Siku gani ulichacha hutaisahau?

Siku gani ulichacha hutaisahau?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ujue sikuziweka hata kwenye pochi ili zisipotee nizione mkononi aki... Ilikuwa budget ya mpaka ijumaa!!

Natafuta wateja wa mayai hapa naona kimya! Kesho sasaaa sijuii
Hahaaa!mkononi ukiporwa je?

Nauli huna ila uhakika wa kula upooo!!!wateja watakuja tu! Ukikosa utakula mayai yenyewe baasii!!!?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unanikumbusha mbali dadekii yaani siku hiyo nguo zote kwenye kabati zitatolewa, mikoba zipu zinafunguliwa na kufungwa. Hakuna kitu kibaya Duniani kama shida hii nyimbo nzuri sijui kaimba nani?
Remmy Ongala kama sikosei.
Mmmh ...shost huyu haijui shida!

Una mwekundu ukachagua kula au kwenda hospital?

Kuna mwingine hata mia hana anaumwa na ana njaa

Sent using Jamii Forums mobile app


Never say never
 
Kuna siku niliamka sina hata mia, watoto wanataka kula ndani kuna unga wao wa uji tu kidogo...

Nikamwambia dada waogeshe watoto (wawili) nikawapikia uji wakanywa wakaoga, nikamwambia dada nendeni kwa babu ( wakati huo baba alikuwa anaishi mbali kidogo na kwangu kama 2km) mkashinde huko nitawafuata.

Hapo nimewaza waende kwa babu wakale mchana na jioni huku nitafute namna ya kupata hela ya kuamkia kesho yake. Hao wakaenda zao kumsalimia babu ( kumbe wanaenda kudoea msosi [emoji23][emoji23][emoji23] lol)

Basi nikaenda kwa rafiki yangu fundi simu nikamwambia hali halisi akasema we kaa hapa tutakachopata tutagawana. Tumekaa kuanzia saa nne asbh mpaka kumi jioni hakuna mteja [emoji26] dah sasa tufanyaje...

Mara katokea mzee amenunua simu sasa hawezi kuweka application basi fasta nikamwambia lete, nikamwekea zote na nikamwambia kuhusu truecaller akaipenda ikabidi nimdanganye hii inalipiwa mzee akasema hakuna shida.

Akatoa elf 10 ikabidi tugawane na mshkaji wangu, mie huyo nikaenda kufuata watoto, nikasubiri cha usiku tukala kabisa bajeti ya siku ikakamilika. Tukarudi zetu home kulala
Mwanamke mipango
 
WANAWAKE HAWAISHIWI MAMBO.
Walikutana Saloon wakati napita maeneo ya mbagala kizuiani.. Niliwaskia wakitambiana majina ya waume zao...

Wa 1- Mimi wangu ni SOSPETER nikipenda namuita SOS au PETER..

Wa 2- Mimi wangu EMMANUEL nikipenda EMMA au NOEL..

Wa 3-..mimi wangu GODLUCK nikipenda GOD au LUCK..

Wa 4- akanuna akaondoka zake !

Kumbe bwana wake anaitwa MBWAMBO!

Msaidie kufupisha.
 
Mbaya chache halafu kuna mtu una mdai pesa ndefu wakati we hata ya kula huna....kuna mpumbavu mmoja alinilisha mihogo minne ya kukaanga saa tatu usiku hapo mchana nilikuwa kwa hisani ya watu wa Marekani

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
2015 nikiwa na mshikaji wangu mmoja, kazini kulikuwa na mambo ya ajabu hivyo pesa ilikuwa haipo.

Imefika tarehe 24 Des hakuna msosi ndani hata wa panya kula, nikamuuliza mshikaji vipi tunafanyaje na hali hii. Akasema sisi ni wanaume hatutakufa njaa kwa siku moja hivyo tuvumilie. Tukafanya maajabu jioni tukapata unga na mboga tukala.

Des 25 Asubuhi tunaamka wote kama kima hakuna mwenye wazo la kwenda kazini ila kila mmoja anawaza atakula nini, wazo likaja kuna mama mmoja ni rafiki yetu huwa anatuuzia sana mboga na muda mwingine anatukopesha kama hatuna cash, yeye alikuwa anatuita Magufuli na Lowasa kwani kipindi hicho hayo majina yaliteka nchi sana na pia muda wote tulikuwa tukiongozana na yule mshikaji.

