Siku hizi ukikutana na mtu ambae hukumchangia harusi yake basi utakuta hakuchangamkii kama zamani

Siku hizi ukikutana na mtu ambae hukumchangia harusi yake basi utakuta hakuchangamkii kama zamani

Mwambie aache ujinga. Suala la kuwezesha harusi ni jukumu lake mwenyewe, wazazi na ndugu zake na si kila mtu kiasi cha kuanza kuwachukia wasiotoa.

Sisi majirani na marafiki si jukumu letu.
 
Skuizi hii nchi imeshakuwq na mambo mengi ya kijinga sana aiseee....
 

Attachments

  • downloadfile-23.jpg
    downloadfile-23.jpg
    39.6 KB · Views: 2
Wanatukosea sana kutudai michango swala la harusi ni wao ndio wanapanga waoane lini wanatakiwa wajiandae kwa kila kitu hii ni michango ni kutafutana lawama tu
Kabisa mkuu afu usipochangia wanaona kama wewe sio rafiki wa kweli wakati suala la kuoa sio dharula
 
Ndio uhalisia, michango ya harusi ndio kipimo cha upendo. Japo naelewa kwa wengi hiyo ndo moment yao kubwa lakini kuifanya kuwa ni lazma kwa watu wao wa karibu pasipo kuangalia hali zao. Si sawa
Kabisa kaka wanatuhukumu bure sio kwamba hatupendi kuchangia ila hali ngumu afu kiasi wanachopanga mtu achangie sio rafiki unakuta single 50000 double 100000 afu wengine kipato chetu 150000 kwa mwezi inasikitisha
 
Naitwa fake friend huku mkuu
Sema kama una pesa jaribu kutoa '' usiache mbachao kwa msala upitao ''

Kwa ishu za kupita ni vyema ukajitoa , maana kuna mengi sana ya kusaidia ..Onyesha umuhimu pale mtu anapohitaji msaada wako kama unao uwezo ..
 
Back
Top Bottom