Sakayo
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 56,368
- 161,448
Hahaha hahaha hahaha
Fanya kunitumia nauli ya kesho aki...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha hahaha hahaha
Aaah wapi.. wakafe mbele na hela zaoHahahaaaa!! Fanya ujibebisha thathaa!!!shoga mwenye nacho hanuniwiii!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji3][emoji3][emoji3]yeye elfu 10 yote hiyoHujafulia wewee!!!una hela watu tunaendaga na 400 ya nauli tuu[emoji3][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaaa!mkononi ukiporwa je?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ujue sikuziweka hata kwenye pochi ili zisipotee nizione mkononi aki... Ilikuwa budget ya mpaka ijumaa!!
Natafuta wateja wa mayai hapa naona kimya! Kesho sasaaa sijuii
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji3][emoji3][emoji3]yeye elfu 10 yote hiyo
Umeona eehh[emoji3][emoji3][emoji3][emoji16][emoji16]!!!yaani kwanza Mimi ningemuambia sina mwanangu kannue msomi La 500 linatosha au Yale profesa ya 1500 baasi chenji yangu nasepa nayo[emoji3][emoji3][emoji3]yeye elfu 10 yote hiyo
Watu hupora pochi dada, thy nikashika kwa mkonoo...Hahaaa!mkononi ukiporwa je?
Nauli huna ila uhakika wa kula upooo!!!wateja watakuja tu! Ukikosa utakula mayai yenyewe baasii!!!?
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha hahaha hahaha hahahaUmeona eehh[emoji3][emoji3][emoji3][emoji16][emoji16]!!!yaani kwanza Mimi ningemuambia sina mwanangu kannue msomi La 500 linatosha au Yale profesa ya 1500 baasi chenji yangu nasepa nayo
Sent using Jamii Forums mobile app
Remmy Ongala kama sikosei.Unanikumbusha mbali dadekii yaani siku hiyo nguo zote kwenye kabati zitatolewa, mikoba zipu zinafunguliwa na kufungwa. Hakuna kitu kibaya Duniani kama shida hii nyimbo nzuri sijui kaimba nani?
Mmmh ...shost huyu haijui shida!
Una mwekundu ukachagua kula au kwenda hospital?
Kuna mwingine hata mia hana anaumwa na ana njaa
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23]Umeona eehh[emoji3][emoji3][emoji3][emoji16][emoji16]!!!yaani kwanza Mimi ningemuambia sina mwanangu kannue msomi La 500 linatosha au Yale profesa ya 1500 baasi chenji yangu nasepa nayo
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha hahaha hahaha hahaha
Nimemuonea huruma sana jamanii... Msomi upili kwani hutumia hizo kweeli
Mwanamke mipangoKuna siku niliamka sina hata mia, watoto wanataka kula ndani kuna unga wao wa uji tu kidogo...
Nikamwambia dada waogeshe watoto (wawili) nikawapikia uji wakanywa wakaoga, nikamwambia dada nendeni kwa babu ( wakati huo baba alikuwa anaishi mbali kidogo na kwangu kama 2km) mkashinde huko nitawafuata.
Hapo nimewaza waende kwa babu wakale mchana na jioni huku nitafute namna ya kupata hela ya kuamkia kesho yake. Hao wakaenda zao kumsalimia babu ( kumbe wanaenda kudoea msosi [emoji23][emoji23][emoji23] lol)
Basi nikaenda kwa rafiki yangu fundi simu nikamwambia hali halisi akasema we kaa hapa tutakachopata tutagawana. Tumekaa kuanzia saa nne asbh mpaka kumi jioni hakuna mteja [emoji26] dah sasa tufanyaje...
Mara katokea mzee amenunua simu sasa hawezi kuweka application basi fasta nikamwambia lete, nikamwekea zote na nikamwambia kuhusu truecaller akaipenda ikabidi nimdanganye hii inalipiwa mzee akasema hakuna shida.