Tulienda hadi gengeni hiyo ilikuwa saa 6 na pale tulipokuwa tunaishi walitutambua kwa sababu ya ucheshi wetu, majirani asubuhi wanauliza mbona hakunukii huko kwenu sisi hatuna muda nao njaa imeanza ku-take off kwenye runway. Wakati tunaondoka kwenda kwa yule mama kukopa mboga huku nyuma tukaacha vumbi, tuliwaambia majirani pikeni ila sisi tukirudi hapa tutafanya kufuru [emoji23] [emoji23] [emoji23].

Tumesogea hadi gengeni ili tupate mboga kwa yule mama ila hatukuamini tulichokiona pale gengeni. Yule mama hakuwepo na walikuwepo tu wauza nyanya, nikiwa bado najaribu kushirikisha moyo wangu nilichokiona ghafla nikaona demu wangu anatoka salon na rafiki yake pamoja na mtoto wa huyo rafiki yake.

Demu wangu alikuwa anakaa mtaa mwingine na rafiki yake alikuwa anaishi mtaa ule hivyo alikuja kwa rafiki yake siku ile ili wajiandae kwenda beach. (sikuwa na maelewano mazuri na yeye wakati huyo)

Akaniita na kuniuliza mbona mko hapa mchana huu mnafanya nini, nikamjibu tumekuja kununua nyanya tukapike mboga , akauliza mmepika nini nikamjibu KUKU. Wakaaga na sisi tubaki na maswali tutakula nini mtegemezi wetu hayupo (yule mama).

Mshikaji akasema oooh nimekumbuka nina shangazi hapa mjini, akapiga simu kwa shangazi yake kumuuliza kama yupo nyumbani na akasema yupo akamtania mshikaji njoo leo kwangu basi. Oooh alitania pasipo na dakika hiyohiyo tukaondoka na kwenda kwake, alikuwa kajiandaa vya kutosha tulikula na kusahau shida zetu na jioni ikafika sasa turudi kulala.

Majirani wakati huo wanasubiri kishindo chetu kumbe mikwara tu hatuna hata nyanya, tulifika kila mmoja akaingia ndani kwake kimya na kulala, haujapita muda mshikaji akanigongea oya leta sufuria kubwa, nikampa kumbe majirani wametuchagia chakula kama wahanga wa kimbunga. Aisee kile chakula kilikuwa kingi tukala siku mbili kingine tukamwaga maana kilituzidi.

Chakula mseto: nyama ya bata humo humo, ya kuku, ya ng'ombe, ya mbwa, ya bundi.
Mkuu nimecheka sana kwa fix mlizokua mnapiga kumbe hamna kitu...."mnapika nini KUKU"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kipindi nipo nakaa hostel kuna siku niliamka sina hata mia mfukoni. sikula mchana nikanywa maji mengi ya kudownload. rafiki zangu wote wa chuoni na mtaani nikawaomba wanikopeshe lakini wote wakasema hawana kitu hata kidogo.

Sikuwa na mazoea ya kuomba hela nyumbani najiona nimekua sitegemei home. basi ikafika saa kumi jioni njaa kali sina hela na hakuna matumaini ya kupata hela ya kula. Nikafikiria nikope TALA najaribu kulog in naambiwa simu imeshatumika na mkopaji mwingine hivo siruhusiwi kukopa.

Nikaazima simu kwa mshikaji akawa hana bando la intaneti. Tukaanza kuzunguka room za jirani kutafuta mtu mwenye bando ili tuunge wifi. tukabahatika kupata bando ila hatukuwa na kitambulisho cha mpiga kura. tukaanza kutafuta kw washkaji ikabidi tuazime kwa mtu. Hapo imefika saa moja kamili zaidi ya masaa mawili tunahangaika kukopa.bila mafanikio.

sijui ilikuaje TALA ikashindikana kabisa tukadownload BRANCH. wakati bado tunaendelea na heka heka hizo simu ya jamaa ikazima na umeme ulikua umekatika.

Nikaunga waifai kwangu nikaingia jF nikafungua thread ya kuomba hela ya kula (sio kwa ID hii). wengi waliniponda ila kuna mtu alinisaidia elfu kumi ndo ikawa ponapona yangu nikaenda dukani kununua maandazi. sitamsahau mtu huyu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom