Siku gani ulichacha hutaisahau?

Siku gani ulichacha hutaisahau?

Siku ya kwanza kufanya mapenzi na kukojoa, sitokaa sahau ile raha mpaka nywele zinasimama, aisee hii kituina utamu zaidi ya asali.
 
Mwaka jana kuna siku nimeamka asubuhi sina kitu ,wife anaumwa ,mtoto anatakiwa kula ,ndani kuna unga,maharage Ila sina hela ya mkaa. Jirani muuza mkaa ananidai buku 7 ma siwezi kwenda kukopa tena. Nilidata kabisa,sina vocha kwenye sim na hata ningekua nayo bado sikua na mtu ambaye angeniazima hata buku.

Sent using Jamii Forums mobile app
@ipyax ukawezaje man story tam sana

Voxser empire
 
Haya maisha ukiona mtu ana kitu ana ringa muache tu..
Kuna siku nimegombana na baba mtoto
Akasusa akaondoka kama wiki
Hapo ni mjamzito

Sasa akiba ikawa imeniishia sina unga sina chumvi wala sukari,
Nikamtafuta shoga yangu tuliyekuwa tuna mtindo wa kukopeshana akaniambia mpaka saa saba atakuwa ameshanitumia 10,000
Moyo ukatawanyika na tabasamu likarejea
Nilikaa kwenye saa mpaka saa 12 jioni
Nikapiga simu yake mpaka sasa mwaka wa tano huwa hapokei simu.

Kama unapita hapa rafiki yangu T nilishasamehe usiogope kupokea simu yangu.


Sent using Jamii Forums mobile app
Haaahaaa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787]...mashost hao! Daadeki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
@ipyax ukawezaje man story tam sana

Voxser empire
Nilitoka home mkuu nikaanza kunzunguka tu mtaani make kelele za mtoto kulia zilikua zinaniumiza moyo.Kufika saa tano hivi nikaenda kwa rafiki yangu mmoja nikakuta mkewe yuko home.Nikamuuliza kama wana jiko la umeme waniazime,Bahati nzuri walikua na jiko dogo hawalitumii basi akanipatia.

Home nimeweka utaratibu wa kununua umeme wa mwaka mzima,units zilikuwepo za kutoshamake ilikua mwanzo wa mwezi.Nikapita kwenye kibustani chetu nikachuma mboga kufika ndani nikapia faster spinach,ugali nikawa nimeokoa siku. Tulitumia jiko la umeme kwa wiki 2 ndipo mambo yaka kaa sawa kuweza kulipa deni la mkaa kwa Jirani na kuweza kumudu kununua mkaa tena.

Baada ya hapo nilirudisha jiko kwa jamaa ,nikanunua la kwangu la umeme kwa ajili ya emergency kama ile ikija tokea tena. Fimbo za maisha sio poa kabisa sometimes.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom