Siku, dakika za mwisho kabla ya Ben Saanane kutoweka

Siku, dakika za mwisho kabla ya Ben Saanane kutoweka

Hata kama nitapita miaka 20 haya mambo yatakuja kuwa hadharani na waliohusika hata kama ameshakuwa vikongwe watasongezwa kwa pirato kujibu tuhuma. Jinai huwa haiozagi ... ndipo utamu ulipo.
 
Hata kama nitapita miaka 20 haya mambo yatakuja kuwa hadharani na waliohusika hata kama ameshakuwa vikongwe watasongezwa kwa pirato kujibu tuhuma. Jinai huwa haiozagi ... ndipo utamu ulipo.
Na habari za Ben hazitofutika milele kwa vizazi na vizazi
 
Haikuwepo haja ya kumpoteza pamoja na ameuliwa na hawa madhalimu wakuja lakini yameshindwa kuuwa siri.
Ushindi ni kuuwa siri na sio kuuwa watu,ukiuwa mtu siri uhamia kwa wengine.Uwa siri usiuwe mtu.
 
Ukishajua kuwa Kuna kitu kinaitwa nyuma ya mapazia huna haja ya kulalama!
Ili siasa ziende kuna Mambo mengi huwa yanaendelea chini yake! Naandika kifumbo
Jamii ambayo haina nyuma ya pazia Ni rahisi kuteketea.
Inategemea na huyo aliyoko nyuma ya hiyo pazia sasa kama ni lucifer. lazima haya yatokee, nchi yenye viongozi ambao hawamtegemei Mungu wa kweli hata matukio ndio dalili zake hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
US is Watching ...Bashite Ushamezeshwa NDOANO ...On To The Nex One --KICHWA SAMAKI.
 
Uongozi wa chama alichokua anakifanyia kazi ni mzito sana kwenye ufuatiliaji wa hili jambo.
 
Hata kama nitapita miaka 20 haya mambo yatakuja kuwa hadharani na waliohusika hata kama ameshakuwa vikongwe watasongezwa kwa pirato kujibu tuhuma. Jinai huwa haiozagi ... ndipo utamu ulipo.
Daaah! Kesi ya mbowe imeibua mambo sana huyu ASP Jumanne Malangahe ahojiwe
20220111_200336.jpg
 
Siku, dakika za mwisho kabla ya Ben Saanane kutoweka


Siku chache kabla ya kupotea katika mazingira yasiyoelezeka, kada wa Chadema, Ben Saanane alifanya mambo mengi kama mawasiliano yake binafsi na pia ya chama chake.
Hata hivyo, kati ya mawasiliano hakuna kilichosaidia kung’amua ni katika mazingira gani mwanasiasa huyo kijana alipotea na yuko wapi hivi sasa; hai au amekufa.

Novemba 14 mwaka jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa Ben kuonekaka ofisi za makao makuu ya Chadema yaliyopo Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni ambako alitumia muda wake mwingi.

Siku hiyo alisaini kitabu cha mahudhurio ya watumishi wa ofisi hiyo na kufanya shughuli zake za kichama. Hiyo ikawa siku ya mwisho kwa Wanachadema kumuona.

Ben alikuwa msaidizi wa karibu wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akimsaidia kufanya tafiti na uchambuzi katika masuala ya siasa na uchumi.

Siku alipotoweka, vikao vya Bunge vilikuwa vikiendelea mjini Dodoma, na ni katika kipindi hicho hicho Taifa lilitangaziwa kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta.

Wakati hayo yakitokea, Ben hakuwa Dodoma na bosi wake lakini aliwasiliana na Mbowe kwa kumtumia ujumbe mfupi wa simu kumpa pole kwa msiba mkubwa wa kitaifa. Hii ikawa mara yake ya mwisho kuwasiliana na Mbowe.

Ingawa kwa wanachadema, Novemba 14 ilikuwa siku ya mwisho kuonana naye, kwa majirani zake na watu wengine walikuwa na siku moja zaidi. Siku iliyofuata, yaani Novemba 15, Ben aliamkia nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya ufuatiliaji wa mawasiliano yake ya simu inaonesha kuwa Ben alitoka Mabibo asubuhi na kwenda au kupelekwa maeneo ya mikocheni ambako alitumia muda mrefu sana huko.

Mawasiliano yanaonyesha baada ya kutumia masaa kadhaa eneo la Mikocheni, alirudi ama kurudishwa eneo la Mabibo jioni. Alikuwa na nani na akifanya nini ni swali ambalo si ndugu zake wala vyombo vya usalama wameweza kulijibu.

Ufuatiliaji wa mawasiliano yake unaonyesha pia kuwa siku hiyo hiyo jioni simu yake ilitumika kutoa Sh50, 000 kwa wakala wa M-Pesa aliye eneo la Mburahati. Hiki kilikuwa kitendo cha mwisho kufanywa na Ben kupitia simu yake ya mkononi. Tangu hapo utambuzi wa simu yake ukapotea kabisa katika mtandao.

“Tumejaribu kufuatilia inaonekana wamei-block (wameizuia) ile simu,” alisema John Mrema, ambaye ni mkurugenzi wa uenezi, mawasiliano na mambo ya nje wa Chadema.

“Mtu anayeweza kufanya hivyo si mtu wa kawaida. Tulikuwa tunatumia njia mbalimbali kutafuta taarifa za Ben, sasa huwezi tena kum-trace (kumpata).

“To be frank (kusema kweli) ukitafuta namba ya Bern Saanane, ukiingiza kwenye system (mfumo) yao, unatakiwa uwe na password (nywila). Na ni simu hiyo tu sio simu zote zina password. So inaonekana ni mtu mmoja tu ndio anaweza kuaccess details (kuziona taarifa) za simu ya Ben.

“Kwa hiyo, inaonekana kuna mtu ambaye anacontroll (anadhibiti) hiyo system.”

Wakati ndugu wa karibu na viongozi wa Chadema wakitumia kila mbinu kujua aliko Ben, Desemba 24, siku moja kabla ya sikukuu.........

Habari hii ya kupotea kwa Ben Saanane ina endelea kwenye App ya Chadema ifungue uendelee kusoma au download hapa.

View attachment 601722
Chadema News – Програми Android у Google Play

PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana

~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia

- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Rip ben
 
Back
Top Bottom