Pole sana....! I feel you, lkn mkuu ukiona unasuasua au unajibana sana kulipa ada ktk hizo shule, basi jua kuwa uwezo wako ni mdogo, usijilazimishe (huu ni ukweli mchungu), hata mimi binafsi suala la ada kwa mtoto huwaga changamoto, ila nimepanga na mwenzangu kukaa na kureview upya......ni kweli tunapenda watoto wetu wasome shule bora kbs, lkn ukweli ni kwamba uwezo wetu kutokana na majukumu ni mdogo, ada zimekuwa too much nowdays. Na hili nakuhakilishia siyo wewe tu, wapo wengi mnoooo, ambao wanashindwa na ada za hizi shule....ni vile tu hujapata wasaa wa kuona list ya wanaodaiwa wenzako.
Zamani Kulikuwa na option ya kuwapeleka watoto shule za serikali za English medium kama Olympio, diamond etc. Kwa hapa Dar, lkn hv sasa hizo shule hazina tofauti na za kayumba za kawaida, na kwa hali ilivyo hivi sasa mtoto kusoma shule ya English medium siy tu fashion, Bali ni lazima sana, sababu huko mbele mfumo wa ajira na elimu utabadilika sana, so ukimpeleka mwanao shule za kayumba tulizosoma sisi, utakuwa umemnyima fursa nyingi sana kwa kizazi chao huko mbele.
Mwisho lengo la kukuambia ukae na wazazi wenye same problem, ilikuwa uweze kupata faraja au hata utatuzi wa shida yako. As you know penye wengi pana mengi, unaposkia mtu mwengine ana tatizo kama lako, unapata psychological relief, na inakusaidia kuona ur not alone.