Mpemba Mimi
JF-Expert Member
- Jul 6, 2013
- 1,656
- 2,483
Sababu ni kuwa mechi zetu ni za ukweli,na matokeo ni ya ukweli, hizo nyingine inategemeana na watu walivyo-bet....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwanini Englanda haifanyi vizuri EURO na haichukui kombe la Dunia? Jibu utalopata ndo hilohilo kwa Tanzania.Kwa nini AFCON hatufanyi vizuri?
Kwa nini hatuchukui ubingwa CAF?
Siyo kuangalia tu, quality ni muhimu. Bongo movies bado sana na sioni dalili za mageuzi leo wala kesho, ni TAKATAKA kabisa.Mbona movies za Ulaya na Marekani bado mnaangalia badala ya kuangalia bongo movies tu??
Hiyo siyo sababu, football ina utamaduni wake, kukutana pamoja kuangalia na washakaji...hilo limepungua siku za karibuni limebaki kwa ligi ya ndani tu. Kipimo tosha ni siku kuwe na mechi ya Man U, Arsenal, City, Madrid au Barca alafu siku hiyohiyo kuwe na mechi ya Simba au Yanga then watu haohao unaosema wanaangalia kwenye sim utakutana nao mabanda umiza na masinagogi wakifatilia mechi za ndani na si za ulaya! Mambo yamebadilika.Hoja hapo ni kuwa ligi nyingi za ulaya unaweza kutazama kupitia simu yako tena free bila sijui vifurushi ni Mb zako tu chanel nyingi zinaonesha ligi hizi kuliko hiyo ligi yako unayojisifu nayo
Kwamba wakenya wametupita parefu hata kwenye football!? Bilashaka umelewaBongo muziki tu kwingine mnadanganyana.
Tasnia ya burudani kiujumla, ukiacha mziki, bongo hata wakenya tu wametupiga parefu.
Hili lina uhalisia.Tatizo kuu la watu kutovutiwa na ligi za Ulaya kwasasa ni masuala mazima ya BETTING!
BETTING imekuja kuondoa Radha ya mpira hasa timu kubwa za Ulaya!
BETTING NDIYO SABABU KUU
Una ujuaji mwingi, unahisi ukijitofautisha na wenzako utaonekana mjanja ila ukweli unabaki palepale we ni mshamba tu. Hilo soccer la Ulaya ndo limeharibika kabisa watu wanacheza kama maroboti hakuna ubunifu wala mvuto wowote! Kifupi sayansi ya mpira imeharibu mpira na hilo limewaathiri sana Ulaya so wabingi wengi wamebaki na team zao za nyumbani ambako angalau mpira bado unachezwa kwa misingi yake ya zamani japo napo tunaelekea kulekule walipo ulaya.Wanaofuatilia mpira wa bongo ,80% hawajui mpira ni ile tu sababu azam media imerahisisha access ya kutazama mechi hizo na pia wasipitwe na mabishano yanayoendelea mtaani.
Angalia hao mashabiki wa mpira wa bongo kina mama na wadada shazi hawajui lolote ni ile tu ushabiki wa na mimi nimo.
Mpira wavbongo hapana sijawahi kuwa na mzuka nao kabisa maana ni vichekesho, pasi inapigwa kwasababu mtu yupo mbele na magoli si yakutegenezwa bali sababu tumefika golini basi ww piga tu[emoji23], yaani mpira hauna mbinu kabisa mchezaji anapiga krosi iingie ndani sio kwasababu kamuona mtu ila anapiga tu watu wagombanie tu mpira au shoot unaona linapaa juu anapiga kokote tu yaani ni kubahatisha kulenga goli.
Kuna siku niliona George ambagile anachambua match za bongo sijui ilikua mashujaa na tanzania prison , nikaona kabisa anatupiga fix et sijui mashujaa wakiwa na mpira wanacheza sijui 4 42 wakiwa hawana mpira sijui wanabadilisha mfumo sijui 3 2 3 nini sijui kitu ambacho si kweli , team nyingi za bongo zinacheza mpira ili mradi hakuna mbinu yoyote ile inatumika.
