Siku hizi kila nikila maharage tumbo linavurugika

Mama Sabrina

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
16,620
Reaction score
27,589
Zamani nilipenda sana kula maharage. Harage zito lililoungwa na vitunguu vingii na hoho, nazi au maziwa. Nilikuwa nikijaza maharage kwenye sahani wali unakuwa tepetepe, basi nilikuwa napenda kweli.

Hata enzi zile sekondari nilikuwa nakula tu naweka vitunguu, sukari na blueband na pilipili

Sijui nini kimetokea yamenikataa kabisa jamani nikila tumbo linaparanganyika kama vita humo ndani. Itanifanya hivyo hata wiki nzima au mbili jamani mpaka nimeyaogop. Sasa nayamiss leo naona yamepikwa hapa nimeona nilee kidogo nikanywa na maziwa nilipomaliza kula.

Je, kuna wengine mmeyashindwa kama mimi? Vidonda vya tumbo nimepima sina.

Nini itakuwa tatizo wajameni?
 
Last edited by a moderator:
Mimi maharage nachanganya na mboga za majan ni matamu balaa au mchuzi wa nyama
 
Mimi shule nilikua sili kabisa maharage. Hata home wakipika nilikua sili. Cha ajabu siku hizi nayapenda hatarii.
Yaan nikila wewe usiku nitajamba mweeeee lakin leo nimewahi nikanywa maziwa naona tumbo liko poa lakin nilikula kidogo tu
 
Me kama wewe zamani nilikua nayafakamia balaa siku hizi siyagusi kabisa maana nikila tu hizo gesi ntazotoa ni balaa. Nakaa mbali nayo kabisaa
 
Me kama wewe zamani nilikua nayafakamia balaa siku hizi siyagusi kabisa maana nikila tu hizo gesi ntazotoa ni balaa. Nakaa mbali nayo kabisaa
Yaan tumbo linakuwa kama kuna mtu anaendesha bajaji ndani [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…