Updates:
Kuna mdau kaja na hesabu kali sana. Yeye, kama yeye anasema kuwa manage watu wengi ni tatizo kwa namna fulani. Nimemtoa shaka kuwa wala si tatizo maana watu wanakuwa managed kama wanunua hisa kwenye mabenki wanavyokuwa managed.
Lakini yeye katoa plan moja kali sana.
Anasema hivi:
Ili hiki kitu kiweze kwenda vizuri sana watu wasisumbuane ni lazima wawepo watu wenye maamuzi mazito, hao ndo watakuwa na commitment kubwa na drive kubwa kufanikisha jambo.
Nilipomuelewa nami kichwani kikaja wazo kama hivi maana of koz yupo sahihi.
Kwamba,
Kwa mfano, badala ya members 400,000 kila mmoja kutoa sh 5,000/- ambapo patapatikana sh. 2,000,000/- (bilioni mbili).
Tunaweza kufanya members 20,000 kila mmoja kutoa sh. 100,000/-
Yaani 20,000 x sh. 100,000/- = sh. 2,000,000,000/-. Hapa KEY members watakuwa wamepungua sana.
Ama, hata members 10,000 kwa kila mmoja kutoa sh 200,000/- sawa na sh. 2,000,000,000/-
Ama, members 5,000 kila mmoja kutoa sh. 400,000 sawa na sh. 2,000,000,000/-
Ama members 2,000 kila mmoja kutoa sh 1,000,000/- sawa na sh. 2,000,000,000/-
Tunaweza kusema sh 1,000,000/- itolewe ndani ya mwaka mmoja, kwamba kila mwezi member atoe sh 83,333.33/- kwamba ndani ya mwaka atakuwa ametoa sh. 1,000,000/-.
Halafu, hawa members 2,000 kunatengenezwa vikundi 2,000 ambapo kila member hapa atakuwa anawajibika kusimamia kikundi chake. Kunaweza kuwepo kikundi cha Temeke, USA River, Mabatini, Nyegezi, Area D, nk. Hiki kikundi sasa ndio kinakuwa kinawasajili wanachama wake kwa jinsi inavyofaa kwa utaratibu uliowekwa na JF Members SACCOS Limited. Nao kama kikundi kinaendesha business zao kwa jinsi waonavyo ina faida na msimamizi mkuu anakuwa yule KEY member.
Hao, watakaosajiliwa ndo hao JF visitors (guests and members) ambapo sasa watakuwa chini ya usimamizi wa yule KEY member founder wa JF Members SACCOS.
Mfano:
Kikundi cha Maghorofani kina wanachama 20. Nao wana mtaji wa sh 20,000,000/- (sio mchango bali mtaji kutoka JF Members SACCOS). Nao wakakopeshana labda kwa riba ya 5% kwa mwezi. Riba lazima iwe ndogo ili kuwezeshana. Ama wakafanya biashara yeyote watakayoona inafaa.
Nako JF Members SACCOS faida inayopatikana inashushwa kwenye vikundi vile vyenye wanachama, maana kazi kuu ya hii SACCOS ni kuhakikisha ustawi wa wanachama.
Hivyo kuna mawili mazuri hapa: Moja, kikundi kinafanya biashara na pia kuna gawio kutoka JF Members SACCOS kutokana na biashara za SACCOS.
Tunaweza pia kuamua, kila biashara ya kikundi faida inayopatikana sehemu fulani (nje ya gawio la kawaida) arejeshewe yule KEY member ule mchango wake wa sh. 1,000,000/- founding of the JF Members SACCOS Limited.
I think this is more superb interms of management!