba watumie uwezo huu mara moja, na mpaka watakapofanya hivyo, ni wakati wa wao kulipa gharama kubwa sana!
28 - Novemba - 2024
Nimekuwa na mazungumzo mazuri sana na Rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum Pardo.
Amekubali kusitisha uvukaji kupitia Mexico na kuingia Marekani (kinyemela), hatua inayofunga kabisa mpaka wetu wa Kusini.
Pia tumefanya mazungumzo kuhusu hatua za kusitisha wimbi kubwa la dawa za kulevya zinazoingia Marekani, pamoja na matumizi ya dawa hizi ndani ya Marekani. Mazungumzo haya yamekuwa yenye mafanikio makubwa!
30 - Novemba - 2024
Justin Trudeau, Waziri mkuu wa Canada kapanda Jet mpaka Marekani na kunyooka moja kwa moja Florida nyumbani kwa Trump kwajili la mazungumzo ya ana kwa ana