Akatoa elf 10 ikabidi tugawane na mshkaji wangu, mie huyo nikaenda kufuata watoto, nikasubiri cha usiku tukala kabisa bajeti ya siku ikakamilika. Tukarudi zetu home kulala
Mkuu nimecheka sana kwa fix mlizokua mnapiga kumbe hamna kitu...."mnapika nini KUKU"2015 nikiwa na mshikaji wangu mmoja, kazini kulikuwa na mambo ya ajabu hivyo pesa ilikuwa haipo.
Imefika tarehe 24 Des hakuna msosi ndani hata wa panya kula, nikamuuliza mshikaji vipi tunafanyaje na hali hii. Akasema sisi ni wanaume hatutakufa njaa kwa siku moja hivyo tuvumilie. Tukafanya maajabu jioni tukapata unga na mboga tukala.
Des 25 Asubuhi tunaamka wote kama kima hakuna mwenye wazo la kwenda kazini ila kila mmoja anawaza atakula nini, wazo likaja kuna mama mmoja ni rafiki yetu huwa anatuuzia sana mboga na muda mwingine anatukopesha kama hatuna cash, yeye alikuwa anatuita Magufuli na Lowasa kwani kipindi hicho hayo majina yaliteka nchi sana na pia muda wote tulikuwa tukiongozana na yule mshikaji.
Tulienda hadi gengeni hiyo ilikuwa saa 6 na pale tulipokuwa tunaishi walitutambua kwa sababu ya ucheshi wetu, majirani asubuhi wanauliza mbona hakunukii huko kwenu sisi hatuna muda nao njaa imeanza ku-take off kwenye runway. Wakati tunaondoka kwenda kwa yule mama kukopa mboga huku nyuma tukaacha vumbi, tuliwaambia majirani pikeni ila sisi tukirudi hapa tutafanya kufuru [emoji23] [emoji23] [emoji23].
Tumesogea hadi gengeni ili tupate mboga kwa yule mama ila hatukuamini tulichokiona pale gengeni. Yule mama hakuwepo na walikuwepo tu wauza nyanya, nikiwa bado najaribu kushirikisha moyo wangu nilichokiona ghafla nikaona demu wangu anatoka salon na rafiki yake pamoja na mtoto wa huyo rafiki yake.
Demu wangu alikuwa anakaa mtaa mwingine na rafiki yake alikuwa anaishi mtaa ule hivyo alikuja kwa rafiki yake siku ile ili wajiandae kwenda beach. (sikuwa na maelewano mazuri na yeye wakati huyo)
Akaniita na kuniuliza mbona mko hapa mchana huu mnafanya nini, nikamjibu tumekuja kununua nyanya tukapike mboga , akauliza mmepika nini nikamjibu KUKU. Wakaaga na sisi tubaki na maswali tutakula nini mtegemezi wetu hayupo (yule mama).
Mshikaji akasema oooh nimekumbuka nina shangazi hapa mjini, akapiga simu kwa shangazi yake kumuuliza kama yupo nyumbani na akasema yupo akamtania mshikaji njoo leo kwangu basi. Oooh alitania pasipo na dakika hiyohiyo tukaondoka na kwenda kwake, alikuwa kajiandaa vya kutosha tulikula na kusahau shida zetu na jioni ikafika sasa turudi kulala.
Majirani wakati huo wanasubiri kishindo chetu kumbe mikwara tu hatuna hata nyanya, tulifika kila mmoja akaingia ndani kwake kimya na kulala, haujapita muda mshikaji akanigongea oya leta sufuria kubwa, nikampa kumbe majirani wametuchagia chakula kama wahanga wa kimbunga. Aisee kile chakula kilikuwa kingi tukala siku mbili kingine tukamwaga maana kilituzidi.
Chakula mseto: nyama ya bata humo humo, ya kuku, ya ng'ombe, ya mbwa, ya bundi.
Aint you tired of little money, you need a big boyKila siku nimechacha hata leo