Siku gani ulichacha hutaisahau?

Siku gani ulichacha hutaisahau?

hapo kwenye maji ya kudownload umenikumbusha mbali aisee
kipindi nipo nakaa hostel kuna siku niliamka sina hata mia mfukoni. sikula mchana nikanywa maji mengi ya kudownload. rafiki zangu wote wa chuoni na mtaani nikawaomba wanikopeshe lakini wote wakasema hawana kitu hata kidogo.

Sikuwa na mazoea ya kuomba hela nyumbani najiona nimekua sitegemei home. basi ikafika saa kumi jioni njaa kali sina hela na hakuna matumaini ya kupata hela ya kula. Nikafikiria nikope TALA najaribu kulog in naambiwa simu imeshatumika na mkopaji mwingine hivo siruhusiwi kukopa.

Nikaazima simu kwa mshikaji akawa hana bando la intaneti. Tukaanza kuzunguka room za jirani kutafuta mtu mwenye bando ili tuunge wifi. tukabahatika kupata bando ila hatukuwa na kitambulisho cha mpiga kura. tukaanza kutafuta kw washkaji ikabidi tuazime kwa mtu. Hapo imefika saa moja kamili zaidi ya masaa mawili tunahangaika kukopa.bila mafanikio.

sijui ilikuaje TALA ikashindikana kabisa tukadownload BRANCH. wakati bado tunaendelea na heka heka hizo simu ya jamaa ikazima na umeme ulikua umekatika.

Nikaunga waifai kwangu nikaingia jF nikafungua thread ya kuomba hela ya kula (sio kwa ID hii). wengi waliniponda ila kuna mtu alinisaidia elfu kumi ndo ikawa ponapona yangu nikaenda dukani kununua maandazi. sitamsahau mtu huyu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Apa ni sisi ambao tumechacha benk hamna ata hela ya kula hamna hujui utakula nini...,we kumbe atm imesumbua kwa masaa
Hamna mwenye uzi kauliza "Siku gani ulichacha hutaisahau?" na me siku hiyo ndio niliyochacha zaidi. Kukosa chakula ni kawaida!..
 
Back
Top Bottom