Siku gani ulichacha hutaisahau?

Siku gani ulichacha hutaisahau?

jamaa ana utani na shida huyu.... yani mfukoni una 10k na hadi una option kabisa ya kula au kununua dawa alafu anasema ana shida daaaaaaah



Sent using Jamii Forums mobile app
Hujui malaria wewe! Usiku ulikuwa mrefu sana. Dozi 10,000 siwezi kunywa hadi nile na ni mara tatu kwa siku. Afadhali ukose hata sumni ila usiwe mgonjwa unaweza kulala na njaa
 
kipindi nipo nakaa hostel kuna siku niliamka sina hata mia mfukoni. sikula mchana nikanywa maji mengi ya kudownload. rafiki zangu wote wa chuoni na mtaani nikawaomba wanikopeshe lakini wote wakasema hawana kitu hata kidogo.

Sikuwa na mazoea ya kuomba hela nyumbani najiona nimekua sitegemei home. basi ikafika saa kumi jioni njaa kali sina hela na hakuna matumaini ya kupata hela ya kula. Nikafikiria nikope TALA najaribu kulog in naambiwa simu imeshatumika na mkopaji mwingine hivo siruhusiwi kukopa.

Nikaazima simu kwa mshikaji akawa hana bando la intaneti. Tukaanza kuzunguka room za jirani kutafuta mtu mwenye bando ili tuunge wifi. tukabahatika kupata bando ila hatukuwa na kitambulisho cha mpiga kura. tukaanza kutafuta kw washkaji ikabidi tuazime kwa mtu. Hapo imefika saa moja kamili zaidi ya masaa mawili tunahangaika kukopa.bila mafanikio.

sijui ilikuaje TALA ikashindikana kabisa tukadownload BRANCH. wakati bado tunaendelea na heka heka hizo simu ya jamaa ikazima na umeme ulikua umekatika.

Nikaunga waifai kwangu nikaingia jF nikafungua thread ya kuomba hela ya kula (sio kwa ID hii). wengi waliniponda ila kuna mtu alinisaidia elfu kumi ndo ikawa ponapona yangu nikaenda dukani kununua maandazi. sitamsahau mtu huyu.

Sent using Jamii Forums mobile app
I'd yako ya zamani ni ipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu hili ni tatizo la watu wengi sana kwa hv sasa...hzi shule za kisasa ada zake zinakufanya upate msongo wa mawazo kuna haja ya wazazi wenye changamoto kama hizi wakutane na kujadili namna ya kulikabili hili swala.....shule za serikali nazo siku hizi hamna kitu aisee.
Bora Wewe, Mimi sijalipa ada ya term ya kwanza, yaani sijatoa hata Mia, nahisi akirudi likizo ya pasaka wanamtimua.
 
Daaah...
Mimi leo bana, metoka nyumbani natembea ili kusave hela ya boda iwe ya lunch, barabarani asubuhi mida ya 12:30 asubuhi nikakutana na mwanafunzi kama wa kidato cha tatu, akanisalimia ile tunapishana akasema dada samahi! Nikamjibu bila samahani mdogo wanguu, niambie akaniambia nakuomba unisaidie elfu moja ya daftari, niongezee na hii elfu hapa( huku akinionyesha elfu ingine) ninunue counter book baba kanipa elfu na haitatosha!

Nikasisimka kwanza, nikahisi kulia! Mkononi nimeshika elfu kumi na moja! Elfu tano mbili na elfu! Nilichokifanya nikampa ile elfu tano, anununue daftari mbili!

Nikamwambia Mungu asante kwa pumzi niliyonayo! Yaaani ilibaki nauli ya kazini kwenda na kurudi na chai pekee! Namshukuru Mungu hapajatokea dharura yoyotee!
aise;
 
Ndugu yangu hili ni tatizo la watu wengi sana kwa hv sasa...hzi shule za kisasa ada zake zinakufanya upate msongo wa mawazo kuna haja ya wazazi wenye changamoto kama hizi wakutane na kujadili namna ya kulikabili hili swala.....shule za serikali nazo siku hizi hamna kitu aisee.
Sasa mkuu tutajadili nini? Wenyewe wanatuambia Kama huwezi muhamishe mtoto, unashindwa maana shule Ina vigezo vyote ambavyo unavihitaji kwaajili ya mtoto wako. Labda serikali iingilie Kati hizi shule binafsi kitu ambacho naona Ni ngumu kidogo.
 
Back
Top Bottom