Siku hizi Ligi za Ulaya hazina watazamaji wengi huku kwenye vibanda umiza

Siku hizi Ligi za Ulaya hazina watazamaji wengi huku kwenye vibanda umiza

Hapo umenena mkuu. Bongo tunajitahidi sana kwenye upande wa burudani

Ukiachana na mpira kuna kipindi nilikuwa siwezi sikiliza kabia Bongo Flava ila siku hizi najikuta siku nzima ni Bongo tu.
Bongo muziki tu kwingine mnadanganyana.

Tasnia ya burudani kiujumla, ukiacha mziki, bongo hata wakenya tu wametupiga parefu.
 
Siku hizi services za kustream ni nyingi. Na unaweza kustream mechi za ligi nyingi za nje hizi timu zetu ili ustream labda icheze michezo ya kimataifa.

So hapo mtu anayeweza kumudu bando hutamuona bandani.

Man City kuigeuza epl nyumbani kwake.

Kuwepo kwa madish cheap (canal +)

Location pia. Mfano kijiji nilipo haijalishi ni mechi gani watu hawajai, haijalishi ni mechi ya nje au ya ndani na hata awe anacheza nani.

Hawa canal + wangepata usajili rasmi Tz hawa dstv wangefunga virago
 
Hili jambo nililiongelea hapo kale 2014 to be exact..., AKA 10 Years Ago....; Hongera kwa Azam kwa kufanya nilichosema...

 
Kweli kabisa
Mechi nyingi za Ulaya zimejaa formation kuliko Raha za mpira zile zama za Gaucho Zizzou n.k hazipo unaenda kuangalia mpira ambao anauelewa kocha na wachambuzi we mtazamaji hupati kabisa rhythm ya mchezo
uzi ufungwe hapa umemaliza. nimeacha kuangalia pira la ulaya miaka dahari. ladha hakuna. ni maonyesho ya tattoo na vipaji less
 
Simba na yanga pia mara zote wanalia watu kujaa viwanjani. Ni teknolojia kukua, watu matokeo wanafatilia live

Pia kubet napo kumefanya wasiangalie sana. Zamani watu wanajazana kuangalia kuona ufundi ladha na kila burudani, lakini sasa hivi akili yote ya watu ipo kwenye mkeka utick tu
 
Baada ya Azam tv kuamua kuonyesha kila mechi ya Ligi Kuu ya NBC kwasasa Vibanda umiza vinajaza zaidi mechi za ligi ya NBC kuliko zile za Ulaya.

Mechi za Ulaya huko siku hizi hazina watazamaji wengi huku vibandani.

Coastal Union vs Yanga inaweza ikajaza ukumbi halafu huku Arsenal Vs Liverpool watazamaji wanahesabika ukumbini.

Sokoni DStv kwasasa ana hali mbaya, Watanzania wanapenda ligi yao inayooneshwa AzamTv kuliko ligi za Ulaya zinazooneshwa na DStv.
Watazamaji wa EPL wamehamia kuangalizia kwenye simu maana hio competition ya TV bandani ni dhidaa. EPL Au NBC wengi waachiwe TV
 
Ushabiki ulikuwepo zamani, enzi hizo mnafuta mechi za UEFA Kijiji mpaka Kijiji tena saa Tano usiku hakuna betting Wala nini soka lilikuwa rohoni. Michuano ya AFCON ndio ilikuwa balaa, siku hizi wazee wa kubett ndio mashabiki wa soka. Makampuni ya kubett yametuharibia mpila wetu.
 
Back
Top Bottom