Japo kuna kipindi niliangalia baadhi ya mechi nikashangaa mpira waliocheza ulikus mzuri niliona kama maajabu mpira huo kuchezwa bongo , kuna mwaka simba vs alhaly na hata juzi juzi yanga vs waarabu walishinda 4 ile na baadhi ya mechi chache chache.
Kwa mbaali kidogo yanga anajitahidi hata pasi na possession play unaona kuna mpira anacheza hasa last season .
Hii ni kweli. Wale wa Chelsea, Barca m Man U na Arsenal hawana nguvu za kwenda kucheki mechi.Timu kubwa zimeyumba ulaya,watu wamezisusa.
1)Man u angekuwa anafunga watu
2) Arsenal ubingwa mara moja moja
3) Barcelona angekuwa wa moto kama motoalio nao sasa,maana El clasico hii ndio ilikuwa na vibe kabla ya mechi
Watu timu zao wamezikimbia ulaya kwa matokeo mabovu
Hata story zao ni zile zile tu. Mapenzi na uchawi, huwa hawatoki nje ya hapo. Lakini story za movie za mbele angalao zipo creative yaani unacheki movie unakutana na story mpya kabisa kichwani mwako.Siyo kuangalia tu, quality ni muhimu. Bongo movies bado sana na sioni dalili za mageuzi leo wala kesho, ni TAKATAKA kabisa.
Kwamba wakenya wametupita parefu hata kwenye football!? Bilashaka umelewa
Yaani unamuongelea mitrovic aingie kwenye tuzo yoyote ya dunia uko serious😂 , huyo mitrovic kacheza epl na hakuna alichofanya .Mpira wa Ulaya umekuwa science sana wachezaji wamekuwa robots
Haya Rodri kabeba balon mbele ya kina Martinez Vini n.k lakini ukiangalia huoni hata uchezaji wa sanaa ya mpira ndani ni aghalabu kusikia mtoto akisema ndoto yake ni kuwa kama Rodri
Ukiangalia ligi kama ya Roshn Saudia Kuna mtu kama Mitrovic husikii akitajwa ila jamaa anafanya mpira uonekane kitu kizuri ila sababu hayuko Ulaya humsikii kwenye tuzo yoyote ya dunia
Mpira upi unaongelea ambao bongo wamebaki nao , bongo hakuna mpira na hakujawahi kuwa na mpira.Una ujuaji mwingi, unahisi ukijitofautisha na wenzako utaonekana mjanja ila ukweli unabaki palepale we ni mshamba tu. Hilo soccer la Ulaya ndo limeharibika kabisa watu wanacheza kama maroboti hakuna ubunifu wala mvuto wowote! Kifupi sayansi ya mpira imeharibu mpira na hilo limewaathiri sana Ulaya so wabingi wengi wamebaki na team zao za nyumbani ambako angalau mpira bado unachezwa kwa misingi yake ya zamani japo napo tunaelekea kulekule walipo ulaya.
Baada ya Azam tv kuamua kuonyesha kila mechi ya Ligi Kuu ya NBC kwasasa Vibanda umiza vinajaza zaidi mechi za ligi ya NBC kuliko zile za Ulaya.
Mechi za Ulaya huko siku hizi hazina watazamaji wengi huku vibandani.
Coastal Union vs Yanga inaweza ikajaza ukumbi halafu huku Arsenal Vs Liverpool watazamaji wanahesabika ukumbini.
Sokoni DStv kwasasa ana hali mbaya, Watanzania wanapenda ligi yao inayooneshwa AzamTv kuliko ligi za Ulaya zinazooneshwa na DSt
Ungetuambia na maeneo ulipo!Baada ya Azam tv kuamua kuonyesha kila mechi ya Ligi Kuu ya NBC kwasasa Vibanda umiza vinajaza zaidi mechi za ligi ya NBC kuliko zile za Ulaya.
Mechi za Ulaya huko siku hizi hazina watazamaji wengi huku vibandani.
Coastal Union vs Yanga inaweza ikajaza ukumbi halafu huku Arsenal Vs Liverpool watazamaji wanahesabika ukumbini.
Sokoni DStv kwasasa ana hali mbaya, Watanzania wanapenda ligi yao inayooneshwa AzamTv kuliko ligi za Ulaya zinazooneshwa na DStv.